Jumatatu, 23 Muharram 1446 | 2024/07/29
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Huku Imran Khan Akiwa Ameivunja Migongo Yetu, Upinzani Hautaleta Mabadiliko Vilevile. Iondoeni Demokrasia na Msimamishe Khilafah

(Imetafsiriwa)

Habari:

Kabla ya hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu Imran Khan, MNAs kadhaa wa PTI mnamo Alhamisi, 17 Machi 2022, walipatikana wakiishi katika Jumba la Sindh, lililoko katika eneo jekundu la mji mkuu wa jimbo hilo. Wabunge hao wapinzani waliapa kupiga kura ‘kulingana na dhamiri zao.’ wakimaanisha kwamba watapiga kura dhidi ya chama chao cha PTI.

Maoni:

Mnamo tarehe 7 Machi 2022, vyama vya upinzani viliwasilisha pendekezo la kutokuwa na imani katika Bunge la Kitaifa likimshtumu Imran Khan kwa kuharibu uchumi, na kusukuma mamilioni zaidi chini ya mstari wa umaskini. Kitendo hiki cha vyama vya upinzani hakikuwa cha kushangaza. Tangu mzozo kuhusu uteuzi wa jeshi ulipoibuka mnamo Oktoba 2021, imeonekana kuwa taasisi ya kijeshi inajitenga na PTI. Vyama vya upinzani sasa vinaeleza kwa sauti kubwa kwamba taasisi ya kijeshi sasa haiegemei upande wowote, hivyo hoja yao ya kutokuwa na imani itafanikiwa.

Akihisi kutelekezwa, Imran Khan ametoa simulizi kwamba dola za kigeni zinataka aondolewe madarakani kwa sababu alisema "hapana kabisa" kwa kambi za Marekani. Kiuhalisia Marekani haikuwahi kuuliza na sasa imempa kazi Imran Khan kulinda amani. Kwa kutapatapa, Imran Khan ameamua kuandaa mikusanyiko ya watu kote nchini huku joto la kisiasa linalomkabili likizidi kumpanda.

Hata hivyo, suala muhimu ni wapi watu wa Pakistan wanapaswa kusimama. Mbali na wafuasi sugu wa vyama vya kisiasa vya sasa, umati jumla wa watu unakataa kambi zote mbili. Wananchi wameshauona utawala wa chama cha Pakistan People’s Party (PPP) na chama cha Pakistan Muslims League (PML-N). Sasa wanauona uamuzi wa chama cha Pakistan Tehreeki-i-Insaf (PTI). Uongozi wote wa sasa wa kisiasa umefeli vibaya. Chini ya demokrasia, hakuna chama kitakacholeta mabadiliko yoyote au kutoa unafuu. Hakuna chama cha kisiasa chini ya mfumo huu wa kidemokrasia, wa kirasilimali kinachoweza kutoa isipokuwa makombo machache ya mkate uliooza na hivyo ushindani wao wa kisiasa hauna maslahi kwa umma.

Mabadiliko ya kweli hayawezi kamwe kuwa chini ya demokrasia kwa sababu yanatabikisha mfumo wa kirasilimali ulioundwa ili kulinda maslahi ya dola za kigeni na makundi tawala ya ndani pekee. Mabadiliko ya kweli yatakuja pale tu mfumo huu utakapoondolewa na Khilafah kwa Njia ya Utume kusimamishwa mahali pake. Khilafah pekee ndiyo inayotabikisha maamrisho ya Mwenyezi Mungu (swt) katika kila nyanja ya maisha, iwe uchumi, utawala, mahakama, elimu, maadili ya kifamilia au  sera ya kigeni. Utabikishaji wa maamrisho ya Mwenyezi Mungu (swt) unahakikisha kwamba hatutanyonywa na zana za wakoloni, IMF, Benki ya Dunia, FATF na US CENTCOM. Khilafah ndiyo itakayong’oa mfumo dhalimu wa sasa wa kiulimwengu, ambao umeyazamisha mataifa madogo na masikini chini ya mateso, ili kudumisha himaya ya dola za kikoloni ya kiulimwengu.

Mabadiliko ya kweli yanaweza kutokea na yatatokea kama alivyotuahidi Mwenyezi Mungu (swt), lakini ikiwa tu tutabakia kuwa watiifu Kwake (swt), tukiwa hatumuogopi yeyote isipokuwa Yeye (swt) na kujitahidi mchana na usiku kutafuta Nusra Yake. Mwenyezi Mungu (swt) amesema:

 (وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُم فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَى لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُم مِّن بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْنًا يَعْبُدُونَنِي لَا يُشْرِكُونَ بِي شَيْئًا وَمَن كَفَرَ بَعْدَ ذَلِكَ فَأُوْلَئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ)

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu.” [Surah An-Nur 24:55].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Mhandisi Shahzad Shaikh
Naibu Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu