Jumatano, 15 Rajab 1446 | 2025/01/15
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Wilayah Tunisia: Press Conference on the Penal Policy of the State towards Hizb ut Tahrir

Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia:

Mkutano na Wanahabari kuhusu Sera ya Adhabu ya Serikali kwa Hizb ut Tahrir

(Imetafsiriwa)

Mnamo Alhamisi, 01/06/2023, Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia ilifanya mkutano na waandishi wa habari katika makao makuu yake huko Ariana chini ya kichwa: "Sera ya adhabu ya serikali kwa Hizb ut Tahrir: Je, ubaguzi utaendelea hadi lini?"

Mkutano huo na waandishi wa habari ulianza kwa ujumbe wa Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Tunisia, Ustadh Khabib Kerbaka, ambapo aliwatambulisha wajumbe wa Kamati ya Ulinzi ya Hizb ut Tahrir, na kuzungumzia mbinu iliyopitishwa na utawala wa Tunisia kuwahangaisha ٍMashababu wa Hizb ut Tahrir, hasa baada ya Julai 25, wakikumbuka asili ya kazi ya kisiasa ya Hizb ambayo inalenga kuubadilisha utawala na kuikomboa nchi kutoka kwenye nira ya ukoloni na kuuokoa Ummah, ikiwa ni pamoja na watu wa Tunisia, kutokana na migogoro iliyokusanyika kwa kurejesha mamlaka ya Uislamu kikamilifu na bila kupunguzwa, ambayo ni tishio kwa dola za Magharibi na kuwafanya vibaraka wake nyumbani, vibaraka tu ambao dori yao imefungwa katika kuvuruga shughuli za wafanyikazi wanaofanya kazi ya kuregesha tena maisha kamili ya Kiislamu.

Ama kuhusu machangio wa mwisho, ulifanywa na Wakili Imad Eddin Haddouk, ambapo alitoa takwimu rasmi na tarakimu kuhusu idadi ya waliokamatwa katika safu ya Hizb ut Tahrir katika miaka ya hivi karibuni, ambapo alithibitisha kuwa kulikuwa na kesi 69 zilizofutiliwa mbali kutoka 2015, ambapo Mashababu walikamatwa na kuhukumiwa na kutosikilizwa kwa kesi hizo isipokuwa kesi 7 ambazo zinazingatiwa, kwa sababu haiwezekani kuwashtaki watu kwa tuhuma zinazoelekezwa dhidi ya mtu mwenye maadili, ambayo ni haiba ya Hizb ut Tahrir katika suala la kesi, tofauti na ilivyotokea kwa Shab, Adel Al-Ansari huko Nabeul, ambayo ni kashfa ya kisheria na ya kihistoria kwa viwango vyote. Imad Eddin Haddouk aliuliza kuhusu kiwango cha kisayansi cha hakimu aliyetoa uamuzi huo katika Mahakama ya Mwanzo ya Nabeul, akiomba uthibitisho wa cheti chake cha kisayansi.

Pia, watu 90 wametiwa mbaroni tangu mwaka 2015 hadi leo, ambapo rufaa hiyo ilipelekwa kwenye Mashtaka ya Umma na kisha kwenye nguzo ya kupambana na ugaidi, na wote waliachiliwa huru, jambo ambalo ni dalili tosha ya kushindwa kwa utawala huo kuambatanisha tabia ya kigaidi kwa masuala ya Mashababu wa Hizb ut Tahrir, kwa sababu wao ni washupavu katika kazi ya kisiasa ya kifikra mbali na aina zote za kazi ya kimwili. Bali, ni ushahidi wa ziada wa kufilisika kifikra kwa dola ya kisasa ambayo watawala wake hawana uwezo wa kukabiliana kifikra na kisiasa kwa mdahalo na Hizb ut Tahrir. Kwa hivyo, Ust. Haddock alirudia wito wake wa kufungua milango ya mjadala na majadiliano kuhusu chama chenye uwezo mkubwa wa kuiondoa nchi na watu wake kutoka katika hali ya utegemezi, mateso, na taabu inayoletwa na utekelezaji wa urasilimali nchini Tunisia.

Kuhusu kesi hizo, Ustadh Haddouk alieleza kuwa kuna rufaa ya mahakama ya kijeshi ya Tunis na nyingine ya Sfax, huku mahakama za kiraia zikiwamo Tunis 1, Tunis 2, Ariana, Ben Arous, Manouba, Bizerte, Nabeul, Majaz al-Bab, Beja, Jendouba, Sousse, na Mahdia, Sidi Bouzid, Kairouan, Sfax, Gabes na Tozeur.

Kwa njia hii, anathibitisha bila ya shaka yoyote kwamba kuna ulengaji wa kimfumo wa wanachama wa Hizb ut Tahrir ili kuwabughudhi mbele ya mahakama na kuwafuata kimahakama kwa tuhuma dhaifu, na kwamba kila mtu anahusika katika njia hii ya kisiasa isipokuwa kwa rehema ya Mola wangu Mlezi, kuanzia manispaa na serikali na mpaka Wizara ya Mambo ya Ndani na Wizara ya Sheria, Kwa hiyo, kukabiliana kibaguzi na Hizb ut Tahrir ni sera ya serikali.

Ama zile zinazoitwa jumuiya ya kiraia, ni sehemu ya njama chafu dhidi ya watetezi wa Khilafah, ambapo kauli mbiu zote za uhuru, demokrasia na haki za binadamu huisha, mara tu inapokuja kwa Hizb ut Tahrir.

2023 06 01 TNS NADWA POSTER

Kalima ya Ustadh Abdul Raouf Al-Ameri Mkuu wa Afisi ya Kisiasa ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia Pembezoni mwa Amali ya Semina kwa Wanahabari

Alhamisi, 12 Dhu al-Qa’adah 1444 H – 01 Juni 2023 M

Kwa maelezo zaidi tafadhali zuru mitandao ya Hizb ut tahrir / Wilayah Tunisia:

Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia

Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia

Tovuti Rasmi ya Jarida la Al-Tahrir

Ukurasa wa Facebook wa Jarida la Al-Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu