Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Uingereza – Jamhuri Mpya ya Fujo

Na: Adnan Khan*

Uingereza kwa muda mrefu imekuwa katika kilele cha kutawala kiasi kwamba jua halikuchwa na kileleni mwake taifa hili la kisiwa lilitawala zaidi ya asilimia 25 ya watu duniani. Lakini hilo lilikuwa zamani sana na hivi leo Uingereza imeshindwa na mataifa kama Pakistan, Bangladesh na Zimbabwe katika kuonekana kuwa ni mazuri. Kwa kuzingatia kuwa mnamo 2019, India itakuwa na Mapato ya Taifa (GDP) makubwa kuliko UK. India ambayo mpaka hivi majuzi ilikuwa ni taifa la ulimwengu wa tatu, taifa ambalo lilikoloniwa na UK litakuwa na uchumi mkubwa kuliko UK. India inayo kila haki kuiondosha UK ndani ya Umoja wa Mataifa (UN) na katika mazungumzo ya kibiashara. India iliyokuwa imevamiwa na UK itakuwa na umuhimu mkubwa katika uchumi wa dunia kuliko taifa ililolikoloni. Dunia inabadilika na ndani ya UK kigezo hicho kimeipelekea kutathmini nafasi yake ndani ya Umoja wa Ulaya (EU) na nafasi yake duniani.
Kikundi cha wanasiasa ndani ya Uingereza wamekuwa katika msuguano kuhusu uanachama wake ndani ya EU na kwa namna gani unaisaidia UK. Mgawanyiko huu umesababisha mzozo mkali wa kindani ambao umekuwepo kwa miaka arubaini. Kura ya maoni ilipelekea kushinda kwa wanaotaka kujiondoa lakini kwa miaka mitatu mtawalia wanasiasa wamefanya kila wawezalo ili wasitekeleze maamuzi ya uchaguzi wamechelewesha kuondoka katika EU na wameweka masharti juu ya masharti katika mazungumzo yao na EU na kilichowazi hivi sasa kwa umma ni kwamba kura yao haikuzingatiwa na wanasiasa hawajali matakwa ya watu.
Nafasi ya Uingereza inaonekana lau kama ambaye Uingereza itabakia basi ipate mgao ambao utakaoiwezesha kupata manufaa ya EU, muungano wa forodha na soko moja lakini iweke vikwazo kwa uhamiaji na kujiweka mbali na michakato yoyote ya EU ambayo itakuwa haiwafai. Ikiwa mgao hautopatikana basi Uingereza ni bora iwe nje ya EU. Mazungumzo na EU kuhusiana na hilo yanaelekea kufeli kwani Uingereza inataka mgao maalum ambao hakuna mwanachama aliyenao ndani ya EU.
Tatizo kwa Uingereza ni kwamba hakuna sababu ya EU kujifunga na masharti hayo. Ni kwa maslahi ya EU kuhifadhi EU na kuibakisha Uingereza ndani ya EU kwa kuwa hakuna taifa lililowahi kutoka EU. Ugiriki licha ya kuwa ndani ya kina cha janga la kiuchumi wakati ambapo Ujerumani ilikuwa inaweka masharti makali rai ya umma ilibakia juu kwa Ugiriki kubakia ndani ya EU. Lakini kwa kuwa mazungumzo yamechukua muda wa miaka mitatu wengi ndani ya EU wanaitizama Uingereza kama mtoto mkorofi asiyestahiki kupewa manufaa ya EU.
EU iliipa mgao UK pale ambapo itahitajika kukubali haki ya Wauropa kusafiri kwenda UK nao wairuhusu kuingia katika soko moja na muungano wa forodha. Lakini bunge la Uingereza lilikataa kukubali mgao huo kwa kuzingatia kuwa uhamiaji ulikuwa suala muhimu kwa waliopiga kura ya kujiondoa katika EU. Theresa May aliwasilisha mgao huo mara tatu bungeni kwa matumaini kwamba ungepita lakini alifedheheshwa na kulazimishwa kuondoka afisini.
Boris Johnson aliingia afisini akiwa na mkono dhaifu, EU ilikuwa imeweka wazi kwamba haitokubali kuzungumza tena mgao wowote na kwamba ule aliopewa Theresa May ndio wa mwisho. Johnson aliingia afisini nyuma huku akizingatia kuwa amejiandaa kuitoa UK pasina mgao wowote. Amejaribu kuulazimisha mkono wa EU. Viongozi wa Ulaya kwa muda mrefu wamemtazama Boris Johnson kama ni mjinga asiyemuanifu anayeongozwa na matamanio ya kibinafsi. Serikali zote za May na Johnson zimejaribu kwa muendelezo kutolijumuisha bunge katika kuwa na dori ndani ya mazungumzo ya kujiondoa, huku jaribio la Boris la hivi majuzi ni kuhairisha bunge.
Kujionda katika EU kumefichua uhalisia wa demokrasia, nidhamu ya utawala wa wachache kwa wachache kwa ajili ya wachache. Boris Johnson kiuhalisia anajiandaa kuweka maandalizi ya uchaguzi mkuu usioepukika. Kilicholengwa kuwa ni talaka ya kimya kutoka EU imegeuka na kuwa ni maonyesho ya kila siku katika TV yaliyokuwa na visa vipya ambavyo hakuna anayeweza kuvihimili.
Iwe itakavyokuwa ni wazi kwamba Uingereza ima itabakia ndani au nje ya EU inadondoka katika kikundi cha mataifa makuu, wakati ambapo India hivi karibuni itaitizama Uingereza ikiwa nyuma. Ahadi ambazo kikundi cha wanasiasa ilizotoa kwa raia wake zilikuwa ni porojo tu za kuficha nia zao za kweli.

*Imeandikwa kwa ajili ya Gazeti la Ar-Rayah - Toleo 255

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumamosi, 18 Aprili 2020 15:45
Yaliyomo ndani ya kifungu hichi: Somalia Iliyomakinika Kisekula: Ndoto ya Marekani »

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu