- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia:
Matembezi ya Takbira kutoka Tunisia hadi Palestina!
Katika siku ya nane ya Dhu al-Hijjah (Siku ya Tarwiyah), Hizb ut-Tahrir / Wilayah ya Tunisia iliadhimisha Sunnah ya Takbira katika mji mkuu, Tunis, kwa kuandaa matembezi makubwa yenye kichwa “Matembezi ya Takbira kutoka Tunisia hadi Palestina.” yalianza baada ya Swala ya Ijumaa mbele ya Msikiti wa Al-Fath, nayo ni matembezi ya 37 mfululizo, tangu kuanza kwa Kimbunga cha Al-Aqsa, ambayo yaliitishwa na Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Tunisia, watu wa Al-Zaytouna, yaliyohudhuriwa na umati mkubwa wa watu, ambapo walizunguka katika barabara za mji mkuu hadi Barabara ya Al-Thawra yakishuhudiwa na kuungwa na wapita njia na wamiliki wa maduka kwa namna chanya, wakiimba, wakipiga takbir, na tahlil na wakainua mabango mawili makubwa, bango kuu likiwa na limeandikwa kichwa cha matembezi hayo, huku mengine yakiwa na takwimu za mashahidi na waliojeruhiwa, kama ambavyo watoto, wanawake na wanaume pia walinyanyua makumi ya mabango yaliyosomeka, “Mwenyezi Mungu ni Mkubwa, Enyi Majeshi ya Waislamu,” “Mwenyezi Mungu ni Mkubwa, Enyi Wanazuoni wa Kiislamu,” “Mwenyezi Mungu ni Mkubwa, Enyi Vijana wa Kiislamu,” “Mwenyezi Mungu ni Mkubwa, Enyi Umma wa Kiislamu,” na “ Rafah inaomba Nusra kwa Majeshi ya Waislamu,” ambapo wahudhuriaji walipaza sauti wakati wote wa matembezi: “Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar, La ilaha illa Allah, Allahu Akbar, Allahu Akbar wa lillah al-hamd. Allahu Akbar kabira, wa al-hamdulillah kathira, wa subhanallah bukratan wa aswila, La ilaha illa Allah wahdahu, swadaqa abdahu, wa naswara abdahu, wa aaza jundahu, wa hazama al-ahzab wahdahu. La ilaha illah Allah, wala naabudu illah iyyahu mukhliswina lahu al-dina walau kariha al-kafirun”
wakafika katika barabara ya Al-Thawra. Matembezi hayo yalitamatika kwa kalima iliyotolewa na mwanamke kutoka Tunisia kutoka kitengo cha wanawake wa Hizb ut Tahrir/ Wilayah Tunisia, mbele ya ukumbi wa michezo wa manispaa, aliwakumbusha watu wa Tunisia kuhusu jeraha la damu la Gaza na kwamba “yeyote anayepambauka na ilhali hajali mambo ya Waislamu si miongoni mwao,” kama alivyosema Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) na juu ya ulazima wa majeshi kusonga, kuangusha viti vya utawala, na jihad kwa ajili ya Mwenyezi Mungu... na kwamba kadhia hii leo ni kadhia ya itikadi ambayo ni vita kati ya Uislamu mtukufu na ukafiri, na kwamba mkuu wa dola za kikafiri ni Marekani pia akatoa wito wa kuwepo na khutba ya kutangaza Khilafah iwe ya nne baada ya khutba ya Ijumaa, khutba ya Arafa, na khutba ya Idd... Pia, mmoja wa mashababu wa Hizb aliimba kauli mbiu “Umma unataka kupinduliwa viti vya utawala” na “Umma unataka kuhamasishwa majeshi.” “Umma unataka kutangazwa jihad,” jambo ambalo wahudhuriaji waliokuwa nyuma yake waliliimba kwa shauku na hamu kubwa, matokeo yake ulinzi ulimkamata shababu huyo mbele ya watoto wake na mkewe na kumpeleka kwenye kituo cha usalama ambako alihojiwa kuhusu kauli mbiu hizi ambazo ziliikasirisha serikali... Hivyo, Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Tunisia inaendelea kuinusuru Gaza, haijali kukamatwa au kufuatiliwa kwa mashababu wake mfululizo, jambo ambalo litaongeza tu uimara na azma yao tukimuomba Mwenyezi Mungu aharakishe kuangushwa kwa watawala wabaya na kusimamishwa jengo tukufu la Uislamu, Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, itakayoikomboa Masra ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), na nchi za Kiislamu zilizobakia ((وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ، بِنَصْرِ اللَّهِ ۚ يَنصُرُ مَن يَشَاءُ ۖ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ )) “Na siku hiyo Waumini watafurahi. Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.” [Al-Rum: 4-5]
Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Tunisia
Ijumaa, 08 Dhu al-Hijjah 1445 H sawia na 14 Juni 2024 M
- Sehemu ya Amali ya Matembezi -
https://hizb-ut-tahrir.info/sw/index.php/dawah/tunisia/4034.html#sigProIdd686879277
- Alama Ishara za Amali -
#طوفان_الأقصى
#الجيوش_إلى_الأقصى
#الأقصى_يستصرخ_الجيوش
#AksaTufanı
#OrdularAksaya
#ArmiesToAqsa
#AqsaCallsArmies
Kwa maelezo zaidi tafadhali zuru mitandao ya Hizb ut tahrir / Wilayah Tunisia: