Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Habari na Maoni

UK Inajivunia Kuchukua Msimamo wa Kinafiki katika Vita dhidi ya Ugaidi

Habari:

Serikali ya Uingereza hivi sasa imedhamini milioni Sh60 za ujenzi wa kituo cha kupambana na ugaidi katika Mji wa Mombasa. Akizungumza akiwa Pwani katika uzinduzi wa eneo la ujenzi huo katika Makao Makuu ya Polisi Pwani, Kamishna wa Uingereza nchini Kenya, Nic Hailey alisema kuwa UK imejitolea kikamilifu kuisaidia Kenya katika kupigana na ugaidi ili kuwalinda raia wa UK na wenyeji. Hailey alisema "UK inajivunia kuwa mdhamini wa jengo jipya la ATPU hapa Mombasa. Tumeona kwa masikitiko makubwa katika miezi na miaka ya karibuni athari mbaya ya ugaidi. Umetupiga sisi ndani ya UK na hapa nchini Kenya na hivi juzi ndani ya Sri Lanka."

Maoni:

Udhamini huu sio jaribio la kwanza kutoka kwa Uingereza katika kuendeleza vita dhidi ya Waislamu chini ya bendera ya kupigana na ugaidi nchini Kenya. Mnamo 2014, Jennifer Anderson ambaye alikuwa ni Mkuu wa Kupambana na Ugaidi katika Afisi ya Kigeni na Jumuiya ya Madola ya Uingereza alikutana na wakuu wa kitengo cha ATPU ambapo aliuhutubia idara za Kenya namna ya kupambana na ugaidi. Agosti mwaka jana, katika ziara yake nchini Kenya, Waziri Mkuu Theresa May aliahidi upanuzi wa kituo cha kupambana na ugaidi ili kiwe kituo cha kieneo. Majaribio yote haya yanafichua misukumo miovu ya UK ikilenga kuendeleza ukandamizaji na uvamizi wa Uislamu na Waislamu. Kwa masikitiko idara za Kenya ziko tayari kuelekeza risasi dhidi ya raia wake kama ripoti kutoka kwa Human Rights Watch ambazo zimeashiria kuhusika kwa ATPU katika kesi za mauaji, upotezaji wa watu, kudhuru au kuhangaisha washukiwa wa ugaidi nchini.

Ama kuhusu kujitolea kwa Serikali ya Uingereza katika kupigana na ugaidi, hakika huu ni mtizamo wa kinafiki kutoka kwa idara za Uingereza. Hivi sasa Serikali ya Uingereza imetumana wanajeshi waliobeba mabomu kwenda kuwatisha watu wa Libya. Ulimwengu hauto sahau muungano wa Bush na Blair ulio vamia Iraq ambapo mamilioni ya Waislamu wasiokuwa na hatia walipoteza maisha yao. Hapa nchini Kenya, wanajeshi wa Uingereza wanajulikana kwa unyama waliofanya ikijumuisha kubaka na kutia kororoni pasina makosa.

Ni wazi kabisa kuwa 'vita dhidi ya ugaidi' duniani ni vita vilivyo dhaminiwa na Wamagharibi kuushambulia Uislamu kimfumo. Katika mahojiano na BBC aliyekuwa Waziri Mkuu Tony Blair alitoa matamshi akielezea kuwa Uislamu wa siasa kali ni tishio kubwa ambalo linaukumba ulimwengu leo. Kiujanja, sheria za kupambana na ugaidi zinazo pitishwa na nchi changa huwa ni kutokana na msukumo wa tawala za Kimagharibi. Tawala za Kimagharibi zimefeli kikamilifu kupigana na Uislau kifikra na kimfumo, ikiwapelekea kukumbatia kila aina ya njia za mateso na ukandamizaji dhidi ya Waislamu.

Kwa kuwa sasa ni wazi kwa ulimwengu wote kuwa Urasilimali umefeli kiuchumi, kisiasa na kijamii, UK imeungana na dola kubwa duniani Amerika kufanya kazi pamoja kuweka vizuizi dhidi ya Uislamu kama mfumo mbadala ambao unaweza kutatua matatizo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii yanayo ukumba ulimwengu leo. Wanasiasa na mashirika ya uchambuzi ya Kimagharibi wanaona tishio la Uislamu la kuibuka kwa dola kubwa duniani ambayo itauondosha mfumo wao fisadi wa kirasilimali. Hivyo basi wanatumia vita dhidi ya ugaidi kupambana na Uislamu. Jamii ya Waislamu wanatakiwa kuinuka na kulingania Uislamu kwa kutumia njia ya kifikra ya kindani na ya kisiasa pasina kutumia nguvu ili kuonyesha kuwa Uislamu ni muongozo kamili kwa wanadamu.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Kenya

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 09 Agosti 2020 06:32

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu