Jumapili, 26 Rajab 1446 | 2025/01/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia:

Matembezi ya Ukombozi: “Enyi Jeshi la Algeria: Gaza inahitaji Misafara na Vifaru, sio Ujenzi wa Hospitali!”

Matembezi ya 46 mfululizo yalifanyika tangu kuanza kwa Vita vya Kimbunga cha Al-Aqsa, yakianzia mbele ya Msikiti wa Al-Fatah katika mji mkuu wa Tunis, hadi barabara ya Al-Thawra, ambayo yaliitishwa na Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Tunisia kwa watu wa Al-Zaytouna kuwanusurur watu wa Palestina na Al-Aqsa iliyo mateka, na kichwa chake kilikuwa “Enyi Jeshi la Algeria: Gaza inahitaji Misafara na Vifaru, sio Ujenzi wa Hospitali!” na kama kawaida matambezi haya yalihudhuriwa na umati mkubwa wa watu wa Tunisia ya kijani kibichi, yalizunguka katika barabara za mji mkuu zinazoelekea Barabara ya Al-Thawra, ambapo wahudhuriaji waliimba kauli mbiu, ya muhimu zaidi ikiwa: “Enyi Enyi maafisa wa jeshi la Algeria, jibuni vilio vya wanawake” “Enyi nchi ya mamilioni ya mashahidi nyanyueni bendera ya Tawhid,” “Jihad, jihad na majeshi yako tayari” waliinua mabango bango kuu likiandikwa kichwa cha matembezi hayo, na jengine idadi ya mashahidi, na kwenye mabango mengine, “Enyi, jeshi la Tunisia, mlango wa Magharibi unakusubirini,” “Enyi jeshi la Waislamu, Mtume wa Mwenyezi Mungu anakuiteni,” “Enyi, jeshi la Algeria, Kamanda Barbarossa anakuiteni.” Matembezi yalikamilika kwa kalima iliyotolewa na mmoja wa mashababu wa Hizb ut Tahrir aliyelaani na kukashifu kauli za Rais Tebboune wa Algeria wakati wa kampeni zake za uchaguzi, ambapo aliwaahidi watu wa Gaza kuhamasisha jeshi lake kujenga hospitali nchini Palestina inayokaliwa kwa mabavu, na sio kuliangamiza umbile la Kiyahudi kwa mizinga na ndege zake, alitoa wito kwa maafisa wanyoofu na askari katika jeshi la Algeria kurekebisha haraka mapungufu yao katika kuinusuru Gaza na wajibu wa kutaharaki kwao maramoja kusitiri hadhi yake kama jeshi lenye kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu kwani wao ni wajukuu wa  Mujahidina na wafunguzi, Barbarossa na Arrog...

Hizb ut Tahrir haifungwi na mipaka ya Sykes-Picot na ulinganizi wake hauzuiliwi na watawala vibaraka waovu, inawalingania na kuyaliliwa majeshi yenye ikhlasi ya Umma katika kila sehemu ya dunia mpaka Mwenyezi Mungu atakaporuhusu nusra yake na kusimamishwa Dola ya Kiislamu, Khilafah Rashida ya pili iliyoahidiwa, yenye kuondoa giza hili na kuangaza ulimwengu kwa nuru za hukmu tukufu za Uislamu.

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Tunisia

Ijumaa, 18 Safar Al-Khair 1446 H sawia na 23 Agosti 2024 M

- Angazo la Video la Amali ya Matembezi -

[Enyi Jeshi la Algeria: Gaza inahitaji Misafara na Vifaru, sio Ujenzi wa Hospitali!]

- Sehemu ya Amali ya Matembezi -

- Alama Ishara za Amali -

#طوفان_الأقصى

#الجيوش_إلى_الأقصى

#الأقصى_يستصرخ_الجيوش

#AksaTufanı

#OrdularAksaya

#ArmiesToAqsa

#AqsaCallsArmies

Kwa maelezo zaidi tafadhali zuru mitandao ya Hizb ut tahrir / Wilayah Tunisia:

Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia

Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia

Tovuti Rasmi ya Jarida la Tahrir

Ukurasa wa Facebook wa Jarida la Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu