Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Je, Amerika Inaipa Mgongo Sayansi na Kupoteza Mbio Zake dhidi ya China?

(Imetafsiriwa)

Habari:

Makala mawili wiki hii kutoka kwa Independent kila moja inatoa mwangaza kwa njia tofauti juu ya wapi Amerika inaelekea kisayansi. Mnamo tarehe 11 Oktoba, kichwa kimoja cha habari kilisomeka: "Afisa wa Pentagon aacha kazi kudai usalama wa mitandao wa Amerika ni 'limbukeni' ikilinganishwa na China," na mnamo 13 Oktoba kichwa kingine kilisomeka: "Mgombea wa anayemuunga mkono Trump anapendekeza kuzitoa boti zote nje ya maji ili kupunguza viwango vya bahari.”

Maoni:

Makala ya kwanza yalikuwa juu ya kujiuzulu kwa Nicolas Chaillan ambaye alikuwa ametumikia kwa miaka mitatu kama mkuu wa kwanza wa usalama wa mitandao wa Jeshi la Anga la Amerika. Anaripotiwa kusema kwamba kupigana na China katika vita vya kimtandao "haiwezekani" na kwamba "hatuna nafasi ya kushindana dhidi ya China katika miaka kumi na tano hadi ishirini." Mtazamo wake kwa Amerika ni wa kutamausha: "tayari ni mpango uliomalizika; kwa maoni yangu tayari umekwisha," na maoni yake sio ya pekee ya kutamausha.

Mnamo mwaka wa 2016, makala moja kutoka Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Hong Kong yaliuliza: "China kama Kiongozi wa Teknolojia wa Ulimwengu katika Karne ya 21: Ndoto au Uhalisia?" Tangu wakati huo, watu wameacha kutumia neno 'ndoto' kuhusiana na matarajio ya teknolojia ya China.

Mnamo mwaka wa 2019, shirika la Carnegie Endowment for International Peace lilichapisha mukhtasari wa uratibu wa ushirikiano wa Amerika na Japan kwa anwani: "Kushindana na China juu ya Teknolojia na Ubunifu," ambao ulitaja maendeleo katika “artificial intelligence (AI), big data, fifth-generation telecommunications networking (5G), nanotechnology and biotechnology, robotics, the Internet of Things (IoT), and quantum computing” kama vipengee vya teknolojia ya mapinduzi ya nne ya viwanda, na alionya kuwa" mafanikio katika nyanja hizi yanaweza kubadilisha usawa wa siku zijazo wa nguvu za kiuchumi na za kijeshi.”

Pia mnamo 2019, "Ripoti ya Uchumi wa Dijitali (DER)" ya Kongamano la Umoja wa Mataifa kuhusu Biashara na Maendeleo iliangazia kwamba uongozi wa uchumi wa kidijitali wa kiulimwenguni unatumiwa kwa ushirika na Amerika na China, na kwamba wanauacha nyuma sana ulimwengu uliosalia. "Nchi hizi mbili zina asilimia 75 ya haki miliki zote zinazohusiana na teknolojia za kuzuia, asilimia 50 ya matumizi ya ulimwengu kwenye IoT (Internet of Things), na zaidi ya asilimia 75 ya soko la ulimwengu la mfumo wa kompyuta wa public cloud.  Na, labda la kushangaza zaidi, wanachangia asilimia 90 ya thamani ya soko la mtaji la majukwaa  70 makubwa zaidi ya dijitali duniani. Hisa ya Ulaya ni asilimia 4." Kwa kuwa mbio hizi ni kati ya Amerika na China, inapaswa kuulizwa: ni yupi kati yao yuko mbele?

Mnamo Aprili 2020, ripoti ya Brookings iliyopewa jina, "Tathmini ya kiulimwengu juu kimataifa dori inayokua ya China ulimwenguni" ilibaini maendeleo ya haraka ya kiteknolojia ya China na kuonya kuwa katika muktadha wa mivutano ya Amerika na China, "China imepita, au ina karibia kuiziba, Marekani ” katika teknolojia kadhaa, na makala moja katika Tathmini ya Biashra ya Harvard mnamo Februari mwaka huu iliuliza swali:" Je! China inaibuka kama kiongozi wa ulimwengu katika AI? " na kuyaelezea maendeleo ya China katika miaka ya hivi karibuni kama "ya kushangaza."

Kwa kuzingatia umuhimu mkubwa kama huo wa kimkakati, kujiuzulu kwa, na ukosoaji wa, mkuu wa kwanza wa usalama wa mitandao wa Jeshi la Anga la Amerika pia ni la kushangaza. Ukosoaji wake ni wa kisiasa, unaolengwa katika kiwango cha kujitolea kifedha na umahiri wa kiutawala wa taasisi ya kisiasa wa Amerika mbele ya China kuipiku Marekani katika usalama wa mitandao, ambao ni sehemu ya mapinduzi ya nne ya viwanda. Inaibua maswali muhimu, moja wapo ni: Je! Amerika inaelewa umuhimu wa sayansi kwa msimamo wake wa kimkakati kuhusiana na China?

Wanasiasa wengi wa Amerika, haswa kutoka kwa mrengo mmoja wa chama cha Republican huonyesha athari inayokua dhidi ya kisayansi kutoka kwa wapiga kura wa Amerika waliokata tamaa ambao waliongoza ulimwengu hivi karibuni katika uenezaji na usambazaji wa nadharia za kijinga kuhusu Covid-19 ambazo zilisaidia kuua karibu Waamerika milioni moja (740,000) na haishii hapo. Hakuna mahali popote ambapo watu wengi wanaamini kuwa dunia iko tambarare kuliko Amerika, na upinzani wa kimfumo kwa mabadiliko ya hali ya hewa na hatari zake pia ni kilio cha watu wengi nchini Amerika; kama inavyothibitishwa kutoka kwa makala ya pili ya habari yaliyonukuliwa na Independent wiki hii, ambapo mgombea ubunge wa jimbo la Republican huko Virginia alipendekeza kwenye Twitter kwamba kuongezeka kwa viwango vya bahari kunaweza kusimamishwa kwa urahisi kwa kuzitoa boti zote nje ya bahari. "Nina hamu, je unafikiri kiwango cha bahari kingeshuka, ikiwa tutazitoa boti zote nje ya maji? Mawazo tu, sio taarifa," alisema mgombea wa Republican, Scott Pio. Anaripotiwa kuwahi "kufanya kazi kama mratibu katika Timu ya Kimataifa ya Utoaji Majibu kwa Haraka ya Rais wa zamani Donald Trump, kikosi kilichopewa jukumu la kuhamasisha usaidizi kwa kiongozi wa Republican wakati atakapocheza gofu huko Virginia." Hakuna mtu anayepaswa kushangaa ikiwa ujumbe maarufu wa Trump utamrudisha Ikulu katika kipindi cha miaka mitatu.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Dkt. Abdullah Robin

Orodha ya Vitabu:

https://www.independent.co.uk/news/world/americas/us-politics/nicolas-chaillan-cybersecurity-china-us-b1936238.html
https://www.independent.co.uk/climate-change/news/virginia-scott-pio-sea-levels-b1937355.html
https://iems.ust.hk/publications/thought-leadership-briefs/china-as-the-worlds-technology-leader-in-the-21st-century-dream-or-reality
https://carnegieendowment.org/2019/10/10/competing-with-china-on-technology-and-innovation-pub-80010
https://unctad.org/system/files/official-document/der2019_en.pdf
https://www.brookings.edu/research/global-china-technology/
https://hbr.org/2021/02/is-china-emerging-as-the-global-leader-in-ai

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu