Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Uislamu Haupaswi Kutumiwa Kufanya Kazi ya Serikali

(Imetafsiriwa)

Habari:

Serikali ya Uganda ina sera mpya ya kukabiliana na ufisadi kwa kuwafanya watoto kupeleleza familia zao. Mradi mmoja ambao umekuwa zoezi jipya la kazi ya nyumbani umekuwa kuwafundisha watoto kutambua tofauti kati ya pesa anazomiliki baba yao na bidhaa za anasa. Wanaombwa kuwasilisha uchunguzi wowote usio wa kawaida kwa mwalimu katika hati yenye jina la baba zao. Kazi hii ya nyumbani ilipewa watoto wa umri wa miaka 10 katika darasa la 5.

Maoni:

Wazo la kwamba watoto watumike kupeleleza familia zao wenyewe chenye ni kitendo cha ufisadi!

Akili zisizo na hatia za mtoto zinapotoshwa katika hali ya uaminifu mdogo kwa wale wanaopaswa kuwaangalia. Utukufu wa nyumba ya familia unahujumiwa na sera hizi kwani katika Uislamu tunafundishwa kuwaheshimu wazee, haswa baba kama kiongozi wa nyumba. Suala la kuwaamini Waislamu wote na kutokuwa na shaka ndio maadili ya kweli ya juu ya Kiislamu ambayo yalisimamia mienendo ya kijamii iliyostaarabika ndani ya Khilafah.

Mahusiano haya ya kizembe hayatawafundisha watoto mwenendo mzuri wa maadili kwani chanzo halisi cha tatizo hakijashughulikiwa. Ufisadi mkubwa zaidi haupo hata katika nyumba za raia wa kawaida, upo katika ngazi za juu za afisi na ndio sifa ya uongozi wa kidikteta wa utawala wa Uganda unaodhibitiwa na wakoloni. Orodha ya Kimataifa ya Ufisadi kama inavyoangaziwa katika jukwaa la data la mtandaoni la Trading Economics huorodhesha nchi kwa namna ifuatayo;

“Orodha ya Mitazamo ya Ufisadi huziorodhesha nchi na maeneo kwa msingi wa jinsi sekta zao za umma zinavyochukuliwa kuwa fisadi. Alama ya nchi au eneo huashiria kiwango kinachochukuliwa kuwa ufisadi katika sekta ya umma kwa mizani ya 0 (fisadi zaidi) hadi 100 (safi bila ya ufisadi). ”

Kwa sasa katika orodha ya 2020/2021 Uganda ilipoteza Alama 27 mwaka wa 2020 kutoka Alama 28 mwaka wa 2019. (chanzo: Transparency International)

Katika Khilafah kuna ushirikiano wa aina moja kati ya mfumo wa elimu ili kuwafunza raia maadili mema ya kutumikia maslahi ya Mwenyezi Mungu (swt) ili wafaulu Duniani na Akhera. Hawafundishwi kuwa jeshi la polisi mbadala. Mfumo wa Mahakama una adhabu kali za wazi kwa kila aina ya ulaghai, ufisadi na wizi kiasi kwamba wananchi huhisi ni jambo lisilowezekana kabisa kujihusisha na tabia hii kwa njia ya kimpangilio, kwani inahitaji operesheni na ridhaa ya wengi. Pia, mfumo wa Uchumi utawapa watu mahitaji yao hivyo umaskini hautawasukuma watu kukata tamaa.

[إِنَّمَا جَزَاءُ الَّذِينَ يُحَارِبُونَ اللَّهَ وَرَسُولَهُ وَيَسْعَوْنَ فِي الْأَرْضِ فَسَادًا أَنْ يُقَتَّلُوا]

“Basi malipo ya wale wanao mpiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wakawania kufanya uchafuzi katika nchi, ni kuuwawa, au kusalibiwa, au kukatwa mikono yao na miguu yao kwa mabadilisho, au kutolewa nchi. Hii ndiyo hizaya yao katika dunia; na katika Akhera watapata adhabu kubwa.” [Al-Maida 5:33]

Wakati Khilafah tukufu itakaporegea kutawala Afrika na dunia watoto watakuwa na haki yao wanayostahiki kama watoto na ufisadi hakika utakuwa ni historia.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Imrana Mohammad
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu