Jumapili, 27 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/29
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Urasilimali Hautoi Akhlaqi za Kudumu,
Manufaa Ndio Thamani Pekee Yenye Kuendesha Maamuzi

Habari:

Mnamo tarehe 2 Novemba 2020, BBC iliripoti kuwa serikali ya India imeanzisha kampeni ya kupigia debe matumizi ya sukari kukabiliana na kujaa kwa sukari iliyo kosa mauzo katika makampuni. Matangazo na kampeni mpya za umma zinawatumia wanasayansi na wataalamu wa lishe ili kugeuza uelewa wa sasa wa umma kuwa ni jambo la kiafya kupunguza matumizi ya sukari iliyosafishwa.

Maoni:

Ukweli kwamba nchi ya kidemokrasia kubwa zaidi ulimwenguni imeanzisha kampeni ambayo inatumikia moja kwa moja maslahi ya biashara kwa gharama ya ustawi wa raia ni mfano wazi wa kusudi halisi la Urasilimali. Maneno "demokrasia" na "huria" ni ubabaishaji tu wa watumiaji ili kutoa hisia kwamba idadi kubwa ya watu wana maslahi katika mfumo ambao unawaona tu watu kama bidhaa za kutumiwa pekee.

Dori ya kweli ya viongozi wa ulimwenguni ni kutenda kama viongozi tasa ili waajiriwe kuhakikisha kuwa mabwana halisi wa kirasilimali wanatimiza matarajio yao yote ya kiuchumi. Hakuna maadili wala haki za binadamu na mahitaji ambayo yanaweza kuja kabla ya faida na mapato ya kimamlaka ya kipote cha wachache. Ndio maana hata ukweli wa kisayansi unaweza kupuuzwa na kupingwa, kwani ukweli unaweza kuchakachuliwa unapoingilia tuzo ya pesa.

Imenakiliwa vizuri kuwa sukari iliyosafishwa ni kemikali isiyo ya asili iliyounganishwa moja kwa moja na ncha kali katika insulin. Mwili lazima usindike ziada ya sumu ya glucose na fructose ili kuepuka madhara yanayotokana na upakiaji huu wa kupita kiasi. Imekuwa kawaida kwa madaktari na taasisi za kiulimwengu, kama WHO, kuonya juu ya ulaji wa carbohydrates iliyosafishwa ili kuzuia magonjwa mengi yanayo nasibishwa nayo. Hivi ndivyo haswa serikali ya India ilivyo fanya mnamo 2014 wakati ilipoilenga Pepsi Cola kupunguza sukari yake kwa sababu za kiafya.

Lakini, ili kuzuia hasara za sasa za kifedha za biashara, serikali ya India, kama ilivyo kila serikali nyingine, itayatoa kafara maisha ya watu wake na kutumia vibaya imani yao kulinda sanamu la pesa kwanza.

Katika mfumo wa Kiislamu, madhumuni ya dola ni kuangalia mahitaji ya raia hata kama kuna hasara katika manufaa ya kifedha. Maisha ya binadamu na usalama hayawezi kuwa ya pili kwani kuna adhabu kubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt) inayo nasibishwa na hili.

(أَهُمْ يَقْسِمُونَ رَحْمَةَ رَبِّكَ نَحْنُ قَسَمْنَا بَيْنَهُم مَّعِيشَتَهُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَرَفَعْنَا بَعْضَهُمْ فَوْقَ بَعْضٍ دَرَجَاتٍ لِيَتَّخِذَ بَعْضُهُم بَعْضًا سُخْرِيًّا وَرَحْمَتُ رَبِّكَ خَيْرٌ مِّمَّا يَجْمَعُونَ)

“Kwani wao ndio wanao gawa rehema za Mola wako Mlezi? Sisi tumewagawanyia baina yao maisha yao katika uhai wa duniani, na tukawanyanyua baadhi yao juu ya wengine kwa daraja nyingi; kwa hivyo baadhi yao wanawafanya wenginewe wawatumikie. Na rehema za Mwenyezi Mungu ni bora kuliko hayo wanayo yakusanya.” [Az-Zukhruf: 32].

 

Makhalifa watukufu wa Kiislamu wa waliopita ni viongozi wenye ikhlasi waliohakikisha kwamba raia wa Kiislamu na wasiokuwa wa Kiislamu haki zao zimelindwa na fedha za serikali zilitengwa ili kuwezesha hili kikamilifu.

Mfano huu ni mojawapo kati ya mengi ambayo yanapaswa kuwa funzo kwa Waislamu kukataa muundo wa uongozi wa sasa unaoufunga ulimwengu kwa maadili ya batili, na yanapaswa kutuhamasisha kufanya kazi ya kurudisha mifano sahihi ya serikali kwa mujibu wa njia ya Mtume (saw) na Quran.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Imrana Mohammad

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoAlhamisi, 24 Disemba 2020 14:31

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu