Jumanne, 20 Shawwal 1447 | 2026/04/07
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu
kesho kutwa

kesho kutwa

Vyombo vya Usalama jijini Umdurman Vyalikamata Kundi la Wanachama wa Hizb ut Tahrir

Kufuatia utekelezaji wa mashababu wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan wa visimamo vitatu katika maeneo tofauti tofauti katika jiji la Omdurman, asubuhi ya Jumatano iliyopita, 25 Rajab 1447 H, sambamba na 14/1/2026 M, ndani ya muundo wa kukumbusha tukio la kupita kwa miaka 105 tangu kuvunjwa kwa Dola ya Khilafah mwezi Rajab 1342 H, vyombo vya usalama viliendelea kuwakamata wanachama watano wa Hizb: Al-Radi Muhammad Ibrahim, Fadlallah Ali Suleiman, Omar Al-Bashir, Hassan Fadl, na Mujahid Adam. Kisha waliachiliwa baada ya Magharibi siku ya Jumatano baada ya nambari zao za simu kuchukuliwa na baada ya kunyakua mabango ambayo Mashababu hao wa Hizb ut Tahrir walikuwa wamebeba katika visimamo hivyo vitatu. Kisha waliitwa mnamo alasiri ya Alhamisi, 15/1/2026, na wangali wako kizuizini hadi wakati wa kuandika taarifa hii!!

Hitimisho la Kampeni “Khilafah sio Ndoto… Bali, ni Kilio cha Ulimwengu Unaowaka Moto!”

Leo, kwa Msaada Wake, tunahitimisha kampeni ya kimataifa iliyozinduliwa na Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir, kwa maelekezo ya Amiri wa Hizb ut Tahrir, mwanachuoni mkubwa Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, katika kumbukumbu ya miaka 105 ya kuvunjwa kwa Khilafah, ambayo iliamshwa na wanaume na wanawake wa Hizb ut Tahrir kote ulimwenguni.

Mikutano na Matembezi ya Kulaani Yaliyoandaliwa na Hizb ut Tahrir / Wilayah Bangladesh: Enyi Watu! Pingeni Mpango wa Kupeleka Jeshi Letu Gaza chini ya Kikosi Kilichopendekezwa na Trump, na Takeni Msimamo Wazi kutoka kwa Wagombea katika Uchaguzi Ujao

Hizb ut Tahrir katika Wilayah Bangladesh, iliandaa mikutano na matembezi mengi ya kulaani leo, Ijumaa (16 Januari 2026), baada ya swala ya Ijumaa, katika majengo mbalimbali ya misikiti jijini Dhaka na Chattogram, dhidi ya mpango wa kupeleka vikosi vya nchi hii kwa “Kikosi cha Kuleta Utulivu wa Kimataifa” kilichopendekezwa na Trump huko Gaza. Ili kupinga mpango huu mbaya wa Marekani, na kuwataka wagombea na vyama vya kisiasa katika uchaguzi ujao kuelezea msimamo wao kuhusu suala hili.

Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu