Jumamosi, 19 Jumada al-awwal 1445 | 2023/12/02
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Wilayah Uturuki: Visimamo vya Kulaani Uadui wa Umbile la Kiyahudi kwa Msikiti wa Al-Aqsa Uliobarikiwa!

Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki iliandaa msururu wa visimamo na maandamano katika miji kumi mikubwa nchini Uturuki (Islampol, Ankara, Bursa, Adana, Şanlıurfa, Ann, Mersin, Gaziantep, Kahramanmaras, Hatay / Antakya) chini ya kaulimbiu:

"Al-Aqsa Haijakosa Mwenyewe!"

Kulaani uadui wa kinyama wa umbile la Kiyahudi kuwanyanyasa wenye kuswali na kufanya itikaf ndani ya Msikiti wa Al-Aqsa Al-Mubarak uliopelekea majeruhi takriban Waislamu 600 wengi wao wakiwa na majeraha ya moja kwa moja kichwani yenye kusababisha hali mbaya.

Kisimamo cha jiji la Islampol kiliandaliwa mbele ya ubalozi wa umbile la Kiyahudi, ambapo Ustadh Mahmoud Kar, Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir, alisoma taarifa kwa waandishi wa habari mbele ya umati wa watu waliokusanyika kutoka pande tofauti kukinusuru kisimamo hicho na kukiunga mkono katika kukemea uhalifu wa umbile la Kiyahudi kwanza mnyakuzi, pili khiyana ya watawala wa Kiislamu ambao hawachangamki kutetea matukufu ya Umma, na tatu, kuyataka majeshi kutekeleza majukumu yao na kwenda kuwanusuru Waislamu katika Msikiti wa Al-Aqsa uliobarikiwa na kuikomboa Ardhi yote Iliyobarikiwa (Palestina) kutokana na uchafu wa Mayahudi.

Kisimamo kikahitimishwa kwa dua kwa Mwenyezi Mungu (swt) ili kuharakisha Nusra na tamkini.

Jumatatu, 28 Ramadhan Al-Mubarak 1442 H sawia na 10 Mei 2021 M

Click to enlarge image 2021_05_10_Turkey_Aksa_Protest_PICs_01.jpg

Click to open image!

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu