Jumatatu, 11 Rabi' al-thani 1446 | 2024/10/14
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir kimezindua Kampeni ya Kiulimwengu:

“Beijing+25: Je, Barakoa ya Usawa wa Kijinsia Imeanguka?”

Mwaka 2020 unaadhimisha miaka 25 ya Azimio la Beijing na Mpango wa Utendaji (BPfA), ni waraka mpana ambao ulikuwa ni matokeo ya Kongamano la Kiulimwengu la nne la UN kuhusiana na Wanawake lililofanyika mnamo Septemba 1995, huko Beijing, Uchina. Lengo lake likiwa ni kupanua haki na kuboresha maisha ya wanawake ulimwenguni kupitia kuasisiwa kwa Usawa wa Kijinsia katika nyanja zote za maisha: kisiasa, kiuchumi na kijamii, na kuhusisha mitizamo ya kijinsia katika sera, sheria na mipango yote ya dola katika kila ngazi ndani ya mujtama.  Waraka ambao ulitambuliwa kuwa ndio ajenda ya ruwaza pana ya kuwawezesha wanawake na wasichana kimataifa. Azimio lilipitishwa na nchi 189, ikijumuisha serikali nyingi katika ulimwengu wa Waislamu, ambazo zilikubali kutekeleza ahadi zake ndani ya dola zao na kulingania ajenda yake miongoni mwa mataifa yao.

            Kwa miongo kadhaa, ‘Usawa wa Kijinsia’ umekuwa ndio alama ya kimataifa ya kustaarabika, kuendelea kwa dola na kiwango cha kupimia namna mataifa yanavyo watendea wanawake wao. Na pia unatizamwa na wengi kuwa ndio njia pekee ya kuwawezesha wanawake wote, kuboresha ubora wa maisha yao na kupanua maendeleo ya mataifa. Hata hivyo, miaka 25 tangu kwa BPfA na ajenda yake pana ya kumakinisha usawa wa kijinsia ulimwenguni, matatizo ya kisiasa, kiuchumi, kimazingira na kijamii yanayowakumba wanawake Waislamu duniani kote na hasa wanawake kimataifa yanabakia kutamausha na kuzidi kila kukicha. Ahadi za kuwawezesha na kuwaboreshea maisha yao hazijatimizwa.

            Hii Machi, Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir kimezindua kampeni ya kiulimwengu kwa kichwa, “Beijing+25: Je, Barakoa ya Usawa wa Kijinsia Imeanguka? Kampeni itakuwa inalenga kuipa changamoto mitazamo iliyokita ya ‘Usawa wa Kijinsia’ na madai yake ya kupigia debe haki za wanawake na maendeleo ya mataifa, na kuwasilisha misingi ya kipekee ya Uislamu ambao una ruwaza pana yenye maelezo ya kina kuhusiana misingi, sheria na nidhamu zinazotekelezwa na nidhamu yake ya kisiasa, Khilafah kwa msingi wa njia ya Utume, ambayo inatoa ruwaza mbadala ya kutegemeeka ili kunyanyua hali ya wanawake kuhifadhi haki zao na kuboresha viwango vyao vya maisha na kuleta maendeleo ya kweli ndani ya dola.

Alhamisi, 17 Rajab 1441 H sawia na 12 Machi 2020 M

         




Ili Kusoma Taarifa kwa Vyombo vya Habari

kutoka kwa Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Ikitangaza Uzinduzi wa Kampeni ya Kiulimwengu:

“Beijing+25: Je, Barakoa ya Usawa wa Kijinsia Imeanguka?”

Alhamisi, 17 Rajab 1441 H - 12 Machi 2020 M

BOFYA HAPA 

Video ya Dkt. Nazreen Nawaz
Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake Katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Akitangaza Uzinduzi wa Kampeni ya Kiulimwengu

Kitangulizi cha Kampeni

#BarakoaYaUsawaWaKijinsiaImevuliwa

#سقط_قناع_المساواة

#GenderEqualityUnmasked

#CinsiyetEşitliğiMaskesiDüştü

Kitangulizi cha Uzinduzi

   
   

   Kupakua Kipeperushi (PDF)

Bofya Hapa

 

 


Wanawake Waislamu Hawahitaji Sherehe za Kila Mwaka za Kufeli Kiulimwengu katika Kusuluhisha Matatizo ya Wanawake. Tunahitaji Khilafah itakayokuwa Mlinzi na Ngao Yetu

Dkt. Nazreen Nawaz
Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

18 Rajab 1441 H - 13 Machi 2020 M

 

 

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumatatu, 30 Machi 2020 21:28

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu