Hizb-ut-Tahrir Afisi Kuu ya Habari
- Imepeperushwa katika Kutuhusu
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
Fikra ambayo juu yake imebuniwa Hizb ut Tahrir, inayo wasilishwa katika wanachama wake na ambayo inafanya kazi kuuyeyusha Umma kwayo, ili uichukue kama kadhia yake, ni fikra ya Kiislamu, yaani, ‘Aqeedah ya Kiislamu pamoja na sheria zinazotokamana nayo na fikra zilizo jengwa juu yake.
jia iliyo tabanniwa na Hizb ut Tahrir kulingania da’wah ni njia ya kisheria iliyovuliwa kutoka katika seerah ya Mtume (saw) katika utendakazi wake katika ulinganizi wa da’wah.
Baada ya kusoma, kutafakari na kuchunguza kuhusu hali ya sasa ya Umma huu na kiwango ulichofikia, na hali katika zama za Mtume (saw), na katika zama za Makhalifah wanne walioongoka na katika zama za waliofuata baada yao, na kupitia kuregelea seerah na njia ambayo yeye (saw) alibeba da’wah kutoka wakati alipoanza mpaka alipo simamisha dola Madina.