- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia:
Nusra kwa Wafungwa wa Dhamiri nchini Uzbekistan!
Kushiriki kwa Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia katika amali za kampeni ya kilimwengu iliyozinduliwa na Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir kwa kichwa,
“Enyi Ummah; Kilio Wanacholia Wafungwa wa Dhamiri nchini Uzbekistan!”
ni kwa ajili ya kuwanusuru ndugu na dada zetu wafungwa wa kisiasa katika magereza maovu ya Uzbekistan si kwa jengine isipokuwa kwa kusema kwao, Mola wetu Mlezi ni Mwenyezi Mungu.
Hakika vita dhidi ya Uislamu, hata vikichukua sura nyingi, vina adui yule yule kila mahali, adui ambaye amedhihirika waziwazi na hafichi tena chuki na ghadhabu yake, na anatekeleza viwango viwili vya uongo na uzushi kwa Uislamu na Waislamu.
Licha ya mateso tunayoyapata kutokana na yale yanayowapata ndugu zetu wa Gaza na madhehebu ya Mayahudi ambao wamekuwa wabaya kwa muda mrefu, dhalimu wa Uzbekistan anajitokeza dhidi yetu kwa kuwakamata mashababu wa Hizb ut Tahrir na kuwatishia kwa vitendo vya ukandamizaji ni yale yale waliyoshtakiwa kwayo na Karimov aliyekufa, na ambayo walifungwa kwa karibu miaka ishirini, mashtaka ya kubuni ambayo hayana ushahidi.
Hizb ut Tahrir katika Asia ya Kati, hasa katika Bonde la Fergana, ambako kunapatikana Uzbekistan, Kazakhstan, na Tajikistan, ilikuwa na athari kubwa katika kurudi kwa Waislamu kwenye dini yao baada ya uhamisho waliopata wakati wa Muungano wa Sovieti kutokuwa na ushindani mkali kutoka kwa makundi ya Kiislamu, hivyo wafuasi wake waliongezeka, hasa miongoni mwa vijana, jambo ambalo lilisababisha hofu kwa madhalimu nje ya nchi na nyumbani, hivyo wakampa mtumishi wao Mirziyev kazi ya kuwakamata mashababu wa Hizb ut Tahrir na kuwatupa kwenye magereza hadi mabwana zao wa Urusi na Marekani, maadui wa Uislamu na Waislamu waliporidhika.
Na sisi tunatuma kutoka Tunisia ujumbe kwa ndugu zetu, tukishikana mikono nao imara na kumuomba Mwenyezi Mungu awajaalie uthabiti, ushindi, na uhuru kutoka katika kifungo, na tunawaambia: Tumekutana kutoka kwa marehemu Ben Ali katika miaka ya tisiini, dhulma na ukandamizaji na Ben Ali ameondoka na Hizb ut Tahrir imebakia, kama vile Karimov amekwenda na Hizb ut Tahrir imebakia, kwa hiyo subirini mpaka madhalimu wote wa dunia watoweke na ubakie Uislamu na Waislamu.
Jumatatu, 09 Muharram 1446 H sawia na 15 Julai 2024 M
Matembezi ya Ijumaa ya kuinusuru Palestina na kuwanusuru wabebaji Da’wah nchini Uzbekistan
Wakati wa matembezi ya kila wiki katika mji mkuu, Tunis, yaliyoandaliwa na Hizb ut Tahrir/Wilayah ya Tunisia, kuwanusuru watu wetu katika Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina), mabango ya kuwaunga mkono ndugu zetu wanaodhulumiwa nchini Uzbekistan yalibebwa na waliohudhuria katika muda wote wa matembezi hayo kutoka mbele ya Msikiti wa Al-Fatah katika mji mkuu hadi barabara ya Al-Thawra, yakivutia hisia za watu wa Tunisia kwamba utawala wa Mirziyev nchini Uzbekistan warudia tena njia ya Karimov aliyekufa katika kuwatesa mashababu wa Hizb ut Tahrir na uadui wake kwa Uislamu, na kwa kuwa Ummah wa Kiislamu ni umma mmoja, kama alivyosema Mwenyezi Mungu إِنَّ هَذِهِ أُمَّتُكُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً وَأَنَا رَبُّكُمْ فَاعْبُدُون “Kwa hakika huu umma wenu ni umma mmoja, na Mimi ni Mola wenu Mlezi. Kwa hivyo niabuduni Mimi.” [Al-Anbiya 21:92] na kama Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alivyosema, "مثل المؤمنين في توادهم وتراحمهم وتعاطفهم مثل الجسد إذا اشتكى منه عضو تداعى له سائر الجسد بالسهر والحمى" “Mfano wa waumini katika kupendana na kuhurumiana kwao ni kama mfano wa mwili: pindi kiungo kimoja kikilalamikia maumivu, mwili mzima hujibu kwa kukosa usingizi na homa” na kama alivyosema katika Hadith nyengine, "من لم يهتم بأمر المسلمين فليس منهم" “Yeyote asiyejali mambo ya Waislamu si katika wao.” Ni wajibu kwa Waislamu wote kuwanusuru ndugu zao katika kila sehemu ya ardhi bila kuzingatia rangi zao, nasaba zao na lugha zao na hili lawajibisha kufanya kazi ya kusimamisha dola Khilafah itakayolinda heshima ya Waislamu, damu yao, na dini yao, na kukomesha unyanyasaji wa watawala madhalimu wahalifu kwa kila Muislamu anayesema “Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu”.
Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Tunisia
Ijumaa, 06 Muharram Tukufu 1446 H sawia na 12 Julai 2024 M
Ujumbe kutoka Afisi ya Habari na Kamati ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia wapeleka barua kwa Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Tunisia kuhusu Uzbekistan
Ijumaa, 06 Muharram 1446 H sawia na 12 Julai 2024 M
Ujumbe kutoka Afisi ya Habari na Kamati ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia wapeleka barua kwa Shirika la Waandishi wa Habari kuhusu Uzbekistan
Ijumaa, 06 Muharram 1446 H sawia na 12 Julai 2024 M
Jumbe na Kalima za Kuwanusuru Wafungwa wa Dhamiri nchini Uzbekistan
Ujumbe wa Dharura kutoka kwa Mashababu wa Tunisia Kuhusu ukandamizaji mkali wa Wabebaji Da'wah nchini Uzbekistan
(1)
Ijumaa, 20 Muharram 1446 H sawia na 26 Julai 2024 M
Ujumbe wa Dharura kutoka kwa Mashababu wa Tunisia Kuhusu ukandamizaji mkali wa Wabebaji Da'wah nchini Uzbekistan
(2)
Ijumaa, 20 Muharram 1446 H sawia na 26 Julai 2024 M
Ujumbe kupitia njia ya Mashababu wa Kuwanusuru Ndugu zao na Dada zao nchini Uzbekistan
Ijumaa, 06 Muharram 1446 H sawia na 12 Julai 2024 M
Kalima ya Kitengo cha Wanawake katika Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia
ya Kuwanusuru Ndugu na Dada zao katika Magereza ya Uzbekistan
(1)
Jumamosi, 07 Muharram 1446 H sawia na 13 Julai 2024 M
Kalima ya Kitengo cha Wanawake katika Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia
ya Kuwanusuru Ndugu na Dada zao katika Magereza ya Uzbekistan
(2)
Jumamosi, 07 Muharram 1446 H sawia na 13 Julai 2024 M
Angazo la Picha la Sehemu ya Amali za Kampeni
https://hizb-ut-tahrir.info/sw/index.php/dawah/tunisia/4106.html#sigProId78b636c72f
Angazo la Vyombo vya Habari la Amali za Kampeni
https://hizb-ut-tahrir.info/sw/index.php/dawah/tunisia/4106.html#sigProIdc3b144ecdd
Alama Ishara za Kampeni
#صرخة_من_أوزبيكستان
#PleaFromUzbekistan
#ЎЗБЕКИСТОНДАН_ФАРЁД
Kwa maelezo zaidi tafadhali zuru mitandao ya Hizb ut tahrir / Wilayah Tunisia:
Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia
Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia