Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

The Netherlands March in Amsterdam  Stop the Genocide in Gaza

Hizb ut Tahrir / Uholanzi:

Matembezi ya Amsterdam “Komesheni Mauaji ya Halaiki Mjini Gaza”

Mbele ya matendo ya kishujaa yaliyofanywa na Mujahidina mashujaa katika Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina) chini ya kauli mbiu ya (Kimbunga cha Al-Aqsa) dhidi ya umbile nyakuzi la Kiyahudi ambalo linaendelea na shambulizi lake dhidi ya Msikiti uliobarikiwa wa Al-Aqsa na kuzingirwa kwake na mashambulizi ya mara kwa mara ya mabomu kwa Ukanda wa Gaza kwa miaka 17, na mbele ya mauaji ya kikatili yaliyofanywa na umbile hili halifu katika kipindi cha miaka saba iliyopita dhidi ya Waislamu wasio na ulinzi katika Ukanda wa Gaza, ambayo yamesababisha kuuawa shahidi na kujeruhiwa kwa Waislamu zaidi ya 115,000 wanaume na wanawake, Hizb ut Tahrir / Uholanzi iliandaa maandamano katika mji mkuu wa Uholanzi, Amsterdam, kuinusuru Gaza, yenye kauli mbiu “Komesheni Mauaji ya Halaiki Mjini Gaza.” Maandamano hayo yalizunguka mitaa ya Amsterdam, yakisindikizwa na nyimbo za vijana wakitaka kunusuriwa kwa Gaza na kuhamasishwa kwa majeshi ya Waislamu. Katika matembezi hayo, wakaazi wengi wa vitongoji vilivyo karibu na njia ya matembezi hayo na idadi ya watu wasiokuwa Waislamu walijiunga nayo, huku baadhi ya wamiliki wa maduka wakianza kuimba kauli mbiu za maandamano hayo. Yalipofika kituo cha mwisho, Ndugu Kamal Abu Zaid alisimama na kusoma aya za wazi kutoka Kitabu cha Mwenyezi Mungu, na kisha akatoa Ndugu Mikael Hassan na Ustadh Okay Balla, Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir nchini Uholanzi, wakatoa kalima fupi kuhusu hali ya kusikitisha ya Gaza na mauaji yanayofuatana nayo, uharibifu na njaa ambayo yamekaribia kuua maelfu ya watu wetu huko kwa upande mmoja, na kwa upande mwingine, uthabiti usio na kifani, imani, subira, na tawakkul ambayo watu wa Gaza wameonyesha kutoka kwa waumini wa mwanzo, pamoja na usaliti na njama zinazoambatana na watawala wa Waislamu na ushirikiano wa serikali za Magharibi ambazo zinashiriki kikamilifu na Mayahudi katika uhalifu wao kwa kuwapa silaha, askari, mipango, nk.

Jumapili, 04 Dhu al-Qa’adah 1445 H sawia na 12 Mei 2024 M

#طوفان_الأقصى

#الجيوش_إلى_الأقصى

#الأقصى_يستصرخ_الجيوش

#ArmiesToAqsa

#AksaTufanı

#OrdularAksaya

Aqsa_calls_armies#

#AqsaCallsArmies

Kwa Maelezo zaidi, Tafadhali Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Uholanzi:

Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Uholanzi

Facebook: Hizb ut Tahrir / Uholanzi

Twitter: Hizb ut Tahrir / Uholanzi

Instagram: Hizb ut Tahrir / Uholanzi

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu