Jumamosi, 25 Rajab 1446 | 2025/01/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Wilayah Uturuki: Taarifa kwa Vyombo vya Habari dhidi ya Kuchapisha Tena Michoro ya Charlie Hebdo ya Vikaragosi Vyenye Kumtusi Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw)

Hizb ut Tahrir katika Wilayah Uturuki ilitoa taarifa kwa vyombo vya habari kwa anwani, "Kumtusi Mtume wa Mwenyezi Mungu hakusameheki", katika Bustani ya Sarachane jijini Istanbul. Taarifa hiyo kwa vyombo vya habari ilihudhuriwa na mamia ya Waislamu, waliounga mkono hafla hii kwa kufuata sheria za janga la maambukizi.

Taarifa hiyo kwa vyombo vya habari ilitolewa kulaani jarida la vichekesho la Kifaransa la Charlie Hebdo, ambalo lilichapisha tena vikaragosi vya kumtusi Rasulallah (saw).

Hafla ilianza kwa utangulizi wa Muhammed Emin Yildirim, Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir jijini Istanbul, ikifuatiwa na Takbira na Kumswalia Mtume (saw) kisha Taarifa hiyo ikasomwa na kuchambuliwa kwa kina na Musa Bayoğlu, mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Uturuki, kabla ya hatimaye Bayoğlu kutoa wito kwa watawala na wanachuoni kumcha Mwenyezi Mungu (swt) kwa kunyanyua sauti zao za haki kumkumbatia Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw).

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

katika Wilayah Uturuki

Mkusanyiko wa Picha

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 06 Septemba 2020 14:23

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu