Jumapili, 22 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Usawa wa Kijinsia Unapelekea katika Maangamivu ya Jinsia

(Imetafsiriwa)

Habari:

Kichwa cha habari katika Gazeti la ‘The Mirror’ mnamo tarehe 11 Juni: “Shule YAPIGA MARUFUKU wanafunzi wote kutovaa sketi chini sheria kali mpya ya ‘kutoegemea jinsia yoyote’” yaonyesha mwelekeo ambao ghiliba ya kijinsia ya Kimagharibi inachukua. Mwalimu Mkuu, Sammy Crook, alieleza sera mpya ya shule katika barua kwa wazazi: "Tutazifuata shule nyingine za sekondari katika kutekeleza zaidi sera ya sare isiyoegemea jinsia yoyote. Wazazi/walezi watafurahi kujua kwamba wengi wa sare hizo zitabakia kama ilivyo, isipokuwa kuanzia Septemba wanafunzi wote watatarajiwa kuvaa suruali."

Maoni:

Mwenyezi Mungu, Mjuzi zaidi na Mwenye habari, ametuusia tuzingatie uumbaji Wake wa wanadamu kutokana na wanaume na wanawake, lakini akili potovu hufikiri kwamba wanaweza kufanya vizuri zaidi kwa kuunda upya jinsia ya binadamu namna watakavyo wao.

 (يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّا خَلَقْنَاكُم مِّن ذَكَرٍ وَأُنثَى وَجَعَلْنَاكُمْ شُعُوبًا وَقَبَائِلَ لِتَعَارَفُوا إِنَّ أَكْرَمَكُمْ عِندَ اللَّهِ أَتْقَاكُمْ إِنَّ اللَّهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ)

“Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamngu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye khabari.” [49:13]

Jinsia ya kibaolojia daima imekuwa kikwazo kwa utabikishaji kamili wa usekula, kwa sababu jinsia, ambayo kimaumbile ni ya pande mbili, husababisha tofauti halisi kati ya jinsia ambazo daima zimesimama kama kikwazo kwa usawa kamilifu. Baada ya kutabanni usekula, Magharibi ilijiingiza katika mapambano ya ndani ya uhuru na usawa, na moja ya mapambano haya ilikuwa mapambano ya usawa wa jinsia. Taratibu, wanawake wa nchi za Magharibi walipata haki ambazo Uislamu ulikuwa umewapa wanawake kwa muda mrefu, lakini ambazo hazikutambuliwa hapo awali katika nchi za Magharibi. Hivyo, wanawake wa Magharibi walipata haki ya kupiga kura na kumiliki mali na kusoma masomo yale yale ambayo wanaume wanaweza kusoma katika vyuo vikuu. Hata hivyo, tofauti za kimwili na kihisia kati ya wanaume na wanawake bado ziliwazuia wanawake kufikia mambo sawa na wanaume.

Maudhui ya jinsia inaendelea kubadilika kwani juhudi zote za kufikia usawa kamili kati ya wanaume na wanawake zimeshindwa. Sheria ya kuwalazimisha waajiri kutoa posho ya likizo ya uzazi imesaidia wanawake kuweka usawa wa uzazi na kazi zao, lakini bado wanawake kwa wastani wanalipwa mishahara midogo kuliko wanaume kutokana na matokeo yasiyoweza kuepukika ya kuwa mbali na maeneo ya kazi, si tu kwa ajili ya kujifungua bali kwa kulea watoto. Kuwashajiisha wanawake kufanya kazi zinazofanywa kwa kawaida na wanaume na kuweka viwango vya ni wanawake wangapi wanapaswa kuajiriwa katika kazi hizi kumeongeza ajira ya wanawake nje ya dori zao zalizofungwa za awali. Hata hivyo, msukumo wa uhuru kamili na usawa haujakomea hapo.

Usawa wa kijinsia umebadilika na kuwa kutoegemea upande wowote wa kijinsia ambapo wadanganyifu wa kijamii wa Magharibi wanatafuta kuifuta jinsia. Wavulana wanashajiishwa kucheza katika kuwa kina mama wakiwa na wanasesere, na wasichana wanashajiiswa kucheza kama kina baba. Huku shule ambayo kwa sasa imewafanya wavulana na wasichana kuvaa nguo zinazofanana kwa jina la 'kutoegemea upande wowote wa jinsia' imechochewa na matatizo ya kupata wasichana kushikamana na urefu wa sketi uliotabanniwa, sio bahati mbaya kwamba shule hiyo ilitafuta uungwaji mkono kwa sera yake mpya kwa kucheza karata yenye nguvu zaidi ya kutoegemea upande wowote wa kijinsia.

Wavulana na wasichana wanazidi kuchanganyikiwa kuhusu wao ni nani huku harakati hii potovu ikishika kasi.

Kituo cha Utafiti cha Pew kiliripoti matokeo ya uchunguzi mnamo tarehe 7 Juni 2022 yakionyesha kwamba "asilimia 5 ya vijana watu wazima nchini Marekani wanasema jinsia yao ni tofauti na jinsia yao waliyopewa wakati wa kuzaliwa" ikilinganishwa na "0.3% tu ya wale walio na umri wa miaka 50 na zaidi ambao wamebadilisha jinsia au wasio na pande mbili." Mnamo tarehe 24 Juni Sheria ya Kutambua Jinsia ya New York, itaanza kutumika kuruhusu watu nakili jinsia zao kama "X" kwenye leseni ya udereva, badala ya mwanamume au mwanamke.

Gavana Hochul alitangaza kwa fahari kwamba “Kila mtu, bila kujali kitambulisho chake au muonekano wa kijinsia, anastahili kuwa na hati ya utambulisho ambayo inaakisi yeye ni nani... Utawala wangu unasalia kujitolea kuhakikisha kuwa New York ni mahali pa thamani, upendo na nyumbani kwa wanachama wa jumuiya ya LGBTQ+." Taasisi nyingi zimeanzisha vyoo vya ‘jinsia isiyoegemea upande wowote’ na hata lugha inabadilishwa iwe na ‘ubaguzi’ mchache wa kijinsia.

Sio kila mtu anafurahia sana juu ya hili. Wafanyakazi wengi wameachishwa kazi au wameaibishwa kwa kutotumia viwakilishi vipya kuelezea wingi wa michanganyiko mipya ya kijinsia ambayo akili potovu zimefikiria. Wanariadha wengi wa kike wameshindwa kushindana na wanariadha wa kiume wenye misuli zaidi ambao wamechagua kujitambulisha kuwa ni wanawake au ambao wamejitambulisha kuwa wabadilishi wa jinsia na kudai kutendewa ‘usawa’ na wanawake wa kibaolojia. Kuchanganyikiwa, upotovu na hata maradhi ndio matokeo, na furaha ya mwanadamu haijaongezwa na mikengeuko kama hii kutokana na maumbile ambayo Mwenyezi Mungu ametuumba nayo.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Dkt. Abdullah Robin

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu