Alhamisi, 09 Rajab 1446 | 2025/01/09
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Habari na Maoni

Kimya Kizito kutoka Kwa Tawala za Waislamu huku Uchina Ikiendeleza Kampeni yake ya Kidhalimu ya Kishirikina Dhidi ya Waislamu

Habari:

Siku ya Jumamosi, 5 Januari, gazeti pekee la Uchina la Kiengereza, Global Times liliripoti kuwa serikali ya Uchina ilipitisha sheria ya kuufanya Uislamu uwiane na ujamaa. Gazeti hilo likasema kuwa maafisa wa serikali, "walikubali kuungoza Uislamu uendane na ujamaa na kutekeleza mikakati ya kuzifanya dini zipitie mchakato wa kuzifanya mujtamaa zisizokuwa za Kichina kuwa chini ya athari ya thaqafa ya Kichina" ndani ya miaka 5 ijayo. Mwanzoni mwa mwezi huu, watawala nchini Uchina katika mkoa wa Yunnan walifunga misikiti 3 iliyobuniwa na Waislamu wanaokandamizwa kutoka kabila dogo la waHui

Maoni:

Matukio haya mapya kutoka kwa utawala wa Uchina ni muendelezo wa kampeni yake ya kidhalimu ili kuuondosha Uislamu kutoka kwa watu Waislamu na kuwalazimisha kufuata imani ya kishirikina kupitia vitisho na uoga. Utawala huo tayari umepiga marufuku katika baadhi ya maeno yake –kufunga saum, kuvaa mavazi ya Kiislamu, kufuga ndevu, na watoto wa chini ya miaka 18 kutoingia msikitini kusikiliza Khutbah. Serikali pia imeharamisha wazazi kutowapa watoto wao wanaowazaa majina fulani ya Kiislamu na kutowapa watoto wao elimu ya Kiislamu au kutoshiriki katika amali za Kiislamu. Hii ni pamoja na kuwashinikiza Waislamu wa Uyghur waoe watu wasiokuwa Waislamu kutoka katika waHan.  Mwaka 2016, katika mpangilio wake wa kupambana na Uislamu utawala huo ulizindua "Kampeni ya Kuwa Familia" –nidhamu ambayo maafisaa waHan kuhamia kwa muda na kuishi na familia za Waislamu ndani ya Xinjiang ili kuchunguza na kuripoti juu ya ishara zozote za wenyeji wao za kujifunga na Uislamu au 'misimamo mikali' –ikijumuisha kukataa pombe, kuswali Jum'a, kufunga Ramadhan, au hata kuweka picha ukutani zikiwa na maandishi ya Kiislamu. Mnamo Disemba 2017, watawala ndani ya Xinjiang waliita jeshi zaidi ya milioni moja kuja kukaa kwa wiki moja na Waislamu wa Uyghur nyumbani mwao kwa lengo hilo. Amal nyingine msingi za Kiislamu zimebandikizwa kuwa misimamo mikali mfano kama kuchagua kula chakula Halali na kutoa salamu za Kiislamu. Viongozi wa Chama cha Kikomunisti ndani ya Urumqi mji mkuu wa mkoa wa Xinjiang walizindua kampeni dhidi ya bidhaa Halali, vitengo vinavyoiongoza vikiapa "kupigana vita vya mwisho" dhidi ya kile walichokiita "mpango wa uhalalishaji." Hakika, chuki ya utawala huu dhidi ya Uislamu imefikia kuwalazimisha Waislamu kuachana na mazishi ya Kiislamu na kukubali shingo upande tamaduni za Kichina za kuchoma maiti zao ambayo serikali ya Uchina inaeneza kwa kasi mkoani Xinjiang.

Pamoja na hayo, zaidi ya Waislamu wa Uyghur milioni moja wametiwa kifungoni daima katika kambi huko Xinjiang kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa (UN), ambapo wanalazimishwa kuachana na imani yao, wanywe pombe na kula nguruwe pamoja kutoa ahadi ya utiifu kwa utawala wa kishirikina wa Chama cha Kikomunisti. Wengi wa walioko korokoroni wanateswa au kuuliwa. Fauka ya hayo, Waislamu wa Uyghur wasiopungua milioni 2 wako ndani ya "kambi za kuwafunza upya" ambapo wanalazimishwa kubeba fikra za kisiasa na kithaqafa zinazopelekea kuachana na Dini yao pamoja na kukashifu imani yao ya Kiislamu na kutamka propaganda za kikomunisti. Kwa mujibu wa AFP, moja katika nakala za serikali zinazohusiana na wale walioko katika "vitengo vya kuelimisha upya" inasema kuwa kujenga raia bora wa Uchina, vitengo hivyo lazima kwanza, "wavunje ukoo wao, wavunje mizizi yao, wavunje ushikamano wao na wavunje asili zao." Dola ya Uchina inaendesha nyumba za mayatima wa watoto wa Uyghur waliochukuliwa kutoka kwa wazazi wao ambao wako kifungoni katika kambi au wamekimbia. Katika nyumba hizi za mayatima watoto wanaelimishwa kwa njia ambayo itaondosha utambulisho wao wa Kiislamu na kuwaweka mbali na Itikadi yao ya Kiislamu. Lengo la Serikali ni kukifanya kizazi kijacho cha watoto wa Waislamu wa Uyghur kuwa watumwa watiifu walioukubali ushirikina. Tamaduni za Wachina waHan na ruwaza ya Beijing ni kuwavunja watu Waislamu wa Uyghur na kuuondosha Uislamu katika maeneo yao.

Licha ya vita hivyo vya wazi dhidi ya Uislamu vikiendeshwa na dola ya Uchina na kampeni yake ya kusafisha jamii dhidi ya watu Waislamu, kumekuwepo na kimya cha aibu kisichoshangaza kutoka kwa tawala na watawala katika ulimwengu wa Waislamu. Licha ya Serikali ya Uchina kutangaza wazi kuwa Uislamu ni "mfumo wa maradhi ya akili" na "kirusi ndani ya ubongo" haikutosha kuamsha cheche za hasira za kweli na kuitikia ndani ya watawala hawa katika serikali ndani ya ardhi za Waislamu ambao kiuwazi hawajali chochote katika matukufu ya Uislamu na maisha ya Waumini. Tawala hizi na watawala katika ardhi za Waislamu ni vifurahisho inapokuja kuwaua Waislamu ndani ya Syria, Yemen, Afghanistan, Pakistan na kwengineko…lakini wanakataa kutumia hata chembe ya kisiasa, kijeshi au kiuchumi kupatiliza kwa ajili ya Uislamu na Waislamu. Serikali ya Pakistan kwa mfano imetuma wanajeshi 15,000 kwenda kulinda eneo la kiuchumi la ushirikiano kati ya Uchina na Pakistan na raia wa Uchina wanaofanya kazi katika miradi ya miundo mbinu katika nchi hiyo; lakini hawajaita hata mwanajeshi mmoja kwenda kulinda hadhi ya Uislamu na Ummah! Hakuna shaka Mpango wa Uchina wa Ukanda na Barabara (BRI) ambao unalenga kuwezesha biashara ya dunia ikijumuisha Asia na Mashariki ya Kati pamoja na Beijing kupitia kujenga njia za biashara ambazo zinapitia Xinjiang…zitaendeleza kununua kimya cha cha tawala hizi zilizouzwa dhidi ya serikali ya Uchina ya msalaba dhidi ya Uislamu. Huku hali halisi ikibakia, ambapo hakuna uongozi wa kikweli wa Kiislamu kusimamia matukufu ya Uislamu na Waumini. Kampeni ya kishirikina ya Uchina dhidi ya Waislamu wa Uyghur itaendelea pasi na kusimama na wataendelea kuwatesa bila wasiwasi pasi na yeyote kuwakabili. Kwa hiyo tunawauliza wale walioko katika majeshi ya Waislamu…nini ambacho kinaendelea kuwafunga kuwa na hawa watawala ambao wameuza roho zao kwa maadui wa Dini yako? Utawezaje kuishi chini ya kivuli na kutumikia uhadaifu wao? Toa nusra yako kwa dharura ili kusimamishwe Khilafah kwa njia ya Utume ambayo itanyanyua cheo chako kuwa na hadhi, shuja wa Dini yao na kuutetea Ummah wako!

 ﴿إِنَّ ٱلَّذِينَ يَشۡتَرُونَ بِعَهۡدِ ٱللَّهِ وَأَيۡمَـٰنِہِمۡ ثَمَنً۬ا قَلِيلاً أُوْلَـٰٓٮِٕكَ لَا خَلَـٰقَ لَهُمۡ فِى ٱلۡأَخِرَةِ وَلَا يُڪَلِّمُهُمُ ٱللَّهُ وَلَا يَنظُرُ إِلَيۡہِمۡ يَوۡمَ ٱلۡقِيَـٰمَةِ وَلَا يُزَڪِّيهِمۡ وَلَهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٌ۬﴾

“Hakika wanao uza ahadi ya Mwenyezi Mungu na viapo vyao thamani ndogo, hao hawatakuwa na sehemu ya kheri yoyote katika Akhera, wala Mwenyezi Mungu hatasema nao wala hatawatazama Siku ya Kiyama, wala hatawatakasa, nao watapata adhabu chungu." [3:77]

Imeandikwwa Kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Dkt. Nazreen Nawaz
Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake Katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 09 Agosti 2020 06:41

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu