- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Kote Ulimwenguni Wafanyikazi Wameanza Kutilia Shaka Uhalali wa Urasilimali Kuleta Maana Katika Jamii
(Imetafsiriwa)
Habari:
Hivi majuzi, gazeti la The Guardian liliripoti kwamba wafanyikazi wanaacha kazi zao kimya kimya kote ulimwenguni katika ulimwengu wa baada ya Uviko-19. [The Guardian] Sababu kuu inayohusishwa na jambo hili ni kwamba virusi vya Korona vimewasukuma watu kutafuta maana ya maisha yao. Kuacha kazi huku kimya kimya kunafuatia kujiuzulu au mabadiliko makubwa, ambayo ni mtindo unaoonekana kwa wafanyikazi wanaojiuzulu kwa hiari kwa wingi mwanzoni mwa 2021. [CNBC] Sababu ya kujiuzulu sana huko iko katika mambo kadhaa kama vile kuongezeka kwa gharama ya maisha, kazi zisizoridhisha, kazi bora kutokana na fursa za nyumbani na kadhalika. Kuacha kazi kimya kimya pamoja na kujiuzulu kukubwa kunazua maswali yasiyofurahisha kuhusu wafanyikazi kukata tamaa na urasilimali.
Maoni:
Wataalamu wa Kimagharibi wamegawanyika sana juu ya dori ya ubepari katika kuchochea mzozo wa wafanyikazi. Profesa Robert Reich, Maziri wa zamani wa Leba wa Marekani anasisitiza kwamba umbile la kikatili la ubepari linachochea kujiuzulu kwa watu wengi. Kulingana na Reich "Hatufanyi kazi kwa ajili ya uchumi, uchumi ndio unaopaswa kufanya kazi kwa ajili yetu." [CNBC] Maria Kordowicz, profesa mshiriki katika Chuo Kikuu cha Nottingham Uingereza anaamini kwamba wafanyikazi wamechoshwa na ubepari na wanaondoka kutafuta maana kwengineko. Kordowicz anaamini kwamba wafanyikazi wanatazamia kufafanua upya uhusiano wao na ubepari kupitia kuuliza maswali kama vile “Kazi inapaswa kumaanisha nini kwangu? Ninawezaje kucheza dori ambayo inalingana zaidi na maadili yangu?"
Kuna sababu kadhaa nyuma ya mvuto unaofifia wa ubepari miongoni mwa wafanyikazi. Katika nchi za Magharibi, wafanyikazi wanalishwa mlo wa kila siku wa ubepari unaopelekea uhuru, ubinafsi, demokrasia na utajiri wa mali. Lakini kazini, wafanyikazi wengi hugundua kwamba maadili hayo hayawezi kufikiwa. Uhuru unabadilishwa na utumwa kwani wafanyikazi wanapaswa kufanya kazi kwa muda mrefu ili angaa kuishi. Ubinafsi hugunduliwa kwani wafanyikazi hujifunza kwa haraka kwamba lazima wafanye kazi ndani ya timu ili kufaulu. Demokrasia inatoa nafasi kwa udikteta wa kampuni, kwani wafanyikazi wanajikuta wana usemi mchache sana juu ya malipo, mazingira ya kazi, majukumu ya kazi, kupandishwa cheo na masuala mengi yanayowaathiri. Mwisho, ni watu wachache tu ndio wanaofika kileleni mwa jedali la utajiri, huku wengi wakijitolea maisha yao kwa ubepari ili tu kustaafu katika umaskini. Baya zaidi ni kwamba wafanyikazi wengi huzitazama kampuni wanazozifanyia kazi zikihujumu demokrasia na kutogawanya faida pamoja na jamii pana. Kwa mfano, makampuni ya nishati yanapata faida kubwa huku watu wakiteseka kutokana na gharama ya maisha na pia zinawafadhili wanasiasa ili kukaa kimya.
Sababu kuu ya kutoridhika kwa wafanyikazi na ubepari ni mfumo wa kimada inaouendesha. Ndani ya jamii za Kimagharibi, utawala wa hisia ya kimada umewapokonya wanadamu hisia yao ya kiroho, roho ya jamii na maadili ya kifamilia. Kuanzia umri mdogo, wafanyikazi katika nchi za Magharibi wanawekewa masharti ya kupata maana katika maumbo ya kimada pekee; hata hivyo, enzi ya Uviko imetoa nafasi kwa wafanyikazi kutathmini upya uhusiano wao na ubepari na kutafuta maana katika maadili na mifumo ya imani isiyo ya kimada.
Katika Ulimwengu wa Kiislamu, kutoridhika kwa wafanyakazi kunazidishwa zaidi kwa sababu wafanyikazi wengi wanang’ang’ana kuwianisha maadili ya kirasilimali yasiyodhibitika ndani ya mazingira ya kazi na maadili yao ya Kiislamu. Hii hupelekea mapambano ya kudumu ya utambulisho mahali pa kazi—wafanyikazi wengi huchagua kupunguza ushiriki wao kazini wakihofia kupoteza kitambulisho cha Kiislamu. Hakika, maendeleo ya kitaaluma huja kwa gharama ya kubeba shakhsiya ya kirasilimali juu ya ile ya Kiislamu.
Katika Uislamu, kazi ni kitendo cha kimada na madhumuni yake—tofauti na Magharibi—ni kutimiza haki na wajibu unaojumuisha maadili tofauti tofauti. Kwa hivyo wafanyikazi katika Uislamu hupata pesa za kulisha, kuvisha na kusomesha familia zao, kuwachunga wasiobahatika katika jamii yao, kujenga misikiti na kujishughulisha na vitendo vya misaada, kuwanusuru mujahidina na kadhalika. Uislamu haudharau maadili yasiyo ya kimada bali unatoa mazingira sahihi na msukumo wa kukidhi majukumu yote katika aina zote za maadili. Hivyo, chini ya dola ya Kiislamu, wasiokuwa Waislamu na Waislamu wote wana maana katika maisha na wanahimizwa kutafuta aina zote za maadili na hivyo kuleta mizani sahihi ya maisha ya kazi kwa jamii. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):
[وَمَنْ أَعْرَضَ عَنْ ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنْكًا وَنَحْشُرُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَعْمَى]
“Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki, na Siku ya Kiyama tutamfufua hali ya kuwa kipofu.” [Taha: 124]
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Abdul Majeed Bhatti – Wilayah Pakistan