Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hakuna Udhuru kwa Muislamu au Asiyekuwa Muislamu Baada ya Leo, Kuhusiana na Vita Vipya vya Msalaba vinavyoitwa Uzayuni

Na Bilal Al-Muhajir – Wilayah Pakistan
(Imetafsiriwa)

Hakuna aliyesalia kwenye uso wa dunia hii ambaye hajui jinai zinazofanywa dhidi ya watu wasio na hatia wa Gaza. Kila mtu anajua jinsi dola jeuri ya Mayahudi inavyolipua majumba, na kuzibomoa juu ya vichwa vya wakaazi wake. Umbile la Mayahudi linawashambulia raia wasio na silaha, na kuwaua shahidi barabarani mchana kweupe. Linaenda kinyume na sheria zote za kiwahyi na maadili ya kibinadamu, huko Gaza na Ukingo wa Magharibi, katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina, eneo la Risala zilizoteremshwa kutoka mbinguni katika zama za Mitume (as). Habari zimeenea kote ulimwenguni za watu bilioni nane. Haiwezekani tena kukataa uhalifu. Haiwezekani kukubali udhuru wa kutojua juu ya jinai hizi, kwa mtu yeyote ambaye ni wa Umma wa Kiislamu, au hata mtu yeyote ambaye si wa umma wa Kiislamu.

Kadhalika, sio siri tena kwa mtu yeyote kwamba mauaji hayo yanafanywa na Mayahudi, huku wakishajiishwa na kuungwa mkono na dola kubwa za Magharibi, zikiongozwa na mkuu wa uovu, Marekani. Dola hizi za Magharibi zinaunga mkono dola jeuri ya Kiyahudi kwa nguvu zao zote za kijeshi, kiuchumi na vyombo vya habari. Bila shaka, sio siri tena kwa watu wa dunia, ukiwemo Umma wa Kiislamu, kwamba tawala na watawala wa Ulimwengu wa Kiislamu ni zana na vibaraka wa dola za Magharibi, na washirika wa dola ya Mayahudi. Ndani ya nyoyo za watawala wa Waislamu kuna chuki na uadui unaozidi kupamba moto dhidi ya Uislamu na Waislamu huko Palestina, na popote pale walipo. Hakuna uadui mdogo ndani ya nyoyo zao, kuliko ndani ya Mayahudi wenyewe. Watawala hawa ni wamoja na Mayahudi. Watawala hawa ni Wazayuni zaidi, kuliko Uzayuni wa bwana wao Biden. Kwa hiyo, ni sahihi kuvisifu vita hivi vinavyoendelea dhidi ya Ummah katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina kuwa ni vita vipya vya msalaba dhidi ya Ummah. Uwanja wa vita hivi vya msalaba wakati huu ni Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina. Umbile la   Mayahudi si chochote zaidi ya chombo kichafu kinachotekeleza kazi chafu ya Hadhara ya Kimsalaba ya Kimagharibi na urasilimali wa kilimwengu.

Kuizungumzia Palestina na watu wake sio sawa na kuizungumzia dunia nzima na watu wake, ingawa dunia nzima ni ya Mwenyezi Mungu (swt), Al-Adhwim, Al-Majid, na viumbe vyote ni viumbe vyake. Mwenyezi Mungu (swt) ameipa ardhi ya Palestina ubora juu ya zengine. Yeye (swt) aliteremsha aya zilizo wazi katika jambo hili, ambazo zitasomwa mpaka Siku ya Kiyama. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[سُبْحَانَ الَّذِي أَسْرَى بِعَبْدِهِ لَيْلًا مِنَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ إِلَى الْمَسْجِدِ الْأَقْصَى الَّذِي بَارَكْنَا حَوْلَهُ لِنُرِيَهُ مِنْ آيَاتِنَا إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ]

“SUBHANA, Ametakasika aliye mchukua mja wake usiku mmoja kutoka Msikiti Mtukufu mpaka Msikiti wa Mbali, ambao tumevibariki vilivyo uzunguka, ili tumuonyeshe baadhi ya Ishara zetu. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia na Mwenye kuona.” [Surah Al-Israa 18:1]. Mwenyezi Mungu (swt) amesema kuhusu Al-Khalil, Ibrahim (as),

[وَنَجَّيْنَاهُ وَلُوطًا إِلَى الْأَرْضِ الَّتِي بَارَكْنَا فِيهَا لِلْعَالَمِينَ]

“Na tukamwokoa yeye na Luut'i tukawapeleka kwenye nchi tulio ibariki kwa ajili ya walimwengu wote.” [Surah Al-Anbiyya 21:71].  Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

[وَجَعَلْنَا بَيْنَهُمْ وَبَيْنَ الْقُرَى الَّتِي بَارَكْنَا فِيهَا قُرًى ظَاهِرَةً وَقَدَّرْنَا فِيهَا السَّيْرَ سِيرُوا فِيهَا لَيَالِيَ وَأَيَّامًا آمِنِينَ]

“Na baina yao na miji mingine tuliyo ibariki tuliweka miji iliyo dhaahiri, na tukaweka humo vituo vya safari. Tukawaambia: Nendeni humo usiku na mchana kwa amani.” [Surah As-Saba 34:18]. Ingawa uchamungu ni kipimo cha wema miongoni mwa watu, Muumba (swt) amewatenga watu wa ash-Sham, na hasa watu wa Palestina, kwa baraka ya wema. Mtume (saw) alipendekeza kuishi ash-Sham na akasema, «عَلَيْكَ بِالشَّامِ فَإِنَّهَا خِيَرَةُ اللَّهِ مِنْ أَرْضِهِ يَجْتَبِي إِلَيْهَا خِيَرَتَهُ مِنْ عِبَادِهِ»  “Nenda ash-Sham, kwani hiyo ndio bora zaidi ya ardhi za Mwenyezi Mungu, humo huwakusanya bora katika waja wake.” [Abu Daud, Ahmad]. Mtume (saw) amesema, اللهَ عزَّ وجلَّ قد تكفَّل لي بالشَّامِ وأهلِه  “Mwenyezi Mungu (swt) aichunga kwa ajili yangu Sham na watu wake.” Ibn Abbas (ra) amesimulia kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema, «أَوَّلُ هَذَا الْأَمْرِ نُبُوَّةٌ وَرَحْمَةٌ ، ثُمَّ يَكُونُ خِلَافَةً وَرَحْمَةً ، ثُمَّ يَكُونُ مُلْكًا وَرَحْمَةً ، ثُمَّ يَكُونُ إِمَارَةً وَرَحْمَةً ، ثُمَّ يَتَكادَمُونَ عَلَيْهِ تَكادُمَ الْحُمُرِ فَعَلَيْكُمْ بِالْجِهَادِ ، وَإِنَّ أَفْضَلَ جهادِكُمُ الرِّبَاطُ ، وَإِنَّ أَفْضَلَ رباطِكُمْ عَسْقَلَانُ» “Mwanzo wa jambo hili ni tume na rehma, kisha itakuwepo Khilafah na rehma, kisha utakuwepo ufalme na rehma, kisha itakuwepo Imarah na rehma, kisha watapigania mamlamka mithili ya wanavopigana punda. Basi shikamaneni na Jihad, na jihad yenu bora ni Ribat (kulinda mipaka), na Ribat yenu bora zaidi ni ‘Asqalan (Ashkelon).” [At-Tabarani]. Ashkelon iko 20 km kutoka Gaza.

Umwagaji damu uwa dhulma ni jinai kwa mujibu wa sheria ya Mwenyezi Mungu (swt), na ni uhalifu ulioje! Hakuna yeyote mwenye kuasi sheria hii kwa mujibu wa yale yaliyobatilishwa, isipokuwa wahalifu waliozikadhibisha sheria za Mwenyezi Mungu (swt), wakaipotosha, wakaizulia uongo, na wakatoka na hoja za kughushi. Hao ndio waliotosheka kuwa watungaji sheria, badala ya Mwenyezi Mungu (swt). Kwa hivyo walikuja na mifumo ya kibinadamu iliyo tungwa na akili za wapagani na mashoga. Hivyo wakaihalalisha damu ambayo Mwenyezi Mungu (swt) ameilinda kwa kauli yake (swt),

[مِنْ أَجْلِ ذَٰلِكَ كَتَبْنَا عَلَىٰ بَنِي إِسْرَائِيلَ أَنَّهُ مَن قَتَلَ نَفْسًا بِغَيْرِ نَفْسٍ أَوْ فَسَادٍ فِي الْأَرْضِ فَكَأَنَّمَا قَتَلَ النَّاسَ جَمِيعًا وَمَنْ أَحْيَاهَا فَكَأَنَّمَا أَحْيَا النَّاسَ جَمِيعًا ۚ وَلَقَدْ جَاءَتْهُمْ رُسُلُنَا بِالْبَيِّنَاتِ ثُمَّ إِنَّ كَثِيرًا مِّنْهُم بَعْدَ ذَٰلِكَ فِي الْأَرْضِ لَمُسْرِفُونَ]

“Kwa sababu ya hayo tuliwaandikia Wana wa Israili ya kwamba aliye muuwa mtu bila ya yeye kuuwa, au kufanya uchafuzi katika nchi, basi ni kama amewauwa watu wote. Na mwenye kumuokoa mtu na mauti ni kama amewaokoa watu wote. Na hakika waliwajia Mitume wetu na hoja zilizo wazi. Kisha wengi katika wao baada ya haya wakawa waharibifu katika nchi.” [Surah Al-Ma'idah 5:32]. Mtume (saw) amesema, «لاَ يَحِلُّ دَمُ امْرِئٍ مُسْلِمٍ إِلاَّ بِإِحْدَى ثَلاَثٍ كُفْرٌ بَعْدَ إِسْلاَمٍ أَوْ زِنًا بَعْدَ إِحْصَانٍ أَوْ قَتْلُ نَفْسٍ بِغَيْرِ نَفْسٍ» “Si halali damu ya Muislamu kumwagwa isipokuwa kwa moja katika mambo matatu: ukafiri baada ya kukubali Uislamu, au zinaa baada ya ndoa, au kuuwa nafsi isiyo na hatia.” [Abu Daud]. Hakika, utukufu wa damu ya Muislamu ni mkubwa zaidi machoni mwa Mwenyezi Mungu (swt) kuliko utukufu wa Kaaba na ulimwengu mzima. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema, «وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ لَقَتْلُ مُؤْمِنٍ أَعْظَمُ عِنْدَ اللَّهِ مِنْ زَوَالِ الدُّنْيَا»  “Naapa kwa yule ambaye nafsi yangu iko mikononi mwake, kumuua muumini ni jambo kubwa sana kuliko kuangamia dunia nzima.” [An-Nisa'a]. Ibn Majah amesimulia kutoka kwa Ibn Umar (ra) ambaye amesema, nilimuona Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akifanya Tawwaf katika Al-Ka'aba na akasema, «مَا أَطْيَبَكِ وَأَطْيَبَ رِيحَكِ مَا أَعْظَمَكِ وَأَعْظَمَ حُرْمَتَكِ وَالَّذِي نَفْسُ مُحَمَّدٍ بِيَدِهِ لَحُرْمَةُ الْمُؤْمِنِ أَعْظَمُ عِنْدَ اللَّهِ حُرْمَةً مِنْكِ مَالِهِ وَدَمِهِ وَأَنْ نَظُنَّ بِهِ إِلاَّ خَيْرًا»  “Una uzuri ulioje na harufu yako ni nzuri ilioje! Una ukubwa ulioje na ukubwa wa utukufu wako! Naapa kwa yule ambaye nafsi ya Muhammad (saw) iko mikononi mwake, utukufu wa muumini ni mkubwa zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu (saw) kuliko utukufu wako, mali yake, na damu yake, na tusimdhanie isipokuwa kheri.”

Kutokana na nususi hizi za Kisheria, na nyingi nyinginezo, inadhihirika kuwa jinai zinazofanywa katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina ni jinai kubwa zenye matokea mabaya. Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

[وَمَنْ يَقْتُلْ مُؤْمِنًا مُتَعَمِّدًا فَجَزَاؤُهُ جَهَنَّمُ خَالِدًا فِيهَا وَغَضِبَ اللَّهُ عَلَيْهِ وَلَعَنَهُ وَأَعَدَّ لَهُ عَذَابًا عَظِيمًا]

“Na mwenye kumuuwa Muumini kwa kukusudia, basi malipo yake ni Jahannamu humo atadumu, na Mwenyezi Mungu amemkasirikia, na amemlaani, na amemuandalia adhabu kubwa.” [Surah An-Nisaa 4:93]. Kama ambavyo Mayahudi wanastahiki adhabu ya Mwenyezi Mungu kwa jinai hii, pamoja na serikali za Magharibi na watawala wa Kiarabu na wa Waislamu ambao ni watiifu na wanawaunga mkono, vivyo hivyo Muislamu hatapata radhi za Mwenyezi Mungu kama atakaa kimya juu ya uovu huu. Imepokewa na At-Tirmidhi kutoka kwa Abdullah ibn Masud (ra) ambaye amesema, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema, «لَمَّا وَقَعَتْ بَنُو إِسْرَائِيلَ فِي الْمَعَاصِي نَهَتْهُمْ عُلَمَاؤُهُمْ فَلَمْ يَنْتَهُوا فَجَالَسُوهُمْ فِي مَجَالِسِهِمْ وَوَاكَلُوهُمْ وَشَارَبُوهُمْ فَضَرَبَ اللَّهُ قُلُوبَ بَعْضِهِمْ بِبَعْضٍ وَلَعَنَهُمْ عَلَى لِسَانِ دَاوُدَ وَعِيسَى ابْنِ مَرْيَمَ ذَلِكَ بِمَا عَصَوْا وَكَانُوا يَعْتَدُونَ»  “Pindi wana wa Israel walipotumbukia kwenye maasi wanazuoni wao waliwakataza lakini hawakukatazika. Basi wakakaa nao katika baraza zao, wakala nao na wakanywa nao. Basi Mwenyezi Mungu akazigonganisha nyoyo zao wao kwa wao na akawalaani kupitia ulimi wa Daud na Isa mwana wa Maryam. Hiyo ni kwa sababu waliasi na walikuwa wakivuka mipaka.” Abu Daud pia amesimulia kwamba Ibn Masud (ra) amesema, “Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,  «كَلَّا، وَاللَّه لَتَأْمُرُنَّ بِالْمَعْرُوفِ، وَلَتَنْهَوُنَّ عَنِ الْمُنْكَرِ، ولتَأْخُذُنَّ عَلَى يَدِ الظَّالِمِ، ولَتَأْطرُنَّهُ عَلَى الْحَقِّ أَطْرًا، ولَتَقْصُرُنَّهُ عَلَى الْحَقِّ قَصْرًا، أَوْ لَيَضْرِبَنَّ اللَّه بقُلُوبِ بَعْضِكُمْ عَلَى بَعْضٍ، ثُمَّ ليَلْعَنكُمْ كَمَا لَعَنَهُم»  “Hapana, naapa kwa Mwenyezi Mungu, hamtaacha kuamrisha mem ana hamtaacha kukataza maovu, na hamtaukamata mkono wa dhalimu na mumshawishi atende haki, isipokuwa Mwenyezi Mungu atazigonganisha nyoyo zenu nyinyi kwa nyinyi kisha akulaanini kama alivyo walaani wao.”

Umma wa bilioni mbili, pamoja na majeshi yake makubwa, una uwezo mkubwa zaidi wa kuikamata mikono ya wale ambao Mwenyezi Mungu (swt) amewakasirikia, Mayahudi. Mayahudi wamethibitisha uoga wao na uduni wao katika kuwakabili watu kwenye viwanja vya vita, katika vikao, na kwenye majukwaa ya fikra na elimu. Wamethibitisha hili, pamoja na wale waliowatangulia kutoka miongoni mwa dola za Kikruseda za Kimagharibi. Hakuna udhuru kwa mtu kukaa kimya. Wajibu wa kutafuta msaada kwa ajili ya waliodhulumiwa katika Ardhi Iliyobarikiwa uko juu yake, hata kama si mwanajeshi. Al-Awzaa'i (لأوزاعي ) (rh) amesema, "ما من مسلم إلا وهو قائم عَلَى ثَغْرَةٍ مِنْ ثُغَرِ الإِسْلامِ ، فمن استطاع ألا يُؤْتَى الإِسْلامُ من ثغرته فليفعل"  “Ilisemwa kuwa hakuna Muislamu  yeyote asipokuwa anasimama kulinda mipaka ya Uislamu, hivyo yeyote anayeweza kuzuia Uislamu usihujumiwe au kushambuliwa, basi na afanye hivyo.” Aalim, msomi, daktari, mlinzi, na umma kwa jumla wana wajibu wa

Shariah wa kuyaita majeshi kutekeleza wajibu wao wa dharura. Sasa inafahamika kuwa ukombozi wa Palestina utafanywa tu kupitia majeshi ya Kiislamu. Kwa hiyo, watawala watiifu kwa Mayahudi, wale wanaowaunga mkono, na wale wanaozuia Umma usiwanusuru ndugu zao lazima wapinduliwe. Majeshi lazima yahamasishwe kwa yale waliyojitayarisha kwayo, kupigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu (swt) chini ya Khilafah Rashida kwa Njia ya Utume.

Kama ambavyo kuwafukuza Mayahudi ni wajibu kwa Waislamu, ni lazima kwa wasiokuwa Waislamu Mashariki na Magharibi kukemea jinai hizo na kuzikana serikali zao ambazo zinaegemea upande wa giza, na kunyamazia kimya mauaji hayo. Nchi za Magharibi zinazoiunga mkono dola hii jeuri, ili kutumikia maslahi yao kwa kueneza ufisadi miongoni mwa watoto wa Umma wa Kiislamu. Vile vile wanaiunga mkono dola hii ya kihuni ili kuhakikisha kwamba Waislamu hawaunganishwi chini ya mfumo wa Mwenyezi Mungu uliowaleta wao pamoja, Khilafah katika Njia ya Utume. Ni Khilafah ndiyo iliyowatendea haki Waislamu na wasiokuwa Waislamu kwa mujibu wa amri ya Mwenyezi Mungu na sheria yake yenye uvumilivu. Mawingu yamekuwa wazi kwa ajili ya watu. Ukweli wa Mayahudi waliokaa katika ardhi waliyoharamishiwa tangu zama za bwana wetu Musa (as), na ukatili wao katika ardhi za Kiislamu zisizokuwa zao, umedhihirika, kwa wengi wa watu wa dunia, hivi kwamba watu wote sasa wanawalaani. Iwapo watu wa dunia watakaa kimya kuhusu viongozi wao madhalimu na kuwakubali kama wawakilishi wao, watakuwa mashahidi wa uongo na washirika katika uhalifu. Umma wa Kiislamu hautawasahau wale walioudhulumu, wala hautawadhulumu wale walioufanyia uadilifu. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[لَتَجِدَنَّ أَشَدَّ النَّاسِ عَدَاوَةً لِلَّذِينَ آمَنُوا الْيَهُودَ وَالَّذِينَ أَشْرَكُوا وَلَتَجِدَنَّ أَقْرَبَهُمْ مَوَدَّةً لِلَّذِينَ آمَنُوا الَّذِينَ قَالُوا إِنَّا نَصَارَى ذَلِكَ بِأَنَّ مِنْهُمْ قِسِّيسِينَ وَرُهْبَانًا وَأَنَّهُمْ لَا يَسْتَكْبِرُونَ]

“Hakika utawakuta walio shadidi kuliko watu wote katika uadui kwa walio amini ni Mayahudi na washirikina. Na utawakuta walio karibu mno kwa mapenzi ni wale wanao sema: Sisi ni Manasara. Hayo ni kwa sababu wapo miongoni mwao makasisi na wamonaki, na kwa sababu wao hawafanyi kiburi.”  [Surah Al-Maidah 5:82].

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu