Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Mateso ya Kashmir, Je hayana Mwisho?

Na: Bilal Al-Muhajir – Pakistan*

(Imetafsiriwa)

Vurugu lilitokea baina ya mamia ya waandamanaji na majeshi ya serikali mnamo Mai 13 katika Kashmir iliokaliwa na India, baada ya kuuliwa kijana wa miaka 25 Mahruddin Bir Shah. Aliyekuwa anaendesha gari, wakati vikosi vya kijeshi vya India vilipo mpiga risasi, karibu na kituo cha upekuzi pambizoni mwa Srinagar, mji mkuu wa Kashmir Iliyo Kaliwa. Shah alipigwa risasi, huku polisi wakidai, kwa sababu alikataa kusimama katika kituo cha upekuzi! Hata hivyo, baba yake, Ghulam Nabi, alipinga taarifa hiyo ya polisi na kusema kwamba “mtoto wake alipigwa risasi kinyama.” Mauaji ya kijana huyu, Mahruddin, yamejiri huku kukiwa na ongezeko la taharuki katika Kashmir iliokaliwa yenye Waislamu wengi, baada ya New Delhi kufutilia mbali uhuru wa kujitawala wa Kashmir, na kuweka amri ya kutotoka nje tangu Novemba 1, 2019, ili kudibithi mchafuko. Hili linajiri huku kukiwa na marufuku kamilifu ya matembezi nchini India, ili kupigana dhidi ya kusambaa kwa virusi vya Korona, huku maelfu ya wanajeshi na polisi wakipelekwa katika vituo vya upekuzi, ili kupunguza matembezi.

Awali, kamanda wa operesheni za kundi kubwa la jihadi Kashmir, Hizb ul Mujaheedin, aliuwawa mnamo 6 Mei 2020, baada ya makabiliano marefu na majeshi ya dola ya Kibaniani ya kigaidi. Mamia ya majeshi ya India yalianzisha operesheni ya kijeshi baada ya kupokea habari za ujasusi kwamba Riad Naik, kamanda wa Hizb ul Mujahideen, amejificha katika kijiji cha wilaya ya Pulwama, kusini mwa Kashmir. Kwa zaidi ya muda wa miezi miwili, jeshi la kigaidi la India limewaua wapiganaji 36. Kashmir iliokaliwa imekuwa ikishuhudia upinzani mkali na wa kuendelea kwa miongo mingi, ikipelekea zaidi ya mashahidi elfu sabiini. Katika eneo la Azad (iliyo kombolea) Kashmir, mwanajeshi mmoja na wanawake wawili waliuwawa baada ya majeshi ya India kulenga vituo vya uangalizi na vijiji. Taarifa kutoka kwa jeshi la Pakistan liliikashifu India kwa “ukiukaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano.” Shambulizi hilo pia liliwajeruhi mtoto na mwanamke mwengine.

Katika kujibu uhalifu huu ulio tekelezwa na India dhidi ya haki za Waislamu katika Kashmir iliokaliwa, kukiuka Laini ya Udhibiti na kuwaua Waislamu upande wa Pakistan, Wizara ya Kigeni ya Pakistan ilimuita balozi wa India ili kuelezea “upingaji na kukataa kwao kwa kuvunjwa kwa makubaliano ya usitishaji wa vita, ambako kunahatarisha mchakato wa amani katika eneo hili”!!! Hatua hizi dhaifu ziko sambamba na zile ambazo serikali zilizo tangulia za Pakistan zimetuletea. Kamwe hazijachukua hatua yoyote inayo afikiana na umbile la mzozo baina ya nchi hizo mbili na hatua dhaifu kama hizo haziwiani na umbile la jihad ya Waislamu wa Kashmir na Pakistan.

Waislamu wa Pakistan na Kashmir wamelelewa katika kupenda jihad na kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu (swt). Uadui dhidi ya Dola ya Kibaniani umepandwa ndani yao na wako tayarisha kupigana dhidi ya Mabaniani walioikalia Kashmir. Hakika wako tayari kuwakomboa Waislamu wote wanaodhulumiwa nchini India, wala si Kashmir pekee. Waislamu wengi wa Pakistan wanajichukulia kama wahamiaji, waliohama kutoka kwa ardhi zao hadi Pakistan, baada ya kugawanywa Pakistan, kutoka kwa bara dogo la Hindi. Pakistan iliundwa kiasili kama nchi ya maeneo mawili, moja ambalo ni Pakistan magharibi ya awali, ambayo sasa ndio Pakistan, na Pakistan Mashariki, ambayo sasa ndio Bangladesh. Watu wengi katika mji mkubwa wa Pakistan, Karachi, ambayo iko na idadi ya takriban watu million ishirini, wangali wanajichukulia wahamiaji, huku familia nyingi zao bado zikiwa zimegawanyika baina ya nchi mbili. Hivyo nia ya kimfumo na ya kihistoria miongoni mwa watu wa Kashmir na Pakistan yatosha kutangaza vita dhidi ya India, sio tu kumaliza uhalifu wa India dhidi ya haki za Waislamu ndani ya Kashmir pekee, bali pia kuwakomboa Waislamu wote nchini India ambao wako chini ya utawala wa kidhulma wa Mabaniani.

Uhalisia wa Waislamu katika Bara Dogo la Hindi, ikiwemo Pakistan, Kashmir, Bangladesh, na pia Afghanistan, ni uhalisia wa kuumiza. Wao ni sehemu ya Ummah bora na mara kwa mara wamethibitisha kuwa na zaidi ya uwezo wa kukabiliana na vikwazo kuwashinda wavamizi. Historia yao ya kupigana dhidi ya Raj Mkoloni wa Kiingereza inatoa ushahidi ukweli huu.

Walililazimisha jeshi la Kibepari la Kiingereza kuondoka katika eneo hilo, na kamwe halikujaribu kurudi tena kuwakalia kwa nguvu. Huku ikiwa ni ukweli kwamba Uingereza imepandikiza watawala vibaraka wake katika eneo hili, badala ya kukoloni moja kwa moja kupitia jeshi, Uingereza ilichagua kutumia njia hii kwa sababu ya nguvu ya upinzani mkali walio kumbana nao. Mfano mwingine ni ushindi wa Waislamu wa Afganistan, wakisaidiwa na Waislamu wa Pakistan, dhidi ya uvamizi wa Urusi ya Kisovieti. Ukweli ni kuwa Waislamu kamwe hawaja kabiliana na uvamizi wowote katika eneo hili, isipokuwa wameweza kuushinda, hata katika mizozo mifupi iliyotokea kati ya Waislamu wa Kashmir na Pakistan upande mmoja, na India upande mwengine. Yote haya yameishia na Ushindi kwa Waislamu, na kushindwa na kufedheheka kwa India. Mfano wa hiyo mizozo mifupi, ni mzozo wa Kargil  wa 1999, ambapo jeshi la India lilishindwa vibaya mno mikononi mwa jeshi la Pakistan. Lau kama si khiyana ya Nawaz Sharif na Pervez Musharraf, ambao walijisalimisha kwa amri za Amerika, Kashmir iliokaliwa wakati huo ingekuwa imekombolewa.

Ni ukweli kwamba Waislamu wa Kashmir wako katika shida na mateso makubwa na mikononi mwa India, tangu kugawanywa mnamo 1947. Hata hivyo, India pia inajihusisha na vita vya msuguano huko, ambavyo vinanyonya vibaya uchumi wa India. Mfano mwepesi ni kwamba India imepoteza takriban dolari bilioni moja na nusu, kwa miezi mitatu ya amri ya kutotoka nje ambayo imeiwekea Kashmir, tangu Novemba 1, 2019. Ama hasara yao ya kijeshi, pia ni kubwa mno, na hesabu ya hasara hizo hufanywa kulingana na vita walivyo ndani yake. Na kubwa zaidi kushinda hasara hizi katika kukabiliana na India, ni kukuwa kwa kujiamini kwa Waislamu katika eneo hili katika uwezo wao wa kukabilina na India na kuishinda. Hata hivyo, kile kinacho wazuia kutofanikiwa ni watawala wa eneo hili haswa watawala wa Pakistan, ambao kila mara hutelekeza na kupoteza watu katika jitihada za kuwashawishi watu kukubali “mchakato wa amani” ambao Amerika inataka kuutabikisha juu ya nchi hizo mbili. Mpango wa Amerika ni kuwawezesha watawala wote wawili wa Pakistan na Dola ya Kibaniani kuwa huru na kujitolea wenyewe kidhati katika kumkabili mshindani imara zaidi wa Amerika aliye mashariki, China, na pia dhidi ya ukuwaji wa mwamko wa Ummah ambao unafanya bidii kurudisha Khilafah kwa njia ya Utume katika eneo hili. Hata hivyo, kile wanacho kitamani makafiri kiko mbali, mbali sana. Amerika na watawala wake wameshidwa kuwazuia Waislamu katika eneo hili dhidi ya hamu yao ya kutaka ukombozi kutoka kwa mikono ya Amerika na India na wale wanao shirikiana nao miongoni mwa watawala wajinga wa Waislamu. Hakika Waislamu hawa wamekitisha nyoyoni mwao Hadith ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) inayo toa bishara njema kwao kuhusu kuikomboa India yote, wala si Kashmir pekee.

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ قَالَ: «وَعَدَنَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ غَزْوَةَ الْهِنْدِ فَإِنْ أَدْرَكْتُهَا أُنْفِقْ فِيهَا نَفْسِي وَمَالِي وَإِنْ قُتِلْتُ كُنْتُ أَفْضَلَ الشُّهَدَاءِ وَإِنْ رَجَعْتُ فَأَنَا أَبُو هُرَيْرَةَ الْمُحَرَّرُ«

“Kutoka kwa Abu Hurairah amesema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alituahidi vita vya India. Kama nataishi kuviona, nitajitolea nafsi yangu na mali yangu kwa ajili yake. Na nikiuliwa, nitakuwa bora wa mashahidi, na kama nitarudi kutoka vitani, nitakuwa ni Abu Hurairah Al-Muharrar (Aliye achwa huru na Moto)”.[An-Nasai]

Imeandikwa kwa ajili ya Gazeti la Al-Rayah Toleo 287

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu