Jumapili, 15 Muharram 1446 | 2024/07/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Habari na Maoni

Kizazi cha Watoto wa Uyghur Kinaibwa na Uchina 

Habari

Utawala wa Uchina unaendelea kuwaweka watoto wa Waislamu wa Uyghur ambao wametiwa korokoroni katika kambi au walio kimbia kutokana na kuteswa na dola hiyo, katika nyumba nyingi za mayatima zinazoendeshwa na serikali ndani ya Mashariki ya Turkestan.

Kumeripotiwa watoto 500 wa Uyghur walioko kifungoni katika "shule" iliyofungwa ndani ya mji wa Kashgar pekee ambapo hawaruhusiwi kuwa na mahusiano na ulimwengu wa nje. Katika nyumba za mayatima, watoto hawa Waislamu wanapenyezewa thaqafa ya kikomunisti ili waweze kuikataa imani yao ya Kiislamu na wachukue itikadi ya ujamaa na kuwa watumwa watiifu wa dola hiyo. Tathmini ya ilani za ununuzi katika Mashariki ya Turkestan iliyofanywa na Associated Press ilipata kuwa tangu mwanzo wa mwaka 2017, serikali ya Uchina imetenga bajeti ya zaidi ya dola milioni 30 ili kujenga au kupanua takribani nyumba za mayatima 45 ili ziweze kuwa na vitanda vya kutosha kuweza kuhudumia takribani watoto 5000. Kwa mujibu wa gazeti la The Independent, mnamo Julai na Agosti mwaka jana, utawala huo ulikaribisha fursa za ujenzi wa vitengo ndani ya kaunti kadhaa mkoani humo. Ilani moja iliitisha nyumba moja katika kaunti ya Moyu iwe na ghorofa nne za mabweni ambayo yatakuwa makubwa kuliko viwanja 3 vya mpira.

Maoni

Utenganisho huu wa kinguvu wa watoto wa Uyghur kutoka kwa wazazi wao na familia zao ni sehemu ya msalaba wa Beijing wa kuyakata kikamilifu mafungano ya Waislamu wachanga na Dini yao na kuwabadilisha utambulisho wao- kimsingi na kimitagaa – ili kubuni kizazi chote cha Uyghur ambacho ni cha watumwa watiifu kwa Chama cha Kikomunisti na maadui wa Uislamu. 

Kando na kuwafunga watoto wa Uyghur katika nyumba hizi za mayatima zinazoendeshwa na serikali, utawala wa Uchina pia umejenga maelfu ya shule za chekechea za "lugha tofauti" ili kuweza kupenyeza thaqafa kwa watoto Waislamu. 4,300 ya shule za chekechea zilijengwa au kuboreshwa ndani ya mwaka 2017 kwa mujibu wa serikali. Ndani ya taasisi hizi, watoto wanafunzwa "kuipenda Nchi yao" na kwamba dini za wazazi wao ni jambo la ajabu na lenye misimamo mikali na hivyo basi ina takiwa kuondoshwa. Imeripotiwa kuwa maafisaa mara kwa mara wamekuwa wakizuru hizi shule za chekechea na kuwauliza wanafunzi ikiwa wazazi wao wanasoma aya za Qur'an nyumbani au wanashiriki katika amali za kidini –kiukamilifu wakiwalazimisha watoto kuwachunguza wazazi wao na familia zao. Zaidi ya hayo, utawala umebuni maelfu ya shule za lugha tofauti, nyingi ambazo ni za kulala huko huko ambamo watoto wa Uyghur wanalazimishwa kuhudhuria, muda wao unadhibitiwa wasikae na wazazi wao na kuhamisha udhibiti wa malezi yao kutoka kwa familia zao za Waislamu hadi kwa serikali ya kishirikina, ambayo ina walazimisha kuishi kama wasiokuwa Waislamu wa China waHan. Gazeti la Independt liliripoti kuwa, "Ilani ya serikali iliyochapishwa Februari 2018 ndani ya mji wa Kashgar inasema kuwa watoto katika darasa la nne na kuendelea walio na wazazi walioko korokoroni lazima wapelekwe shule za bweni mara moja – hata kama mzazi mmoja yuko nyumbani. Wanafunzi lazima wamakinishwe na maadili ya kikomunisti, ilani hiyo ilisema na wafunzwe "kuipenda elimu na wawe na mapenzi ya kuifanyia kazi nchi yao" na waepuke "tabia aina 75 zinazoonyesha misimamo mikali." Serikali inasema mfano wa tabia hizo ni kama kulingania "vita vitakatifu" hadi kufuga ndevu na kuacha kuvuta sigara na kunywa pombe kwa sababu za kidini." Uyghur wengi wanahofia kuwa mbinu hizo zinasambaratisha thaqafa na utambulisho wao wa Kiislamu kutoka mtoto mmoja hadi mwengine. Inafanana na "Vizazi Vilivyoibwa" vya watoto wa Aboriginal ambao walitenganishwa na wazazi wao kinguvu na serikali mtawalia za Australia katika miaka ya 1900 na kuwekwa chini ya taasisi zinazoendeshwa na serikali ili kuondosha utambulisho wa uenyeji wao.

Kumekuwa na kelele na maandamano ya watu wa kawaida duniani kote dhidi ya Uchina kutokana na ukandamizaji wa jamii, kuwafunga mamia na upenyezaji wa thaqafa kwa Waislamu wa Uyghur wa Mashariki ya Turkestan…lakini serikali na taasisi gani zimesikia kiukweli vilio vyao na kuchukua hatua ya kusitisha uhalifu huo wa kutisha??!! Tutarajie lolote kutoka kwa mashirika kama Umoja wa Mataifa (UN) zaidi ya kawaida yake ya kutoa kauli za kukashifu ambazo hazifanyi kitu katika kumaliza janga hili? Ni zana inayofanya kazi tu kwa maslahi ya dola kubwa zilizopo katika Baraza la Usalama ambalo Uchina ni mwanachama. Urithi wake umekuwa kufeli jumla katika kuyalinda maisha ya Waislamu –ima ndani ya Syria, Ardhi Tukufu ya Palestina, Kashmir, Myanmar, Afrika ya Kati au kwengineko. Na hatutarajii lolote kutoka kwa serikali za Kimagharibi au tawala zilizoko sasa ndani ya ardhi za Waislamu ambao wanaogopa kupoteza maslahi yao ya kiuchumi na Uchina na ambao wameonyesha kwa kujirudiarudia falsafa yao ya kirasilimali –kupata maslahi ya kifedha daima yatapelekea kuondosha maangamivu na ukandamizaji wa wanadamu.

Kuna msemo maarufu wa Kiengereza unaosema kuwa, "Uwendawazimu ni kufanya jambo hilo kwa hilo na kutarajia majibu tofauti." Hakika, kama Waislamu tunatakiwa kutambua kuwa na matumaini na UN, serikali za kibinafsi za Kimagharibi au tawala tofauti zisizokuwa za Kiislamu ndani ya ulimwengu wa Waislamu katika kuwalinda ndugu zetu wa Mashariki ya Turkestan itapelekea kufeli na kuendelea kwa maangamivu. Kuwakomboa Waislamu wa Uyghur kutoka katika makucha ya utawala wa Kichina unataka dola ambayo haipangi vitendo vyake kwa mtizamo wa maslahi ya kiuchumi bali kwa Sheria na Maamrisho ya Mwenyezi Mungu (swt) pekee, ambayo inajumuisha Agizo la (swt) la kuwalinda Waumini, pasi na kupiga hesabu za kifedha. Inataka dola ambayo kiukweli ina wakilisha na kulinda maslahi ya Uislamu na Waislamu, kuliko mashirika na serikali ambazo zinatoa shinikizo za kisanii katika kumaliza maangamivu ya wanadamu. Serikali hii ni ya Khilafah Rashidah kwa njia ya Utume ambayo Mtume (saw) ameisifu kama ngao na mlinzi wa Ummah na Dini. Tuliona kwa mfano namna chini ya uongozi wa Kiislamu, katika karne ya 8 ya Khilafah ya Ummaya, Al-Walid ibn Abd al-Malik, alipounganisha jeshi lenye nguvu la maelfu chini ya uongozi wa jenerali Muhammad ibn Qasim, kupigana na mfalme wa Hindu –Raja Dahir ndani ya Sindh, India, alipowashika mateka wanawake na watoto Waislamu. Wanajeshi Waislamu walipambana na jeshi kubwa mara kadhaa idadi yao lakini waliwashinda na kuwaokoa Waislamu wanawake na watoto kutoka kwa waliowateka na kuikomboa Sindh yote kutoka katika udikteta wa utawala wa Kihindu. Kitendo hichi hakikupigiwa hesabu za kifedha bali ni kuitikia mwito wa Mwenyezi Mungu (swt) wa kuwanusuru Waislamu kutoka katika udhalimu wazi. Kwa hiyo ikiwa twataka kumaliza madhila ya Ummah wetu ndani ya Mashariki ya Turkestan na ardhi zote duniani, basi lazima tuweke umakinifu na juhudi zetu katika udharura wa kusimamisha Khilafah Rashidah.

Imeandikwwa Kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Dr. Nazreen Nawaz
Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake Katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 09 Agosti 2020 06:37

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu