Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Jeshi la Kiingereza la India na Uungaji Mkono Wake wa Ukoloni wa Kiingereza

(Imetafsiriwa)

Habari:

Maadhimisho ya Vita vya Haifa yaliadhimishwa mnamo 23 Septemba nchini India na 'Israel'. Kila mwaka katika siku hii, maafisa wa India hutoa heshima kwa wanajeshi wao waliopigana na kuishinda Khilafah Uthmani. [1]

Maoni:

Uhusiano kati ya India na Israel hakika umekuwa haki maalum tangu kuundwa kwa umbile hilo haramu mnamo 1948. Mnamo 1950, wakati wa utawala wa Nehru, waziri mkuu wa kwanza wa India, India iliitambua rasmi serikali ya 'Israeli'. Baada ya uhusiano wa siri kwa miongo kadhaa, uhusiano kamili wa kidiplomasia ulianzishwa mnamo 1992 kwa kufunguliwa kwa balozi za 'Israeli'. Ziara ya Modi kwa 'Israeli' mnamo 2017 ilifuatiwa na mikataba mingi ya kimkakati ya uchumi na ulinzi. Wakati wa ziara hii, Modi alitembelea Haifa kutoa heshima kwa wale waliokufa wakipigana katika jeshi la Kiingereza la India.

Vitengo anuwai vya jeshi viliundwa na Kampuni ya East India baada ya kuanza kuitawala India mnamo 1757. Vitengo hivi kutoka sehemu anuwai ambazo ni Bombay, Bengal na Madras, ziliunganishwa kuunda jeshi la India mnamo 1895 chini ya amri ya moja kwa moja ya serikali ya Uingereza. Dori ya jeshi la India ilikuwa kudumisha utawala wa kikoloni nchini India na kukandamiza uasi wowote dhidi ya utawala wa Waingereza nchini India. Jeshi hili la wakala pia lilicheza dori kubwa katika kudumisha sera za wakoloni za Waingereza kote ulimwenguni. Jeshi la India lilikuwa chanzo kikubwa cha nguvu kwa Waingereza. Jeshi hili lilisaidia Uingereza kushinda 'Vita vya Boer' vya kikoloni nchini Afrika Kusini. "Mashujaa" wa vita hivi vichafu ni nadra kuthaminiwa katika vyombo vya habari vya India vyenye kuhofu Uislamu. [2]

Mojawapo ya malengo makuu ya Vita vya Kwanza vya Dunia ilikuwa ni kuivunja na kuing'owa Khilafah Uthmani. Vita vya Haifa vilikuwa moja ya msururu wa vita vya kuichukua Palestina kutoka kwa Wauthmani na kufungua njia ya mradi wa Uingereza ambao ulikuwa ni kupandikiza umbile geni la Kiyahudi katika Mashariki ya Kati. Jeshi la lililo koloniwa la India lilitumiwa katika mradi huu na Waingereza. Waingereza walikuwa dhidi ya Waislamu kuwa na mamlaka ya moja ulimwenguni ambayo India ilikuwa sehemu yake. Waliwachochea Mabaniani dhidi ya utawala wa Waislamu ndani na kiulimwengu. Haishangazi kwamba Mabaniani Washirikina wengi walishirikiana na Waingereza kupigana dhidi ya Waislamu kwani waliwaona Waislamu badala ya Waingereza kuwa wavamizi.

[وَلَتَجِدَنَّهُمْ أَحْرَصَ ٱلنَّاسِ عَلَى حَيَاةٍ وَمِنَ ٱلَّذِينَ أَشْرَكُوا۟ يَوَدُّ أَحَدُهُمْ لَوْ يُعَمَّرُ أَلْفَ سَنَةٍ وَمَا هُوَ بِمُزَحْزِحِهِ مِنَ ٱلْعَذَابِ أَن يُعَمَّرَ وَٱللَّهُ بَصِيرٌ بِمَا يَعْمَلُونَ]

“Na hakika utawaona ni wenye kuwashinda watu wote kwa pupa ya kuishi, na kuliko washirikina. Kila mmoja wao anatamani lau angeli pewa umri wa miaka elfu. Wala hayo ya kuzidishiwa umri hayamuondoshei adhabu; na Mwenyezi Mungu anayaona wanayo yatenda.” [Al-Baqara 2:96]

Mayahudi na Washirikina daima wameshirikiana dhidi ya Uislamu na Waislamu tangu Vita vya Ahzab hadi muungano wa leo wa Washirikina wa Kibaniani na Mayahudi. Wanaendelea kusherehekea udhalilishaji wa Uislamu na Waislamu, lakini maadui wa Mwenyezi Mungu (swt) wanaweza kufurahi kwa muda tu na Mwenyezi Mungu (swt) ameahidi ushindi wa mwisho kwa waumini katika ulimwengu huu na kesho Akhera.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Abdul Fattaah ibn Farooq

Maregeleo:

[1] https://www.firstpost.com/india/battle-of-haifa-when-indian-lancers-charged-heavily-defended-ottoman-and-german-positions-for-a-glorious-victory-9990001.html

[2] https://thewire.in/history/india-britain-boer-war

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu