Jumamosi, 18 Shawwal 1445 | 2024/04/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Uongozi wa Taliban ulianzia Oslo ambako Wasaliti wa Shirika la Ukombozi wa Palestina (PLO) Walianzia.
Uongozi wa Taliban Utaishia kwa kile ambacho PLO Ilimalizia Nacho, Usaliti Mkubwa dhidi ya Uislamu na Waislamu.

(Imetafsiriwa)

Habari:

Wanadiplomasia wa Taliban na wa nchi za Magharibi wanafanya mkutano nje ya mji mkuu wa Norway Oslo kwa ajili ya mazungumzo yanayoangazia mgogoro wa kibinadamu wa Afghanistan, ambao umeongezeka kwa kasi tangu Agosti mwaka jana wakati Taliban iliporegea mamlakani miaka 20 baada ya kupinduliwa katika uvamizi ulioongozwa na Marekani. Majadiliano hayo ya faragha na wawakilishi wa Marekani, Ufaransa, Uingereza, Ujerumani, Italia, Muungano wa Ulaya na Norway yalifanyika mnamo tarehe 24 Januari katika Hoteli ya Soria Moria, juu ya kilima chenye theluji nje ya Oslo.

Maoni:

Viongozi wa Taliban walikataa pendekezo la Hizb ut Tahrir la wao kusimamisha dola ambayo itatawala kwa Kitabu na Sunnah. Kisha viongozi wa harakati hiyo wakakataa kuunganisha leo lao na lengo la Ummah mzima wa Kiislamu. Kwa hiyo, watu wa Afghanistan walidogoshwa, ndani ya miezi michache, hadi kuwa watu wenye njaa, ambao hawakuweza kujipatia riziki, na watafutaji hifadhi, wakipanga foleni mipakani na katika viwanja vya ndege wakitoroka nchi hiyo. Watu walishushwa chini na nguvu za kibinadamu ambazo zilitakiwa kutumika kujenga nchi zikaisha. Baada ya haya yote na maafa mengine, viongozi wa harakati ya Taliban wanaelekeza nyuso zao upande wa Magharibi ambayo inaunyemelea Uislamu na kuwanyanyasa Waislamu. Wanazigeukia nchi za Magharibi ambazo daima zimekuwa zikiwahadaa watu wa Afghanistan na kuunda miungano ya kijeshi ambayo ilizivunja ngome za Afghanistan, na kuwauwa mashahidi watu wake, kuwafanya wajane wanawake wake na kuwafanya mayatima watoto wake. Je, haya yote hawakuyaona viongozi hawa, yamefutika kwenye kumbukumbu zao? Je, viongozi wa namna hii wanastahili uongozi?!

Wakati viongozi wa Shirika la Ukombozi wa Palestina, lililoongozwa na msaliti mkubwa zaidi Yasser Arafat, lilipokwenda Oslo mnamo 1993, sura za mwisho zilianza kwa ajili ya kufutwa kwa kadhia ya Palestina, ambayo ilisababisha kuundwa kwa "Mamlaka" ya Palestina ambayo inafanya kazi kama mlinzi wa umbile vamizi la Kiyahudi. Majadiliano yatakayofanyika na Taliban yanaelekea upande mmoja. Thomas West, mjumbe maalum wa Marekani kwa Afghanistan, yuko katika mji mkuu wa Norway kwa mazungumzo na ujumbe wa Taliban. Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilisema wajumbe wa nchi za Magharibi watajadili "kuundwa kwa mfumo wakilishi wa kisiasa, kukabiliana na majanga ya dharura ya kibinadamu na kiuchumi, masuala ya usalama na kupambana na ugaidi, na haki za binadamu, haswa elimu kwa wasichana na wanawake."

Kitakachokubaliwa baina ya pande hizo mbili, huku viongozi wa Taliban wakitobaki nyuma katika utekelezaji wake, ni kuunda mfumo wa kisiasa wa kiutendaji na wa kiraia kwa muundo wa Magharibi, ambao hautawali kwa Uislamu, badala yake unazuia kurudi kwa Uislamu na unafuatilia watetezi wa kuregeshwa kwa Khilafah, ambayo Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani inaiita "hofu ya usalama na kukabiliana na ugaidi." Kinachotakiwa pia ni uingizaji Umagharibi kwa jamii ya Afghanistan na kutiwa kwake usekula, kama Muhammad bin Salman anavyofanya katika ardhi ya Haramayn, jambo ambalo Magharibi hujificha nyuma ya pazia ya "elimu kwa wasichana na wanawake."

Huku nchi za Magharibi zikihakikisha kwamba viongozi wa harakati ya Taliban wanatekeleza njama hizi dhidi ya watu wa Afghanistan, huku viongozi hawa wakiuza kile walichoamrishwa kufanya, nchi za Magharibi hazijachukua hatua yoyote ya kivitendo, hata kwa njia ya kuonyesha "nia njema." Hakuna nchi ambayo tayari imeitambua serikali ya Taliban na hata kuwakaribisha nchini Norway sio utambuzi wa kimyakimya kwao. Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway, Anniken Huitfeldt, alisisitiza kwamba mazungumzo hayo "sio uhalali au utambuzi wa Taliban."

"Misaada ya kimataifa" kwa serikali kibaraka ya Ghani, ambayo ilifadhili takriban asilimia 80 ya bajeti ya Afghanistan, ilisitishwa ghafla, huku Marekani ikizuia $9.5 bilioni ya mali ya Afghanistan katika benki za Marekani, na kusababisha kuzorota kwa kiasi kikubwa kwa hali nchini Afghanistan. Umoja wa Mataifa umeonya kuwa asilimia 95 ya watu wa Afghanistan watakabiliwa na njaa. Viwango vya ukosefu wa ajira vimeongezeka sana na mishahara ya wafanyikazi wa serikali haijalipwa kwa miezi kadhaa katika ardhi zilizoharibiwa na mawimbi mengi ya ukame. Kutokana na data hii, mtazamaji anaweza kuhitimisha kuwa harakati ya Taliban kwenda Oslo haikuwa kwa mazungumzo bali kwa maagizo. Hakuna mazungumzo kwani harakati hiyo halina lolote la kujadili, kama ilivyotokea kwa viongozi wa Shirika la Ukombozi wa Palestina, wao pia walipoweka silaha chini na kuuza damu ya mashahidi huko Oslo, na kuhakikisha kufutwa kwa kadhia ya Palestina. Ukweli ni kwamba Taliban watakuwa kama PLO. Viongozi wa Taliban walikwenda Oslo baada ya kutoa ahadi mbalimbali za kujisalimisha kikamilifu kwa vita vya makruseda na jumuiya ya kimataifa yenye chuki. Kisha watarudi Afghanistan kutekeleza usaliti walioagizwa.

Iwapo watu wenye ikhlasi wa Afghanistan na harakati ya Taliban hawatarekebisha mambo yao, basi kafara kubwa walizozitoa zitaishia katika yale ambayo mihanga ya watu wa Palestina iliishia, kuwa ni dhihaka ya mamlaka chini ya nguzo za maadui. Nchi dhaifu, tete na duni ya kiraia, inayotegemea ridhaa ya muungano wa makruseda. Kwa hili wamepoteza dunia hii na akhera, hivyo waaminifu katika harakati hii na watu wa Afghanistan wanapaswa kusafisha safu zao kutokana na viongozi wanaonyoosha mikono yao kwa Magharibi. Ni lazima waregee kukubali pendekezo la Hizb ut Tahrir na kuipa Nussrah ya kusimamisha Khilafah inayomtegemea Mwenyezi Mungu (swt) pekee na juhudi za Umma wa Kiislamu.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Bilal Al-Muhajir – Wilayah Pakistan

#Afganistan                         #Afghanistan                       أفغانستان#

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu