Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Ni Nani Atakayewapa Makaazi ya Kweli Waislamu wa Rohingya Wanaotapatapa?

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mnamo tarehe 4 Juni, mashua iliyokuwa na wakimbizi 81 wa Rohingya, wakiwemo wanawake 49 na watoto 11 iliegesha katika mwambao wa Kisiwa cha Idaman, karibu na pwani ya Mkoa wa Aceh Indonesia, baada ya kuelea kwa zaidi ya siku 100 baharini. Watu tisa waliokuwa wameabiri mashua hiyo walifariki wakati wa safari yake ya hatari. Waislamu hawa wa Rohingya wanaotapatapa walikuwa wameacha kambi za wakimbizi zilizojaa watu wengi, ovyo na zilizo na magonjwa nchini Bangladesh kutafuta maisha bora katika nchi jirani. Lakini, walikataliwa kuingia India, Malaysia, na kuingia tena Bangladesh. Baada ya kufika kwenye kisiwa cha Indonesia, inaripotiwa pia kwamba polisi wa eneo hilo waliwataka wakimbizi hao kurudi kwenye mashua yao na kuondoka bahari ya Indonesia, lakini walikataa. Sasa wanasubiri uamuzi kutoka kwa mamlaka za Indonesia kuamua hatma yao ikiwa wanaweza kubaki au wataregeshwa baharini. Hata wakipewa ruhusa ya kuingia nchini humo, hawataruhusiwa kufanya kazi au kukaa kwa kudumu kulingana na sera na sheria za kinyama za kitaifa zinazotekelezwa na serikali ya Indonesia.

Maoni:

Wakati huo huo, mnamo Juni 1, Waislamu wa Rohingya kwenye Kisiwa cha Bhasar Char kilicho na ukiwa ambacho walikuwa wamehamishiwa kutoka kambi ya wakimbizi ya Cox na serikali ya Bangladesh, walipigwa na polisi wa Bangladesh wakati walipojaribu kulalamikia hali yao mbaya ya maisha kwa maafisa wa UN waliotembelea makaazi hayo. Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa limesema katika taarifa kwamba lilipokea ripoti za majeruhi wakati wa tukio hilo, wakiwemo wanawake na watoto. Bhasar Char ni kisiwa chenye kukumbwa na kimbunga na mafuriko katika Ghuba ya Bengal ambapo wakaazi wake wakimbizi wa Rohingya wanaishi chini ya hali kama ya gereza na kunapatikana tu chakula cha msingi ambacho hakijumuishi mboga, nyama au samaki, na bila ya kazi au huduma kama shule sahihi na huduma ya afya. Mamlaka za Bangladesh tayari zimehamisha Rohingya 18,000 kwenda kisiwa hicho kutoka kambi za wakimbizi za bara, kati ya 100,000 waliopangwa, na ahadi kwamba wataweza kufanya kazi, kulima na kuvua samaki katika eneo lao jipya ambalo ilitokea kuwa uongo kabisa. Uzito wa hali yake mbaya unaweza kutathminiwa na ukweli kwamba wakaazi wa kisiwa hicho wameelezea hali mbaya na duni ya kambi ya wakimbizi ya Cox Bazar katika bara la Bangladesh, nyumbani kwa takriban wakimbizi milioni 1 wa Rohingya, kuwa ni bora mara elfu kuliko Bhasan Char. Wakimbizi wengi wamekamatwa na kupigwa kwa kujaribu kutoka kisiwa hicho, wakiwemo wanawake na watoto, na pia kumekuwa na ripoti za mateso na unyanyasaji mikononi mwa vikosi vya Bangladesh katika kisiwa hicho. Kulingana na shirika la Human Rights Watch, watoto wameadhibiwa kwa kuondoa tu katika maeneo yao waliyotengewa. Mnamo Aprili mwaka huu kwa mfano, iliripotiwa kuwa baharia mmoja wa Bangladesh aliwapiga watoto 4 wa Rohingya na paipu ya plastiki kwa kuondoka makao yao kucheza na watoto wa wakimbizi katika eneo jengine.

Mateso, shida, na kutapatapa kwa Waislamu wa Rohingya ni kwenye kuendelea. Sio tu kwamba wamefanywa kuwa wasio na dola kwa kukataliwa uraia nchini Myanmar, nchi ambayo wao na familia zao wamekuwa wakiishi kwa vizazi vingi, lakini hakuna ardhi leo ambapo wanaweza kufurahiya maisha mazuri yenye ulinzi; hakuna ardhi ambayo iko tayari kuwapa makao ya heshima; hakuna ardhi ambapo wanaweza kupaita nyumbani. Hawa ni Waislamu ambao tayari wameteseka uhalifu wa kutisha usiosemeka kama wahanga wa mauaji ya halaiki - kile ambacho Umoja wa Mataifa ulikitaja kama "mfano wa kitabu cha mauwaji ya kikabila". Lakini, badala ya kuwakaribisha kama kaka na dada zao Waislamu na kuwapa mahali salama pa kuishi na kufanikiwa kama vile Mwenyezi Mungu (swt) anavyo amuru, serikali hizi za Waislamu zisizo na huruma, zilizoleweshwa na maadili na nidhamu ya kinyama ya kikafiri ya Kimagharibi ya kitaifa, zinawatazama kama mzigo kwa uchumi wao na kuwafukuza Waislamu hawa wa Rohingya wanaotapatapa kutoka fukwe zao, kuwaweke katika kambi za vifo, au kuwanyima haki za kimsingi, licha ya ukweli kwamba Mtume (saw) amesema waziwazi:

«الْمُسْلِمُ أَخُو الْمُسْلِمِ لَا يَظْلِمُهُ وَلَا يَخْذُلُهُ» “Muislamu ni ndugu ya Muislamu: hamdhulumu wala hamtelekezi”.

Leo, kwa kukosekana kwa Nidhamu ya Mwenyezi Mungu (swt) - Khilafah kwa njia ya Utume, mlezi na ngao ya Waumini, Waislamu wa Rohingya pamoja na Waislamu wengine wanaokimbia mauaji ya halaiki na mateso, kama ilivyo nchini Syria na Turkestan Mashariki, wanakabiliwa na matarajio ya kuishi maisha mabaya ya kudumu chini ya bendera ya 'hadhi ya mkimbizi', waliokataliwa na ardhi wanazotafuta makaazi, na huku wakiwa bila ya makao halisi ambayo wanaweza kuhisi kutunzwa na salama. Kinyume chake, Khilafah ni dola ambayo inaepusha na kupinga utaifa, kwani Mtume (saw) amesema:

«لَيْسَ مِنَّا مَنْ دَعَا إِلَى عَصَبِيَّةٍ وَلَيْسَ مِنَّا مَنْ قَاتَلَ عَلَى عَصَبِيَّةٍ وَلَيْسَ مِنَّا مَنْ مَاتَ عَلَى عَصَبِيَّةٍ»

“Si katika sisi anayelingania Assabiyah (ukabila na utaifa), na si katika sisi anayepigana kwa ajili ya Assabiyah na si katika sisi anayekufa kwa ajili ya Assabiyah.” Badala yake, itatoa haki sawa za uraia kwa wale wanaotaka kuishi chini ya utawala wake - bila kujali imani ya kidini, rangi au kabila, kama Uislamu inavyowajibika - kuwakaribisha wale wanaotafuta hifadhi ndani ya ardhi yake, kuwaadhibu wale wanaowatendea vibaya, na kuwaunganisha na kuunda maelewano kati ya watu tofauti ndani ya jamii yake kupitia sera yake ya Kiislamu ya nyumbani ambayo ndio kelele cha ubinadamu. Hii ndiyo sababu haishangazi kwamba mwandishi wa Uingereza H. G. Wells aliandika kuhusu Khilafah: “Waliasisi mila kubwa ya uvumilivu wa haki. Wanashajiisha watu kwa roho ya ukarimu na uvumilivu, na ni wenye ubinadamu na vitendo. Waliunda jamii yenye utu ambayo kwayo ilikuwa nadra kuona ukatili na dhulma za kijamii, tofauti na jamii yoyote iliyokuja kabla yake." Baada ya kuelewa haya yote, je kusimamishwa kwa dola hii sio hitajio la dharura la zama zetu?

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Dkt. Nazreen Nawaz

Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumatatu, 14 Juni 2021 18:13

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu