Jumapili, 26 Rajab 1446 | 2025/01/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Uholanzi:

Matembezi mjini Amsterdam “Miaka 75, na Mwaka Mmoja wa Mauaji ya Halaiki mjini Gaza!”

Mbele ya matendo ya kishujaa yaliyofanywa na Mujahidina mashujaa katika Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina) chini ya kauli mbiu ya (Kimbunga cha Al-Aqsa) dhidi ya umbile nyakuzi la Kiyahudi ambalo linaendelea na shambulizi lake dhidi ya Msikiti uliobarikiwa wa Al-Aqsa na kuzingirwa kwake na mashambulizi ya mara kwa mara ya mabomu kwa Ukanda wa Gaza kwa miaka 17, na mbele ya mauaji ya kikatili yaliyofanywa na umbile hili halifu katika kipindi cha miaka saba iliyopita dhidi ya Waislamu wasio na ulinzi katika Ukanda wa Gaza, ambayo yamesababisha kuuawa shahidi na kujeruhiwa kwa Waislamu zaidi ya 150,000 wanaume na wanawake, Hizb ut Tahrir / Uholanzi iliandaa matembezi katika mji mkuu wa Uholanzi, Amsterdam, kwa mnasaba wa kupita mwaka mmoja kamili wa vita vya mauaji ya Halaiki dhidi ya Waislamu wa mji wa Gaza Hashem, kunusuru na kuiombea nusra na Izza Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina) na Gaza, kauli mbiu yake ni:

“Miaka 75, na Mwaka Mmoja wa Mauaji ya Halaiki mjini Gaza!”

Basi kuweni pamoja nasi...

Jumapili, 10 Rabi’ ul-Akhir 1446 H sawia na 13 Oktoba 2024 M

- Ripoti Fupi juu ya Maendeleo ya Amali ya Matembezi -

Katika kumbukumbu ya mwaka mmoja wa mauaji ya halaiki na uadui wa kinyama dhidi ya watu wetu mjini Gaza na maeneo mengine ya Ardhi Iliyobarikiwa (Palestine) wa umbile halifu la Kiyahudi, mashababu wa Hizb ut Tahrir nchini Uholanzi waliandaa matembezi chini ya kichwa “Miaka 76 na Mwaka Mmoja wa Mauaji ya Halaiki,” katika jiji la Amsterdam ambapo matembezi hayo yalianza mwendo wa saa nane na nusu mchana mnamo siku ya Jumapili, 13 Oktoba 2024 M, na ndugu na kina dada walioshiriki katika matembezi hayo walizunguka katika barabara za Amsterdam wakiimba kauli mbiu za kutaka nusra kwa Gaza na kupelekwa kwa majeshi ya Umma yaliyofungiwa katika kambi zao, na karibu saa kumi alasiri maandamano yalifikia hatua yake ya mwisho, na kisha mmoja wa ndugu akasoma aya zenye harufu nzuri kutoka kwa Quran Tukufu, ikifuatiwa na kalima ya Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir nchini Uholanzi, Ustadh Okay Balla, ambapo alizungumzia juu ya uwezekano wa kufanya maandamano na kwamba ni jambo dogo zaidi tunaloweza kulifanya kwa ajili ya watu wetu wa Gaza, na tuombe radhi kwa Mwenyezi Mungu, huenda akatusamehe kwa kushindwa kwetu kuwanusuru, na tuwahakikishie makafiri wa Magharibi kwamba sauti ya Waislamu itabaki kupaanzwa katika kutetea mambo yao. Kisha akataja baadhi ya nukta ambazo zilionekana wazi kutokana na mauaji haya ya halaiki yaliyoanzishwa na umbile katili la Kiyahudi kwenye Ukanda wa Gaza, ambayo muhimu zaidi ni anguko kubwa la yale ambayo nchi za Magharibi huyatolea midomo ya usawa, haki za watoto na za binadamu, sheria za kimataifa, na upuuzi mwingine ambayo yamekuwa yakifanya vichwa vyetu vilipuke kwa miongo kadhaa. Jambo la watawala wote wa Kiislamu lilifichuliwa, vijana na wazee wakaanza kutambua kwamba hawa Ruwaibidha ndio walinzi wa umbile la Kiyahudi na safu yake ya kwanza ya ulinzi. Ama kwa Umma wa Kiislamu, imedhihirika mbali na karibu kwamba Waislamu ni Umma mmoja ambao maumivu yake ni mamoja, na hisia zake ni moja, licha ya njama za nchi za Magharibi katika kuweka mipaka ya Sykes-Picot na kufanya kazi ya kuwagawanya Waislamu kwa misingi ya kitaifa, kizalendo.

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir barani Ulaya

Jumapili, 10 Rabi’ ul-Akhir 1446 H sawia na 13 Oktoba 2024 M

­- Sehemu ya Amali ya Matembezi -

#طوفان_الأقصى

#الجيوش_إلى_الأقصى

#الأقصى_يستصرخ_الجيوش

#ArmiesToAqsa

#AksaTufanı

#OrdularAksaya

Aqsa_calls_armies#

#AqsaCallsArmies

Kwa Maelezo zaidi, Tafadhali Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Uholanzi:

Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Uholanzi

Facebook: Hizb ut Tahrir / Uholanzi

Twitter: Hizb ut Tahrir / Uholanzi

Instagram: Hizb ut Tahrir / Uholanzi

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu