Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Habari na Maoni 

Mzozo wa Bahari Kati ya Kenya na Somalia: Mzozo wa Kikoloni Kuhifadhi Maslahi ya Mabwana Wamagharibi

Habari

Mzozo wa eneo katika Bahari ya Hindi kati ya Kenya na Somalia umezidi moto baada ya Nairobi kuamua kukata mahusiano ya kidiplomasia na Mogadishu kwa sababu ya madai kuwa Somalia imepiga mnada maeno ya mafuta yaliyoko katika eneo la mzozo. Eneo lilopo katika mzozo ni mraba mwembamba katika Bahari ya Hindi uliyo na urefu wa maili 62,000. (standardmedia.co.ke)

Maoni

Serikali Kuu ya Somalia iliyoko Mogadishu na inayoongozwa na Mohamed Abdullahi Mohamed "Farmajo" imeegemea Marekani. Tangu Farmajo alipoingia mamlakani mnamo 16 Februari 2017, utawala wake umekuwa ukipata upinzani kutoka kwa Majimbo wanachama wa Somalia yanaoegemea Uingereza na yakiongozwa Ahmed Mohamed Islam "Sheikh Ahmed Madobe" ambaye ndiye kiongozi/rais wa Jimbo la Jubaland nchini Somalia ambao mjini wake ni Kismayo. Viongozi hao wanaoegemea Uingereza waliandaa mkutano wao wa kwanza mnamo Oktoba 2017 na mkutano wa pili mnamo Septemba 2018 ambao ulihudhuriwa na marais – Abdiweli Mohamed Ali Gaas (Puntland), Ahmed Duale Gelle (Galmudug), Mohamed Abdi Ware (Hirshabelle), Sharif Hassan Sheikh Aden (Jimbo la Kusini Magharibi) na Sheikh Ahmed Madobe wa Jubaland ambaye alikuwa mwenyeji wa mkutano huo. Hisia za maoni katika mikutano yote viongozi hao waliitisha kusitishwa kwa mahusiano kati ya serikali za majimbo na serikali kuu (Mogadishu) kwa kisingizio kuwa Rais Farmajo ameshindwa kupigana na Al Shabaab na muendelezo wake wa kuingilia mambo ya ndani ya serikali za majimbo. Sheikh Ahmed Madobe alikuwa gavana wa Kismayo kuanzia 2006 chini ya Muungano wa Mahakama za Kiislamu (ICU) kabla kuvunjwa na uvamizi wa Ethiopia iliyoegemea Marekani.

Serikali ya Kenya inayoegemea Uingereza iliingia Somalia kuhifadhi maslahi ya bwana wake. Hivyo basi, Jeshi la Ulinzi wa Kenya (KDF) mnamo 16 Oktoba 2011 kwa kisingizio cha "kupambana na ugaidi" iliivamia Somalia na kujumuika safu moja na Sheikh Ahmed Madobe ambaye alikuwa anaongoza Kundi la Ras Kamboni, ambalo ni kundi la kijeshi lililotokana na Vuguvugu la Ras Kamboni. Kwa pamoja wakaikomboa Kismayo na hivi sasa iko chini ya Madobe kama rais wa Jimbo la Jubaland Somalia. Eneo la mzozo ambalo lina utajiri wa mafuta linapakana na Jimbo la Jubaland Somalia.

Serikali Kuu ya Somalia ambayo inaegemea Marekani ilipoona hatari inayotokamana na majimbo yanayoegemea Uingereza wakiongozwa na Sheikh Ahmed Madobe wakazindua kampeni pana ya kuwabadilisha viongozi wa majimbo. Hivyo basi, njama zao zikapelekea kubadilishwa kwa Sharif Hassan Sheikh Aden (Jimbo la Kusini Magharibi) akaingia Abdiaziz Hassan Mohamed, aliyekuwa katika serikali kuu kama waziri wa kawi na rasilimali za maji kwa kushinda kura mnamo Jumatano, 19 Disemba 2018. Abdiweli Mohamed Ali Gaas (Puntland) akaondoshwa na kuingia Said Abdullahi Deni, aliyekuwa katika serikali kuu kama waziri wa mipango kwa kushinda kura mnamo Jumanne, 8 Januari 2019. Matokeo ya uchaguzi wa majimbo yaliyobakia ya Hirshabelle, Jubaland na Galmadug hayajulikani lakini inaonesha wazi kuwa uongozi wa serikali za majimbo una wasiwasi kiasi kwamba mnamo Oktoba 2018 Mohamed Abdi Ware (Hirshabelle) alitangaza kuwa atashirikiana na serikali kuu (Mogadishu) na matokeo ya uchaguzi wa Agosti 2019 katika kinyang'anyiro cha Jubaland ambapo Sheikh Ahmed Madobe anaona aking'olewa mamlakani na serikali kuu!

Kutokana na sababu hizo ni wazi kuwa kelele za mzozo wa hivi majuzi kati ya Kenya na Somalia si chochote isipokuwa ni njama za kisiasa kati ya mataifa koloni yakijaribu kupingana kwa mujibu wa maamrisho ya mabwana zao wamagharibi ambayo yanalenga kuhifadhi maslahi yao. Somalia ikaipa onyo Kenya kwa kuwa mwenyeji wa Kongamano la Mafuta ya Somalia mjini London mnamo 7 Februari 2019. Kenya kwa upande mwingine, ikajibu kwa hasira kutokana na tishio kubwa kwa maslahi ya bwana wake nchini Somalia na hususan Jimbo la Jubaland. Ikimaanisha kuwa kura zinazokuja Agosti 2019 ndani ya Jubaland ni tishio la moja kwa moja kwa Uingereza.

Kenya na Somalia zinatawaliwa na mfumo batili wa kisekula wa kirasilimali na nidhamu zake zinazonuka ikijumuisha Demokrasia. Mfumo muovu unaojali tu uporaji wa rasilimali kupitia makampuni ya kimagharibi na kuwaacha watu katika hali za umasikini wa kupindukia! Zaidi ya hayo, Somalia ni ardhi ya Waislamu ambayo miji yake ya kisasa kama Mogadishu ilikuwa chini ya Khilafah ya Abdul Malik Marwan. Mnamo 1875, Waislamu waliiteka Kismayo na ikawekwa chini ya Khilafah Uthmaniyya ikitawaliwa na Sultan Abdul Aziz bin Mahmoud II na kuunganishwa katika Wilaya ya Misri chini ya Wali Ismail Pasha.

Suluhisho msingi na dharura kwa mzozo wa bahari ni kwa uongozi wa nchi mbili hizo na hususan Somalia kwa kuwa ni taifa la Waislamu kukata mahusiano yake ya kimataifa na kukumbatia mwito wa kurudisha tena maisha ya Kiislamu kwa kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume. Khilafah iliyosimamishwa kwa kutozingatia mipaka ya kikoloni ambayo inalenga kuleta husuma kati ya watu kwa kupia debe utaifa! Wakati huo huo rasilimali zinasambazwa kwa haki kati ya raia chini ya Khilafah ili kuhakikisha mahitaji msingi ya watu binafsi, mujtama na ya ziada ya watu binafsi yanakidhiwa kwa ukamilifu ndani ya uwezo wake. Ama kwa taifa la Kenya lisilokuwa la Waislamu ni lazima liurudie Uislamu kama mfumo, liusome na kuulinganisha pasi na kutia maanani tafsiri za kimagharibi juu ya Uislamu. Ni chini ya Khilafah pekee ndipo Kenya, Somalia, Afrika na ulimwengu kwa ujumla utakapopata utulivu, maendeleo na ustawi wa kweli kutokana na utekelezwaji kikamilifu wa Shari'ah (Qur'an na Sunnah) chini ya Khalifah muadilifu anayeongozwa na Uislamu PEKEE.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Ali Nassoro Ali
Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Kenya

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 09 Agosti 2020 06:35

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu