Jumapili, 26 Rajab 1446 | 2025/01/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir: Hotuba kutoka Semina ya Uingereza juu ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake Kuchukua Hatua kwa ajili ya Palestina!

Siku ya Kimataifa ya Wanawake Kuchukua Hatua kwa ajili ya Palestina iliandaliwa na Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari vya Hizb ut Tahrir kwa ushirikiano na Wanawake wa Hizb ut Tahrir ulimwenguni kuyata majeshi ya ardhi za Waislamu kutaharaki haraka ili kuwaokoa wanawake na watoto wa Gaza na kuikomboa Ardhi yote Iliyobarikiwa ya Palestina kutokana uvamizi wa mauaji wa Kizayuni. Siku ya kuchukua hatua ilipanuka kwa zaidi ya mabara 5 na ilijumuisha maandamano, semina na amali zengine za wanawake nchini Palestina, Uturuki, Indonesia, Tunisia, Lebanon, Malaysia, Kenya, Amerika, Australia, Denmark, Uholanzi, Ubelgiji na Uingereza.

#ArmiesToAqsa

Jumapili, 12 Jumadel Awwal 1445 H sawia na 26 Novemba 2023 M

- Hotuba 1 -
Kubadilisha Simulizi juu ya Siku ya Kimataifa ya Kuchukua Hatua kwa ajili ya Palestina

Hii ilikuwa hotuba ya 1 iliyotolewa katika semina ya wanawake nchini Uingereza mnamo Novemba 26 kama sehemu ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake Kuchukua Hatua kwa ajili ya Palestina iliyoandaliwa na Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir kwa kuratibu na Wanawake wa Hizb ut Tahrir Ulimwenguni.

Hotuba hii inaelezea dori ya dola za kikoloni za Kimagharibi na Umoja wa Mataifa katika uanzishwaji na uimarishwaji wa umbile la Kizayuni nchini Palestina. Pia inaelezea yale yanayoitwa kuwa masuluhisho kadhaa ambayo mara nyingi huwasilishwa kumaliza mauaji ya halaiki dhidi ya Wapalestina, kama vile suluhisho la dola mbili na suluhisho la dola moja kwa msingi wa kanuni za serikali za kitaifa na za kisekula. Inaelezea jinsi mapendekezo haya ni mwendelezo wa ajenda za kikoloni za Kimagharibi katika kanda hiyo ambayo yanalinda maslahi ya Magharibi badala ya kuleta kitu chochote kizuri kwa Waislamu wa Palestina. Hotuba hiyo inasisitiza kwamba suluhisho lililojengwa tu juu ya Uislamu pekee ndilo litakalomaliza uvamizi na ukandamizaji wa Waislamu wa Palestina milele.

Hotuba hii ilitolewa na Haniya Abdul Jalil, Mwanachama wa Hizb ut Tahrir Uingereza

- Hotuba 2 -

Ukombozi wa Palestina Yote wa Majeshi ya Waislamu ndio Unaoweza KUMALIZA mauaji ya halaiki!

Hii ilikuwa hotuba ya 2 iliyotolewa katika semina ya wanawake nchini Uingereza mnamo Novemba 26 kama sehemu ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake Kuchukua Hatua kwa ajili ya Palestina iliyoandaliwa na Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir kwa ushirikiano na Wanawake wa Hizb ut Tahrir Ulimwenguni.

Hotuba hii inaangazia jinsi pekee ya Kiislamu, ya kivitendo na ya kudumu ya kumaliza mauaji ya halaiki na ukatili kwa Waislamu wa Gaza na Palestina yote ni ukombozi wa ardhi hii yote iliyobarikiwa kutokana na umbile uaji la Kizayuni na majeshi ya kitaalamu ya nchi za Waislamu. Pia inapinga hoja mbali mbali ambazo zinadai kwamba uhamasishaji wa majeshi ya Waislamu sio lengo la kihakika, kwa kujadili ushindi mkubwa wa majeshi ya Waislamu wa zamani licha ya kuzidiwa kiidadi, na pia uwezo wa Umma na ardhi za Waislamu kwa sasa katika upande wa nguvu za watu, rasilimali, na nguvu ya kijeshi na ya kimkakati ambazo zinaweza kutumika kumaliza mauaji ya halaiki ikiwa utashi wa kisiasa utakuwepo miongoni mwa watawala na serikali za ulimwengu wa Kiislamu.

Hotuba hii pia inaangazia jinsi kizuizi kikuu cha ukombozi wa Palestina ni watawala wa sasa wa ulimwengu wa Waislamu na fikra ya utaifa na mipaka ya kitaifa ambayo inawagawanya Waislamu na ardhi yao. Hotuba hii inawataka Waislamu na maafisa wanyoofu wa majeshi ya Waislamu kuwang’oa watawala hawa waliopandikizwa na kuungwa mkono na Magharibi  na mipaka ya kitaifa inayozigawanya ardhi za Waislamu na kusimamisha uongozi wa Kiislamu wa dola ya Khilafah kwa njia ya Utume ambayo itahamasisha jeshi lake kukomboa ardhi zote za Waislamu zinazokaliwa kimabavu na kuwalinda Waislamu kote ulimwengun kutokana na kukandamizwa.

Hotuba hii inamalizika kwa kupeana ujumbe kwa maafisa wanyoofu wa majeshi ya Waislamu kutekeleza jukumu lao la kuwalinda Waislamu wa Palestina na kwengineko na kuikomboa Ardhi hii iliyobarikiwa na kutoa nusrah yao (msaada wa kimada) kwa ajili ya kusimamisha Khilafah.

Hotuba hii ilitolewa na Dkt. Nazreen Nawaz, Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake katika Afisi Huu ya Habari ya Hizb ut Tahrir. Hotuba hii pia ilitolewa na wazungumzaji katika maandamano na semina mbali mbali zilizoandaliwa kote ulimwenguni ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake Kuchukua Hatua kwa ajili ya Palestina.

- Hotuba 3 -
Ikiwa sio Sasa, basi Lini? Ikiwa sio Majeshi, basi Nani?
(Urdu)

Hii ilikuwa hotuba ya 3 iliyotolewa katika semina ya wanawake nchini Uingereza mnamo Novemba 26 kama sehemu ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake Kuchukua Hatua kwa ajili ya Palestina iliyoandaliwa na Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir kwa ushirikiano na Wanawake wa Hizb ut Tahrir Ulimwenguni.

Ilinyanyua wito kwa maafisa wanyoofu wa Pakistan na majeshi mengine ya Waislamu kutaharaki haraka kwa ajili utetezi wa Waislamu wa Gaza na kuikomboa ardhi yote ya Palestina, na pia kutoa nusrah (msaada wa kimada) yao kwa ajili ya kusimamisha Uongozi wa Kiisilamu wa dola ya Khilafah kwa njia ya Utume ambayo itahamasisha jeshi lake kukomboa ardhi zote za Waislamu zinazokaliwa kimabavu na kuwalinda Waislamu ulimwenguni kutokana na kukandamizwa.

Hotuba hiI ilitolewa na Sarah Feroz, Mwanachama wa Hizb ut Tahrir Uingereza.

- Hotuba 4 -
Ikiwa sio Sasa, basi Lini? Ikiwa sio Majeshi, basi Nani?
(Arabic)

Hii ilikuwa hotuba ya 4 iliyotolewa katika semina ya wanawake nchini Uingereza mnamo Novemba 26 kama sehemu ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake Kuchukua Hatua kwa ajili ya Palestina iliyoandaliwa na Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir kwa ushirikiano na Wanawake wa Hizb ut Tahrir Ulimwenguni.

Ilinyanyua wito kwa maafisa wanyoofu wa Pakistan na majeshi mengine ya Waislamu kutaharaki haraka kwa ajili utetezi wa Waislamu wa Gaza na kuikomboa ardhi yote ya Palestina, na pia kutoa nusrah (msaada wa kimada) yao kwa ajili ya kusimamisha Uongozi wa Kiisilamu wa dola ya Khilafah kwa njia ya Utume ambayo itahamasisha jeshi lake kukomboa ardhi zote za Waislamu zinazokaliwa kimabavu na kuwalinda Waislamu ulimwenguni kutokana na kukandamizwa.

Hotuba hiI ilitolewa na Ustadha Lama, Msomaji Qur’an, Profesa wa Chuo Kikuu na Mtafiti

- Hotuba 5 -

Wito kwa Vijana wa Kiislamu Kufanya Kazi kwa ajili Ukombozi wa Palestina

Hii ilikuwa ndio hotuba ya mwisho iliyotolewa katika semina ya wanawake nchini Uingereza mnamo Novemba 26 kama sehemu ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake Kuchukua Hatua kwa ajili ya Palestina iliyoandaliwa na Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir kwa ushirikiano na Wanawake wa Hizb ut Tahrir Ulimwenguni.

Hotuba hii inaelezea ukatili na ugaidi ambao watoto na vijana wa Palestina wanaishi nao kwa sasa na wameishi nao kwa miongo kadhaa chini ya umbile uaji la Kizayuni. Inaelezea ushujaa ambao vijana wa Palestina wameonyesha licha ya yote haya katika kupinga uvamizi.

Hotuba hii inapaaza wito kwa vijana wa Kiislamu kuwa na uwazi, kujitolea na ujasiri katika kufanyia kazi suluhisho la kumaliza mauaji ya halaiki na ukaliaji wa kimabavu wa Palestina - Uwazi kuhusu historia ya uvamizi na suluhisho sahihi la tatizo hili ambalo limejengwa juu ya Dini yao , Uislamu; Kujitolea katika kufanya kazi kwa ajili ya ukombozi kamili wa Palestina kupitia kuyataka majeshi ya ardhi za Waislamu kusonga kuikomboa Ardhi hii Iliyobarikiwa na pia kufanya kazi kwa ajili ya kusimamisha uongozi wa Kiislamu wa dola ya Khilafah kwa njia ya Utume ambayo italinda Waislamu kote ulimwenguni kutokana ukandamizaji na uvamizi; na Ujasiri ili wakataa kunyamazishwa na vibandiko na vitisho vinavyokuja kutoka kwa serikali mbali mbali na vyombo vya habari vya kisekula kuwanyamazisha kutokana na kutoa nusra yao kwa ndugu na dada zao nchini Palestina au kulingania ukombozi wa ardhi hiyo au kubeba Dawah ya kusimamisha Khilafah ambayo itamaliza ukatili kwa Waislamu wa Palestina na kwengineko milele.

Hotuba hiyo ilitolewa na Umm Bilal, Mwanachama wa Hizb ut Tahrir Uingereza.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu