Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vita vya Urusi na Ukraine ni Fursa ya Kurudi tena kwa Mlinzi na Ngao ya Kweli ya Kiulimwengu, Khilafah

Habari:

Mnamo Alhamisi, 24 Februari 2022 Urusi iliivamia rasmi Ukraine na hivi sasa wamo katika vita vikali. Vita hivi ni kupamba moto kwa mzozo baina ya Urusi na Ukraine ulioanza tokea mwaka 2014 kutokana na kubadilishwa kwa uongozi wa Kiev. Hapo awali uongozi ulikuwa unaegemea Urusi na baadaye ulipinduliwa na sehemu yake kuchukuliwa na uongozi unaoegemea Magharibi (Amerika na NATO).

Maoni:

Mzozo huu mpya unafichua kwa mara nyingine uhadaifu wa ile inayoitwa dola kuu duniani, Amerika katika mahusiano yake na mataifa mengine. Amerika chini ya utawala wa Obama ilizitumia asasi za kijeshi za mauaji za Urusi katika kusambaratisha mapinduzi ya kweli nchini Syria. Utawala wa Trump ukayatishia mataifa ya Ulaya (NATO) ili kuongeza maradufu michango yao ya kifedha kwa ajili ya kulindwa dhidi ya vitisho vya Urusi. Na mtawalia, utawala wa Biden umeanzisha vita huko Ulaya kwa kuichochea na kuisukuma Urusi kuivamia Ukraine kijeshi na hatimaye kutishia usalama wa Ulaya yote. Kwa kuongezea, imetangaza vikwazo kwa Urusi.

Urusi ina maradhi ya ukubwa kutokana na historia yake ya zamani kama mshikadau mkuu wakati ilipokuwa ndio kiongozi wa Muungano wa Jamhuri za Kijamaa za Kisoviet (USSR) kabla kuanguka kwake mnamo 1991 kupitia mikono hiyo hiyo ya Amerika kupitia vita vya uwakala. Hivyo basi, inaghurika na mbinu za Amerika na kujipata kuwa inatekeleza makosa ya kisiasa ambayo huisababishia madhara makubwa. Urusi na Ukraine zote zinatumika kama vikaragosi vya kisiasa na utawala wa Kiamerika ili kuweza kuitathmini upya sera yake ya kigeni katika kujitayarisha kupambana na kuchipuza kwa ushindani wa Uchina dhidi ya uchumi wa Amerika na mshikadau yeyote anayemuunga mkono Uchina.

Ni wazi kwa kuzingatia yaliyoko hapo juu kwamba Amerika inatanua katika mbinu hadaifu za kisiasa. Fauka ya hayo, mataifa yote ya kirasilimali ya kisekula yameasisiwa juu ya msingi sawa wa kupima vitendo kwa kuzingatia manufaa na maslahi. Kwa hiyo, haishangazi kushuhudia Urusi ikiivamia Ukraine, Amerika ikiivamia Iraq n.k kwa kutumia visingizio vyovyote ambavyo vitawapelekea kufikia lengo kwa kuwa lengo huhalalisha njia. Bila shaka mikono ya utawala wa Amerika inatona damu za Waukraine, kwa sababu wao ndio mabwana katika kupanga njama katika mzozo wote huo! Hivyo basi, wao ni washirika katika uhalifu pamoja na utawala wa Urusi.

Ama kuhusiana na vilio vya kiulimwengu ni thibitisho jingine kwamba kiuhakika mfumo wa kirasilimali wa kisekula umefeli kupindukia katika kuwasimamia wanadamu. Ndio tunashuhudia majanga yasiyohesabika kama natija ya uchochezi wa vita usioingia akilini kutoka kwa inayodaiwa kuwa ni mlinzi wa amani duniani. Mizozo ya kuendelea inatokomeza Somalia, Kashmir, Syria, Libya, Xinjiang, Uzbekistan, Afghanistan n.k. Hili limepelekea mwito wa kutaka mlinzi na ngao ya kweli mbadala dhidi ya vita fisidifu ambavyo SIO kwa ajili ya kumridhisha Mwenyezi Mungu (swt). Sasa ni fura ya kusimamisha tena Khilafah kwa njia ya Utume. Fursa adhimu ya kuwakomboa wanadamu kutoka katika minyororo ya Ukafiri hadi kwenye nuru ya Uislamu.

Khilafah haitokuwa tu mdhamini wa kweli wa amani, bali pia itajituma kurudisha mpangilio na ustawi ambao hivi sasa unakosekana chini ya zama hii ya mfumo wa kirasilimali wa kisekula. Zama ambayo pengo la ukosefu wa haki unaendelea kukua kwa kasi inayoshtusha. Ambapo sera za walio nacho na wasiokuwa nacho imemakinishwa kwa kina na inaendelea kupatilizwa na kipote cha wachache walioko katika kilele cha uongozi kama inavyoshuhudiwa leo nchini Kenya na ulimwenguni kwa ujumla. Kutaabika kwa watu ni fursa ya kibiashara kwa tai wa kiuchumi wanaoghilibu kuwa ni wajasiriamali kama ilivyofichuliwa na Covid-19, janga la kimakusudi lililopangwa!

Muda wa Khilafah uko nasi baada ya miaka 101 (Hijria) ya kutokuwepo. Hii ni fursa ya dhahabu kwa yeyote anayefanya kazi kwa bidi ya kurudi kwake, akiwa na matumaini na kuomba kheri, amani, usalama na ustawi duniani. Kurudi kwake ndio mwokozi pekee kutoka katika michafuko hii ya kujirudia. Wakati wa kuitikia mwito wa Mwenyezi Mungu (swt) ni sasa: يَـٰٓأَيُّہَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱسۡتَجِيبُواْ لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمۡ لِمَا يُحۡيِيڪُمۡ‌ۖ “Enyio mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Al-Anfal 8: 24].                                                               

#أقيموا_الخلافة           #الخلافة_101      #TurudisheniKhilafah        #YenidenHilafet

Imeandikwa kwa ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Ali Nassoro Ali

Mwanachama wa Ofisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu