Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Sera ya Marekani ya Kuidhibiti China Imesimama Wapi kwa Sasa?

Na Ustadh As’ad Mansoor, kwa Gazeti la Al-Rayah

(Imetafsiriwa)

Miongoni mwa mbinu zitumiwazo na Marekani ni kushambulia nchi adui ama pinzani kwa nguvu za kijeshi, kuangamiza ama kuihusuru. La ziada, Marekani hutua kwenye mbinu ya kisiasa na kiuchumi katika kile kiitwacho sera ya udhibiti. Marekani ilianzisha vita vya Vietnam ili kuishambulia China na kuizuia katika kulidhibiti eneo la kusini mashariki mwa bara Asia. Pindi Marekani ilipogundua imepata hasara kubwa na iko kwenye shida, ikaanza kufuata sera ya udhibiti. Hivyo ikaanza kuwasiliana na China kupitia aliyekuwa Waziri wa Kigeni, Henry Kissinger, na kuifanya China kuwa ni mwanachama wa kudumu wa baraza la usalama mnamo 1971. Hili likafuatiwa na ziara ya Rais Nixon wa Marekani mwaka wa 1972.

Baada ya kufariki kwa Mao, Deng Xiaoping aliyeshika uongozi wa China mnamo 1979 na akafuata sera ya uwazi na mageuzi. Makubaliano yaliafikiwa kati ya pande hizo mbili kwamba Marekani itatambua China moja, hata ikijumuisha Taiwan ndani yake, katika sehemu ya ushirikiano wa kiuchumi na wa kisiasa. Marekani ikawa na upendeleo kwa China katika mipango ya kiuchumi, kwa hivyo, makampuni ya Marekani yakaingia China na ziada za kibiashara zikazidi kwa upande wa China, kwa hilo Marekani haikuona tatizo lolote. Kwa wakati huohuo, Washington ikaanza kulenga mambo kama haki za kibinadamu, uhuru wa kujieleza, demokrasia na fikra za Kimagharibi. Marekani ikachochea watetezi wa haki za binadamu, ila China iliwanyamazisha kikatili kama ilivyotokea katika mauwaji ya Uwanja wa Tiananmen mnamo 1989. Hata hivyo, Marekani iliendelea kuipendelea China katika mipango ya kibiashara, ili kuendelea na sera ya uangalizi.

Marekani iliimarisha mikakati yake ya ushirikiano wa  kijeshi na kisiasa, wakati wa utawala wa Obama ambaye alizuru China mnamo 2009 na kukaribisha dori ya China kiulimwengu. Hii ilikuwa kwa ajili ya kufanikisha sera ya uangalizi, kupitia kushirikiana kiulimwengu. Kwa hivyo yote ilikuwa ni kuileta China chini ya uangalizi na udhibiti wa Marekani, kuifanya isonge na Marekani. Pindi China ilipoendelea kuimarisha uwepo wake katika bahari ya China Kusini na kutengeneza silaha zake, ushirikiano wao ulisita na Marekani ikafeli katika jaribio lake. Na katika mikakati ya kieneo ya utawala wa Obama “pivot to East Asia”, Marekani ilituma asilimia sitini ya vikosi vyake vya maji katika eneo hilo. Badala yake, China ikatangaza mpango wake wa ukanda na njia (BRI) mnamo 2013 ili kujenga mtandao wa mawasiliano ya bara na baharini, kwa kuunganisha nchi za Asia, Ulaya na Afrika.

Na Trump aliposhika hatamu ya urais, Marekani iliangalia mbinu mpya na hivyo ikatangaza vita vya kiuchumi dhidi ya China mnamo 2018. Marekani ikaweka ushuru katika bidhaa za China, kwa kina cha bilioni $200, ili kuziba pengo la ziada ya kibiashara kati yao. China ikajibu kwa kuweka ushuru wa $ bilioni 60 kwa bidhaa za Marekani. Kisha, Marekani ikazama katika masuala ya ndani ya China na kuyachimba, mfano ni suala la dhulma dhidi ya Waislamu wa Uighur wanaonyanyaswa na China, na vilevile maandamano ya HongKong- “Vuguvugu dhidi ya Marekebisho ya Mswada wa Sheria ya Ufukuzaji mnamo 2019-2020 na kuzuia kuchukuliwa kwa Taiwan na China.

Kwa kuwasili kwa Biden katika uongozi mwanzoni mwa mwaka huu, chini ya wiki tatu baada ya kuchukua hatamu, Washington ilianza kudhihirisha ukali wake na uadui wake dhidi ya Beijing. Kama Biden alivyo sema mnamo 11 Februari 2021, “Kama hatutasonga, watakula chakula chetu cha mchana.” Katika ripoti yake ya “Kamati ya Mpito ya Muongozo wa Mikakati ya Kiusalama ya Kitaifa”, Marekani iliiangazia kwa makini China, zaidi ya ilivyoiangazia Urusi. Ripoti hiyo inasema, “Lazima tupambane na uhalisia kwamba mgawanyiko wa nguvu ulimwenguni unabadilika, ukisababisha matishio mapya.” Ripoti hiyo inaendelea kusema, “Haswa China, imethubutu kwa haraka. Ni mshindani pekee mwenye uwezo wa kujumuisha uchumi, diplomasia, jeshi, na nguvu za kiteknolojia kuwezesha pambano endelevu kwa mfumo imara na uliowazi wa kimataifa.”

Kutokana na hayo, Marekani ilianza kutengeneza miungano mipya ama kuihuisha miungano ya kitambo kama vile Quadrilateral Security Dialogue (QSD), pia inajulikana kama Quad), ambayo inaunganisha Marekani, Japan, Australia na India katika kukabili tishio na mipango ya upanuzi ya China katika eneo la India na Pasifiki. Raisi wa Marekani aliitisha kongamano la mtandaoni na washikadau wenza wa Quad mnamo 12 machi 2021, ikafuatiwa na ziara za mawaziri wa ulinzi na mambo ya kigeni wa Marekani katika nchi wanachama wa Quad, ili kuimarisha Quad. Marekani kisha ikaweka mazungumzo na China huko Alaska mnamo 18 machi 2021, ambayo yalichangia kufeli kwa Marekani. China ikachukua msimamo thabiti katika mjadala, juu ya kuingilia masuala ya ndani ya China na kuikabili kidhati Marekani, kwa kuituhumu juu ya kukiuka haki za kibinadamu ndani na nje ya nchi, ikitafuta kustawisha mamlaka yake juu ya nchi zingine na usaliti.

Hili lilikuwa ni kongamano la wazi ambapo Marekani haingeweza kudhibiti ama kuficha mazungumzo kutoka vyombo vya Habari. Marekani kisha ikapiga firimbi juu ya wingo la tishio la Ujamaa la China, vilevile utafauti wa kithaqafa na maadili na China, ili kupanua mzozo wa pande hizo mbili na kuuelekeza kuwa mzozo wa kihadhara na kimfumo, ili marekani iongoze nchi za mfumo wa kirasilimali katika kuipiga vita China na kuizingira. Marekani inaweka shinikizo juu ya nchi za Ulaya kupunguza mahusiano yao na China na kufutilia mbali baadhi ya mikataba yao ya kibiashara na China na ubadilishanaji wa kiteknolojia, kama walivyoishinikiza Uingereza hapo nyuma katika miaka ya mwisho na kutangua ushirikiano wa Huawei katika mtandao wa 5G. Marekani imeshinikiza nchi zengine ya Ulaya kwa kuzifuata na kuzishawishi katika kushirikiana nazo. Biden alianza ziara zake Ulaya Juni 2, 2021, akianza na Uingereza, na kuhudhuria mkutano wa kilele wa G7 huko Cornwall, Uingereza, ambao ulianza tarehe 11 Juni 2021 na kudumu kwa siku tatu. Hii ilikuwa ni kuweka utawala wa Marekani juu ya nchi za Magharibi. Inatarajiwa Biden ameonesha tishio la China dhidi ya Wamagharibi na kufanyakazi ya kuikusanya Ulaya karibu na Marekani, katika kuishambulia China, kama ziada kwa Urusi, licha ya mkutano wa Geneva mnamo 16 Juni 2021 kati ya Raisi wa Marekani Biden na Raisi wa Urusi Putin, ambao ulikuwa ni jaribio la kuitumia Urusi dhidi ya China.

Hivyo basi, Marekani imesitisha sera ya udhibiti na kuanza sera ya mapambano, kuvunja mifupa kwa njia nyingi, katika jaribio la kuwekea kikomo uwezo wa China na kuweka mamlaka ya Marekani juu ya maeneo, haswa juu ya bahari ya kusini mwa China. Kwa upande mwengine, China, chini ya utawala wa Xi Jinping, inataka kuendeleza sera ya uwazi, marekebisho na kuendeleza uhusiano wake na nchi zingine haswa kupitia Mpango wa Ukanda na Barabara (BRI) ili kuweka uwepo wake na athari juu ya nchi hizo, kwa kuwatega na madeni, yakifuatiwa na unyonyaji kupitia miradi ambayo itakaa kwa miongo. China unatumia sera za kikoloni, ikitumia fedha nyingi juu ya utengenezaji silaha zake, huku ikikwepa mapambano ya wazi dhidi ya Marekani na nchi za Magharibi. Hakika China inataka kuelewana nao bila ya kulegeza msimamo malengo yake.

Hakuna kheri kwa wanadamu katika kuunga ima upande wa China au Marekani, Pamoja na kuamrisha kwake Magharibi na Urusi yote. Wote ni waovu kupindukia. Hivyo basi Khilafah Rashida kwa njia ya Utume lazima isimamishwe tena, ili kuukomboa ulimwengu kutokana na ufujaji wao wa utajiri wa watu, unyonyaji damu yao na kulazimisha utawala juu yao.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu