Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Katika Chuki Yake kwa Uislamu na Waislamu, Urusi ya Sasa Yafuata Nyayo za Tsar na Wakomunisti

Na: Fazil Amzaev*

Mnano July 7, 2020 ndani ya Krimea lilipita wimbi jengine la misako na ukamataji ambapo watu 7 waliwekwa kizuizini:

Ismet Ibragimov, Zekirya Muratov, Vadim Bektemirov, Emil Ziyadinov, Alim Sufyanov, Seyran Khairetdinov na Alexander Sizikov. Dilyaver Memetov, ambaye hakupatikana nyumbani wakati wa upelelezi, anatakiwa.

Wote walio wekwa kizuizini wametuhumiwa kuwa wanachama wa chama cha kisiasa Kiislamu cha Hizb ut Tahrir. Wanashtakiwa kwa kifungu 205.5 cha Sheria ya Jinai ya Shirikisho la Urusi “Kushiriki katika matendo ya kundi la kigaidi.”

Uvamizi huu wa vikosi maalumu vya usalama vya Urusi ni uthibitisho mwingine wa uchu wa chuki kwa Uislamu na Waislamu.

Zaidi ya hayo, kile kilichotokea Julai 7, 2020 kinaashiria kwamba serikali ya Urusi haizipi uzito fahamu za wanadamu na ubinadamu, baada ya yote, Alexander Sizikov aliyeshikwa ni mlemavu wa kundi 1. Ni kipofu kabisa.

Kuhusiana na madai ya ugaidi, umbile la Hizb ut Tahrir la kutokuwa na vurugu ni maarufu ambalo limethibitika kwa zaidi ya miaka 60 ya historia ya uwepo wa chama hichi cha kisiasa. Hizb Tahrir imejifunga na kazi ya kifikra na kisiasa pekee.

Zaidi ya hayo, kutokana na kumbukumbu za kesi za mahakama kwa yale yanayoitwa mashtaka ya Hizb ut Tahrir, hatia pekee ya Waislamu walio kizuizini ni kusoma na kuzungumzia juu ya fikra na sheria za Kiislamu.

Faili za mashtaka hazina silaha, hazina mashambulizi ya kigaidi, hamna majeruhi, wala hazina hata kupanga vitendo kama hayo.

Yote haya yanaashiria uhalisia wa mateso, chini ya kisingizio cha kupambana na ugaidi kwa Waislamu, ambao hawana uhusiano wowote na matendo ya vurugu.

Sheria dhidi ya ugaidi na siasa kali zimekuwa silaha rahisi kupiga upinzani katika mikono ya serikali ya Urusi na huduma maalumu.

Kuhusiana na sababu halisi ya mateso kwa Waislamu wa Crimea, yanaegemea katika kujifunga kwao kwa Uislamu na kutokuwa na nia ya kukubaliana na sera za kihalifu za Urusi dhidi ya Waislamu.

Mwenyezi Mungu asema katika Quran:

﴿وَمَا نَقَمُوا مِنْهُمْ إِلَّا أَنْ يُؤْمِنُوا بِالَّهِ الْعَزِيزِ الْحَمِيدِ

“Nao hawakuona baya lolote kwao ila kuwa wakimuamini Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Msifiwa.” [85:8]

Sera za leo za Urusi kuhusiana na Waislamu wa Crimea, Matatari wa Crimea, sio kitu kigeni. Huu ni muendelezo wa sera za kihalifu ambazo wafalme na wakomunisti walizitekeleza dhidi ya Waislamu wa eneo hili kwa zaidi ya miaka 200.

Uharibifu wa utajiri wa kimfumo wa watu Waislamu, uharibifu wa misikiti na madrasa, ubadilishaji wa majengo haya kuwa sehemu za starehe za haramu na mabohari… siasa zote hizi za kiuadui zinajitokeza kwa nguvu mpya kwa sura ya mamlaka za leo za Urusi.

Kwa hivyo, wafalme na wakomunisti wameungana katika ukatili kwa wasomi, maimamu, na kwa mwanaharakati yeyote miongoni mwa Waislamu wa Krimea.

Hivyo Wafalme na Wakomunisti waliungana kuwaangamiza wasomi, maimamu, wenye elimu na mwanaharakati yeyote miongoni mwa Waislamu wa Crimea.

Leo tunaona sera zilezile, ambapo miongoni mwa waislamu 74 waliowekwa kizuizini na kushtakiwa kwa ugaidi tunawapata wenyekiti wa jamii za kidini, maimamu, walimu wa Tajwid, watu mashuhuri wanaosaidia kusambaza Uislamu, wafanyi biashara, wajuzi wa Kiarabu wanaozungumza lugha ya Quran na wanaojua sayansi za Sharia.

Kwa kufanya hivyo, Urusi, iwe ni ya ki-tsar au ya “Kidemokrasia”, imejaribu kwa zaidi ya karne mbili kuwanyima Waislamu wa Crimea utajiri wa mfumo wao - dini ya Kiislamu.

Yale yanayojiri leo Crimea ni dhihirisho wa kukosa nguvu, hasira na uchungu unayoipata serikali ya Urusi kwa sababu ya kushidwa kwake kuwalazimisha Waislamu kuacha imani yao waliolazimishwa na dini yao.

Bali ni upi ufafanuzi mwengine kumkamata kwa mlemavu kipofu - Alexander Sizikov, anayejulikana kwa msimamo wake jasiri wa Kiislamu, ambao aliudhihirisha katika kutetea Waislamu walio kizuizini, iwe ni katika majengo ya mahakama ama wakati wa maandamano yake binafsi aliyoyapanga mwenyewe katika mji mkuu wa Crimea. Maafisa wa usalama wa Urusi kutokana na hofu yao kwa kusikia neno la haki kutoka kinywani mwa Muislamu huyu, wakatunga dhidi yake kesi ya jinai ya ugaidi ambayo anatishiwa kufungwa kifungo cha maisha.

Licha ya ukamataji na kushtaki wengi uliofanywa na serikali ya Urusi baada ya kuimarisha nguvu zake halisi juu ya bara la Crimea mnamo 2014, Waislamu wa Crimea wanaendelea kusimama upande wa wanaodhulumiwa, wakiwasaidia kwa hali zote.

Katika kuhitimisha, lazima izingatiwe kwamba siasa hizi za kihalifu na dhulma za Urusi ya sasa zitapata hatima moja sawia na wafalme na wakomunisti madhalimu.

Majaribio yao yote ya kuharibu kitambulisho cha Waislamu wa Crimea, Matatari wa Crimea hayakufaulu na wakateseka kwa kumalizwa ghafla, licha ya ukweli kwamba dhulma zao zilikaa kwa miongo mingi.

Madhalimu kama Catherine II na Stalin ambao waliwatendea Waislamu wa Crimea hata uhalifu mkubwa zaidi na kuweka lengo la kumaliza sio tu madhihirisho madogo ya Uislamu ndani ya Crimea pekee, bali hata kujaribu kuwauwa Waislamu kabisa katika ardhi hizi zenye rutuba, walikufa na wakaingia makaburini. Huku Waislamu wa Crimea wakibakia hai na siku baada ya siku wakiimarika na kurudi katika ufahamu na utabikishaji wao wa awali wa Uislamu.

Siku iko karibu ambapo “wapiganaji vita dhidi ugaidi” wa leo watapotea kama walivyo angamia watangulizi wao na tawala zao, na Waislamu wa Crimea wataendelea kuishi katika ardhi yao kwa usalama wakiutekeleza Uislamu kwa uhuru katika maisha yao ya kila siku.

﴿وَيَوۡمَئِذٖ يَفۡرَحُ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ * بِنَصۡرِ ٱللَّهِۚ يَنصُرُ مَن يَشَآءُۖ وَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ

Na siku hiyo Waumini watafurahi. Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu. [30: 4 - 5]

 *Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb Tahrir Ukraine

* Imeandikwa kwa Gazeti la Ar Rayah – Toleo 296

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoAlhamisi, 13 Agosti 2020 11:08

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu