Jumamosi, 21 Shawwal 1443 | 2022/05/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Unafiki wa Ufaransa Umejengwa Juu ya Mfumo wao Kinzani

(Imetafsiriwa)

Habari:

(Reuters) - Balozi wa Urusi nchini Ufaransa mnamo Ijumaa aliitwa na Wizara ya Mambo ya nje ya Ufaransa juu ya chapisho la awali la Twitter la ubalozi huo ambalo Paris ililiona kuwa halikubaliki, wizara ya mambo ya nje ilisema.

Ubalozi wa Urusi jijini Paris mnamo siku ya Alhamisi ulikuwa umeweka picha inayoonyesha mwili ukiwa umelala juu ya meza iitwayo "Ulaya" huku wahusika wakiwakilisha Marekani na Umoja wa Ulaya wakiudunga sindano.

"Tumeliweka wazi hilo leo kwa Balozi wa Urusi," wizara ilisema katika taarifa iliyotumwa kwa Reuters. "Tunajaribu kudumisha njia inahitajika ya mazungumzo na Urusi na vitendo hivi havifai kabisa." Akizungumza na waandishi wa habari mjini Brussels, Rais Emmanuel Macron alipuuzilia mbali vibonzo hivyo na kusema ni propaganda za uongo.

"Haikubaliki. Tunaamini mazungumzo ya heshima na tutayaendeleza na hiyo inamaanisha heshima kwa pande zote. Ni makosa. Yamesahihishwa na ninatumai haitatokea tena. Tunataka iwe hivyo."

Mchoro huo ulimaanisha kuwa bara la Ulaya lilikuwa linaharibiwa na sera zinazofanywa na Marekani na Muungano wa Ulaya.

Sindano hizo, zilizoonekana zikidungwa kwenye mwili unaoonyesha Ulaya, zilikuwa na maneno kama vile "NATO", "COVID-19", "Futilia mbali Utamaduni" na "Vikwazo".

Ubalozi wa Urusi jijini Paris ulikuwa uliweka uchapishaji wake wa katuni hiyo kwa wakati sanjari na mkutano mkuu wa NATO wa mara tatu wa Alhamisi jijini Brussels, G7 na Muungano wa Ulaya kujadili jinsi ya kukabiliana na vita vya Urusi nchini Ukraine.

Maoni:

Vita vya Ukraine vimefichua unafiki mwingi katika jinsi mataifa ya Magharibi na vyombo vya habari vinavyoutazama ulimwengu. Wito wa mabadiliko ya utawala unachukuliwa kuwa mzuri ikiwa ni Amerika ndiyo inayouunga mkono, lakini mbaya ikiwa ni mtu mwingine yeyote. Wakimbizi ni jambo lisilokubalika ikiwa ni Wazungu weupe, lakini "ni jambo la kawaida" ikiwa ni wengine. Unafiki wa hivi punde ni upinzani wa Ufaransa dhidi ya katuni ya ubalozi wa Urusi. Ni wazi hakuna usherehekeaji wowote uhuru wa kuzungumza, kama walivyofanya wakati gazeti la Charlie Hebdo lilipochapisha katuni za kumtukana Mtume Muhammad (saw). Kauli za kuudhi dhidi ya Uislamu na Waislamu zilikubalika na zingali zinakubalika kwa wengi katika nchi za Magharibi, lakini kutilia shaka vitendo vya pande zote kwenye mzozo wa Ukraine haikubaliki.

Unafiki wa viongozi wa Kimagharibi na vyombo vyao vya habari haupaswi kuangaliwa tu kama dhidi ya upendeleo wa Waislamu, kwani ni zaidi kuliko hivyo. Chuki yao ya wazi kwa utawala wa kiimla si ya kweli, kwani wameendelea kuunda na kuunga mkono serikali za kiimla kote duniani. Wanasukumwa katika matendo yao yote na mfumo wao wa kisekula wa kirasilimali usiotambua kipimo chochote cha sawa na makosa, haki na batili, zaidi ya maslahi yao wenye ya kibinafsi, hivyo daima watapinda na kugeuka kinafiki pindi kunapokuwa na manufaa yanayopatikana. Unafiki si tu katika matendo yao, bali maadili na mifumo yenyewe iliyojengwa juu ya imani yao kinzani ya kinafiki ya kisekula.

 (مَثَلُ الَّذِينَ اتَّخَذُوا مِن دُونِ اللَّهِ أَوْلِيَاءَ كَمَثَلِ الْعَنكَبُوتِ اتَّخَذَتْ بَيْتًا وَإِنَّ أَوْهَنَ الْبُيُوتِ لَبَيْتُ الْعَنكَبُوتِ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُون)

“Mfano wa walio wafanya walinzi badala ya Mwenyezi Mungu, ni mfano wa buibui alivyo jitandia nyumba. Na hakika nyumba dhaifu mno kuliko zote ni jumba la buibui, laiti kuwa wanajua.” [Al-Ankabut: 41]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Yahya Nisbet
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Uingereza

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu