Jumatano, 08 Rajab 1446 | 2025/01/08
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki:

Uamuzi wa Mahakama ya Rufaa katika Faili ya Hizb ut Tahrir … Mahakama Ilikataa Pingamizi bila ya Kutoa Sababu Yoyote!

(Imetafsiriwa)

Katika kesi kuhusiana na Kongamano la Khilafah, lililopangwa kufanyika mnamo Machi 5, 2017 jijini Istanbul lakini halikufanyika kutokana na kukataa kwa idara ya raia, Mahakama ya Rufaa ilikataa pingamizi ya uamuzi wa adhabu wa mahakama ya eneo bila kutoa sababu yoyote.

Kongamano hilo lenye kichwa "Kwa Nini Ulimwengu Unahitaji Khilafah?", lililopangwa kufanyika jijini Istanbul mnamo Machi 5, 2017 lilizuiwa bila sababu yoyote halali ya kuridhisha, na kesi zilianzishwa dhidi ya wazungumzaji wa kongamano hilo. Katika kesi iliyoanzishwa na Mahakama ya 30 ya Jinai ya Istanbul; Mahmut KAR, Osman YILDIZ, Abdullah İMAMOĞLU na Musa BAYOĞLU, ambao walikuwa miongoni mwa wazungumzaji wa kongamano hilo, walihukumiwa kifungo cha miaka 31 na miezi 3 kwa jumla.

Pamoja na rufaa ya mawakili wa faili hiyo, kesi hiyo ilihamishwa hadi Mahakama ya Rufaa. Mnamo tarehe 17/05/2022, Jopo la Pili la Kuadhibu la Mahakama ya Haki ya Jimbo la Istanbul ilikataa pingamizi hiyo bila kutoa sababu yoyote. Mahakama ya Rufaa ilisema kwamba hakukuwa na uvunjaji wa sheria katika sheria ya msingi na utaratibu katika kesi iliyofanywa na mahakama ya mwanzo (IST 30th High Criminal Court). Ujumbe wa mahakama ya rufaa ulitupilia mbali pingamizi hiyo, wakisema kuwa hakuna upungufu katika ushahidi na kesi, na kwamba tathmini ilikuwa sahihi kwa mujibu wa ushahidi.

Kwa uamuzi huu, Jopo la Rufaa lilipuuza ukiukaji 9 tofauti wa haki kuhusu kesi za Hizb ut Tahrir na Mahakama ya Kikatiba. Kwa sababu Mahakama ya Katiba ilitoa maamuzi 9 ya ukiukaji wa haki, ikiwemo Mkutano Mkuu 1 na maamuzi ya Jopo la 8, ulisema kwamba mahakama za mwanzo na Mahakama ya Upeo zilikiuka "haki ya uamuzi wa busara" katika kesi kuhusu Hizb ut Tahrir na kuamuru kusikilizwa upya.

Mahmut KAR, ambaye alihukumiwa miaka 12.5 katika kesi hiyo, alisema kuwa uamuzi huu wa Mahakama ya Rufaa ulikiuka mipaka ya Mahakama ya Kikatiba kwa ukiukaji wa haki. Mahmut KAR alisema: “Mahakama ya Rufaa iliiona hukumu niliyopewa mimi na marafiki zangu kutokana na kongamano hilo ambao halikuweza kufanyika mwaka wa 2017 kwa mujibu wa sheria. Sheria ipi? Wakati Mahakama ya Kikatiba inatoa uamuzi kwamba kuna ukiukaji wa haki katika kesi inayohusu Hizb ut Tahrir, uamuzi huu wa Mahakama ya Rufaa ni wa kiholela.”

Baada ya uamuzi wa Mahakama ya Rufaa, İmamoğlu alitoa taarifa kwenye akaunti yake ya Twitter na kutumia taarifa zifuatazo: "Leo, Mahakama ya Rufaa, licha ya maamuzi yote ya ukiukaji wa haki wa Mahakama ya Katiba, ilihalalisha na kuunga mkono hukumu ya kifungo cha miaka 6.3 ya mahakama ya eneo dhidi yangu. Huu ni uidhinishaji usio halali na usiostahili. Sio uhalifu bali ni heshima kupaza sauti kuwa ulimwengu wahitaji Khilafah.”

Wakili Mustafa KOCAMANBAŞ alisema: “Mahakama ya rufaa ilikubali hukumu zilizotolewa kwa kongamano hilo ambalo halikuweza kufanywa, Sababu; Haikujisumbua kuandika, mimi niliandika, hukumu hiyo inafanya kazi, Hii ni dhulma, uzembe, idara ya mahakama ya Uturuki inarudi nyuma, sio mbele, kwa maamuzi haya.”

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Uturuki

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu