Jumanne, 29 Sha'aban 1444 | 2023/03/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Uraibu wa Uhuru na Uvumilivu kwa Ushoga Umeifanya Magharibi Kuipa Mgongo Sayansi Kuweka Sayari kwenye Hatari ya Mkurupuko Mpya wa Virusi Uliokita Mizizi

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mwandishi wa habari za afya na sayansi James Gallagher aliuliza swali muhimu sana wiki iliyopita kama kichwa cha makala yake ya habari ya BBC: "Monkeypox: Je, bado tunaweza kukomesha mkurupuko?" Alifanya zaidi ya wengine wengi ‘kudhihirisha’ ukweli ulio wazi kwamba “kuwashawishi watu wafanye ngono kidogo” kungefaa sana katika kuudhibiti ugonjwa huo, lakini je, alikwenda mbali vya kutosha?

Maoni:

Kuandika ndani ya vizuizi vikali vya "utamaduni wa kughairi" wa kisasa wa Magharibi kwa kiasi fulani amekuwa muoga, juu ya hali ya ushoga ya kuenea kwa virusi vya monkeypox. Kwa mfano, aliandika kuhusu ngono kwa ujumla, lakini data rasmi za Uingereza zimeonyesha kuwa karibu kesi zote ni kwa wanaume wanaofanya mapenzi na wanaume wengine. Kwa hivyo kwa nini hakuandika swali katika suala la ngono ya watu wa jinsia moja? Yeye tu ndiye anayejua, lakini mtu yeyote anayeishi Magharibi anajua kwamba kama angeuliza swali la kuzuia vitendo vya ushoga angetuhumiwa kuwa mbaguzi dhidi ya ile inayoitwa 'jamii ya mashoga'.

Mwandishi huyo hakupuuza kabisa kipengee cha ushoga. Alichukua kama maregeo karatasi ya utafiti katika ‘the New England Journal of Medicine’ akisema kwamba "inakadiriwa 95% ya maambukizi ya monkeypox yalikuwa yakipatikana kupitia ngono, haswa ngono kati ya wanaume." Hata hivyo, kauli hii ni mukhtasari dhaifu wa matokeo ya karatasi hiyo ya utafiti ambayo yanaonekana kutokuwa na ubaguzi mchache kwa watu wa jinsia moja, kwani neno 'haswa' linamaanisha tu kwamba wengi wa 95% ya maambukizi hutoka kwa ngono ya watu wa jinsia moja. Kwa kweli, sehemu ndogo sana ya maambukizi hutoka kwa kitu kingine chochote kando na maingiliano ya watu wa jinsia moja. Jarida la ‘the New England Journal of Medicine’ na lijizungumzie lenyewe: “Kwa jumla, 98% ya watu walioambukizwa walikuwa mashoga au watu wenye jinsia mbili…Maambukizi yalishukiwa kutokea kupitia ngono katika 95% ya watu walioambukizwa.” kwa kuweka taarifa hizi pamoja inaonyesha kuwa ni 2% tu ya kesi ambazo hazina kipengee kilichothibitishwa cha ushoga na ni wazi kuwa karibu 95% yote ya maambukizi ya ngono lazima yatokane na ngono ya watu wa jinsia moja.

Kwa hivyo kwa nini serikali za Magharibi "hazishawishi watu kuwa na "ngono" chache ya ushoga? Makala hayo yanapendekeza kwamba "somo la magonjwa ya zinaa - kuanzia kwa kaswende katika Zama za Katikati hadi sasa - ni kwamba watu bado wanafanya ngono na "chanjo ndio chaguo pekee". Kulinganisha magonjwa mengine yanayoenezwa na ngono sio haki. Utafiti mwingine umeonyesha kuwa takriban theluthi moja ya walioambukizwa virusi hivyo wamefanya mapenzi na wanaume wengine 10 katika kipindi cha miezi 3 iliyopita, hivyo tatizo sio ngono kwa ujumla. Bali, monkeypox inaenezwa kwa uchafu mkubwa wa liwati.

Serikali nyingi za Magharibi zimewazuia watu wasio wanandoa kuishi pamoja katika nyumba moja. Kumekuwa na hata vikwazo kwa watu kuwa pamoja katika mabustani na maeneo mengine ya umma. Kwa hivyo, kwa Uviko-19, Magharibi iliweza kuzuia maingiliano ya kingono kwa jumla, na kwa kweli aina zote za maingiliano, lakini kwa monkeypox serikali za Magharibi hazitafunga maeneo ya mikutano ya wapenzi wa jinsia moja au kuzuia makumi ya maelfu ya watu kukusanyika kwa matembezi ya kila mwaka ya 'ufahari'.

Mtu huenda akasema kwamba Uviko-19 unaambukiza zaidi kuliko monkeypox, na kwa hivyo sheia kali zilihitajika. Tatizo ni kwamba monkeypox huenda ikabadilika, na kadiri ulimwengu wa Kimagharibi usipofanya chochote, ndivyo uwezekano wa virusi hivyo kuzoea vyema kuenea kati ya sekta zote za jamii zetu. Ikitokea hivyo; basi ulimwengu wote utateseka, na sio Magharibi tu, ambayo imekuwa huru sana hivi kwamba inaweza kutuweka sote hatarini. Badala ya kukabiliana na uhuru potovu unaoueneza kwa kiburi, na badala ya kuhatarisha kuwaudhi wafuasi wa upotovu wa kijinsia ambao wametawala jamii zao; watapuuza ukweli ulio wazi na kuacha bendera ya chanjo ingawa hakuna dozi za kutosha na ufanisi wao haujathibitishwa. Wanacheza kamari na afya ya sayari kwa jina la uliberali na kuzipa kisogo kanuni za kisayansi za udhibiti wa maambukizi. Mwenyezi Mungu atuepushe na ujinga wao wa kimfumo.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Dkt. Abdullah Robin

 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu