Jumamosi, 21 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vyombo vya Habari vya Kimagharibi Vyanyonya Nguvu za Watu kupitia Kula Hofu na Matarajio Yao

 (Imetafsiriwa)

Habari:

Kichwa cha habari cha kushtua katika gazeti la Independent mnamo tarehe 15 Julai kinasomeka: "Aina mpya ya Uviko ya 'Stealthy' inaweza kukuambukiza tena na tena kila mwezi." Imewakanganya watu wengi nchini Uingereza, lakini je ni kweli?

Maoni:

Ingawa aina tofauti tofauti za Uviko zinawasilisha hatari nyingi, kile ambacho kichwa hiki cha habari cha Independent kinachodai hakikuungwa mkono na sayansi ingawa makala hayo yananukuu kutoka kwa utafiti bora wa wanasayansi mashuhuri kama vile Profesa Danny Altmann.

Kinachoeleweka vyema na wanabiolojia ni kwamba virusi vinavyosababisha Uviko-19 hubadilika kila mara ili kuepuka kutambuliwa na kingamwili ambazo mifumo yetu ya kinga imetengeneza ili kutulinda dhidi ya maambukizi au chanjo za hapo awali. Wamekuwa wakifanya hivi tangu mwanzo wa janga hili, na wataendelea kwa muda mrefu sana ujao, 'mbio hizi za silaha' kati ya mwanadamu na virusi zitaendelea (misamiati isiyo  na jinsia inatumiwa kwa kiburi hapa - samehe kucheza na maneno ziada). Aina  ya Omicron imekuwa nzuri sana kwa hili hivi kwamba imekuwa familia ya viaina vidogo vinavyotambulika. Kadiri muda unavyopita, kingamwili zinazozalishwa kwa chanjo na virusi vipya kutoka Wuhan vikijitokeza mapema kutoa kinga sifuri dhidi ya maambukizi huku wanafamilia wa hivi punde wakipewa lakabu ya BA.5. Lakini, majibu ya kinga ambayo miili yetu hutoa hupunguza uharibifu unaofanywa na virusi hivi. Hii kwa kiasi fulani ni kwa sababu kingamwili sio silaha pekee inayobadilika katika mfumo wetu wa kinga. Miitikio ya kinga ya seli za T inaweza kubaki thabiti dhidi ya aina mpya, ambazo bado kimsingi ni virusi vilevile, kwa sababu seli za T huviona virusi kwa njia tofauti na seli za B zinazotengeneza kingamwili, na seli zetu za T hazidanganyiki kwa urahisi na aina za virusi kama vile seli B.

Utafiti huo ulioarifu makala hiyo ya Independent ulichapishwa katika jarida maarufu la utafiti wa kisayansi la Sayansi, na mwandishi mwenza Profesa Altmann amenukuliwa katika gazeti la Independent akisema kuhusu Omicron: "Ni aina ya virusi vya siri ambavyo huingia chini ya rada ... hata baada ya kuwa na Omicron, hatujalindwa vyema dhidi ya maambukizi zaidi”. Hajaripotiwa akisema kuwa unaweza kuambukizwa kila mwezi, kwa hivyo labda jina hili la mtindo wa kuvutia lilichaguliwa na mhariri ili kuliletea mapato zaidi gazeti hilo. Hakika, makala hayo hayo yamekuwa yakionekana mara kwa mara katika mipasho ya habari kwa tarehe mpya mpya ili kusalia machoni mwa umma.

Hili ni jambo la kusikitisha kwa sababu sayansi ni ya thamani kubwa zaidi na inapaswa kuletwa kwa utambuzi umma katika mwanga wake sahihi. Makala asili ya utafiti yanaonyesha kwamba 'uwekaji wa kinga' kutokana na maambukizi ya virusi vya asili vya Wuhan Hu-1 ulipendelea majibu ya kinga ya wale walioambukizwa na Omicron baadaye, kama vile majibu ya seli B na T yaliimarishwa dhidi ya virusi vya asili vya Wuhan Hu-1, huku ukiwa mdogo dhidi ya Omicron yenyewe. Kupungua huku kunaitwa ‘immune-damping’. Jambo hilo linaweza kuonekana kuwa la kushangaza, lakini limeelezewa mara nyingi hapo awali kwa virusi vingine. Kwa ufupi, sehemu nyingi za virusi huonekana na mfumo wa kinga kama 'vitu vigeni' na kingamwili na vipatanishi vyengine vya kinga hutengenezwa dhidi ya hivi ili kutulinda dhidi ya maambukizi ya siku zijazo. Sehemu hizi za virusi huitwa epitopes, na endapo tutaambukizwa tena mfumo wetu wa kinga sasa  utakuwa imara sana kwa 'epitopes' hizi na huongeza pakubwa mwitiko wa kinga dhidi yao. Kwa bahati mbaya, ikiwa virusi hivi vitabadilika kidogo, kupitia kugeuka maumbile ya baadhi ya epitopes hizi, mwitiko mdogo wa kinga hutolewa dhidi ya epitopes mpya na mfumo wa kinga huelekeza nguvu zake nyingi katika kuimarisha ulinzi wake dhidi ya epitopes hizo za virusi ambazo zinabaki vilevile.

Omicron na aina zozote zitakazofaulu huenda zitaendelea kuwadhuru watu kwa muda fulani ujao na janga hili ni baya mno pasipo na uhamasishaji na kurudia kuripoti tena ukweli huo huo mara kwa mara hadi watu watakapokuwa na kinga zaidi dhidi ya sasisho muhimu za afya ya umma zaidi ya walivyo kwa Uviko-19.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Dkt. Abdullah Robin

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu