- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Siku ya Kila Mwaka ya Ukumbusho Utekelezaji Wake Umeharamishwa Nchini Kazan
Habari:
Kamati ya Utendaji ya Kazan imefutilia mbali ruhusa ya Kituo cha Umma cha Tatar (ATPC) kufanya mnamo Oktoba 18 mkutano wa hadhara katika bustani ya Tinchurin kwenye hafla ya "Hәter kөne" - siku ya kila mwaka ya ukumbusho wa watetezi wa Kazan waliokufa kutoka kwa vikosi vya Kutisha vya Ivan mnamo 1552. Barua barua mkabala wa hilo iliyotiwa saini na mkuu wa idara ya kamati ya utendaji ya jiji Yevgeny Varakin ilitumwa kwa mwenyekiti wa ATPC Farit Zakiev. Zakiev mwenyewe alielezea kuhusu hili.
Mamlaka za Kazan zinaelezea kufafanua uamuzi huu kupitia amri iliyotolewa na afisi ya mwendesha mashtaka wa jiji. Hapo awali, waandishi wa habari waliripoti kwamba ATPC kwenye jaribio la tatu pekee waliweza kukubaliana juu ya kufanya "Hәter kөne", ambapo watu watatu waliletwa katika uwajibikaji wa kiidara mwaka jana, akiwemo mwandishi Fauzia Bayramova, ambaye alitozwa faini ya rubles elfu 10.
Uadhimishaji wa Siku ya Ukumbusho na wasomi wa kitaifa nchini Kazan ulianza mnamo 1989 na haujakatizwa tangu wakati huo. Mwaka jana, katika Bustani ya Tinchurin mkutano huo ulihudhuriwa na karibu watu 200. Kulingana na mwenyekiti wa ATPC, mnamo Jumatatu shirika lake litakata rufaa uamuzi huo kortini.
Maoni:
Haiwezi kusema kuwa uamuzi huu wa mamlaka ulikuwa mshangao kwa mtu. Kwa kweli, katika miaka ya hivi karibuni, mamlaka za Tatarstan zimepunguza polepole lakini kwa hakika vitendo hivi vya kila mwaka hadi kutoweka, kila wakati wakizuia zaidi na zaidi, wakisukuma hatua hiyo kutoka katika barabara kuu na viwanja katikati mwa mji huo mkuu.
Lakini kuna wakati vitendo hivi vilivutia maelfu ya watu, na kaulimbiu za vitendo hivi zilikuwa za ujasiri sana. Nyuma mnamo 2001, moja ya maandamano yalihudhuriwa na mabango kama: "Hatutaruhusiwa kuhalalisha kazi!", "Tumechoka na ukoloni wima wa dola ya Urusi!", "Asilimia 10 ilikuwa inatosha kwa Batiy, lakini hata asilimia 70 haikumtosha Putin. "Hapana" kwa ushuru wa unyonyaji!","Ikiwa unaunga mkono ubwana wa Tatarstan - jiunge na safu za Vuguvugu la Narodniy!", "Putin anapaswa "kuuawa" katika Mahakama ya Hague!" Na katika miaka ya 90, wakati maoni ya kupinga ukoloni bado yalikuwa na nguvu sana kati ya watu, haswa kwa kuzingatia vita vya Wachechen vya uhuru, maandamano kama hayo yalihitaji tu kujitenga kutoka kwa Shirikisho la Urusi. "Hatukuingia Urusi!" - waandamanaji kisha waliandika kwenye mabango.
Kukomeshwa kwa taratibu kwa maandamano haya yote kulipatikana, ni wazi, kupitia Kazan Kremlin, yaani magavana wa wakoloni wa Urusi kutoka miongoni mwa Waislamu chini ya uongozi wa Rais Minnikhanov. Na ikiwa mwanzoni mwa miaka ya 2000, wakati Rais Shaimiev alikuwa angali na ujasiri wa kuitishia Moscow kwa hisia za kujitenga na alitumia mikutano na maandamano haya kuwatisha Warusi, sasa hali ni tofauti kabisa. Baada ya makubaliano juu ya mamlaka kukosa kufanywa upya, baada ya kuvunjwa kabisa kwa ishara zote za ubwana hata ndani ya shirikisho, wasomi wa eneo hilo, wakitetemeka kwa ajili ya kuziokoa familia zao na koo zao, wako tayari kuchukua hatua yoyote kupata imani ya Moscow . Sasa haiwezekani tena kuhifadhi muonekano wa wapiganiaji haki za watu. Lazima wapewe Putin kwa kila mkutano na watoe taarifa za makusudi zinazounga mkono Urusi, wakiruhusu serikali ya Urusi na matendo yake yote bila masharti.
Watu wa Tatarstan hawapaswi tena kumtegemea ima Shaimiev au Minnikhanov, bali wanapaswa kutambua kwamba hatima yao iko mikononi mwao, kwamba sera ya maelewano na ukoloni wa Urusi chini ya visingizio vyovyote na aina zake zote kuendelea kwake ni kosa kuu tangu mwanzo.
"Hәter kөne", yaani Siku ya Ukumbusho inapaswa kuwa msingi wa ajenda mpya ya habari kati ya wanaharakati na watu wa maarufu, kwa sababu licha ya historia ndefu zaidi ya uvamizi miongoni mwa Waislamu, Watatari bado wanakumbuka uhalifu wote mbaya waliotendwa dhidi yao kwa zaidi ya karne tano zilizopita. "Hәter kөne" ni ishara kwamba licha ya ukweli kuwa leo sisi, kwa bahati mbaya, hatuwezi kuondoa mara moja ukoloni wa Kirusi, jukumu letu kama Waislamu sio kukubaliana nayo na kuichukia kwa nyoyo zetu zote.
Mwenyezi Mungu Mtukufu asema:
[وَلَن يَجْعَلَ اللَّهُ لِلْكَافِرِينَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ سَبِيلًا]
“Wala Mwenyezi Mungu hatawapa makafiri njia ya kuwashinda Waumini.” [4:141].
Imendikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Muhammad Mansur