Jumapili, 22 Muharram 1446 | 2024/07/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Kujumuishwa kwa Aliyekuwa Msemaji wa Al-Shabab katika Serikali ya Kidemokrasia nchini Somalia

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mwanzilishi mwenza na msemaji wa zamani wa harakati ya Mujahidina ya Al-Shabab, Mukthar Robow ameteuliwa kuwa Waziri wa Masuala ya Kidini na Waziri Mkuu wa Somalia. "Tunakaribisha uteuzi wake. Hatua hiyo itaendeleza maridhiano na itakuwa mfano mzuri kwa uasi wa ngazi za juu kutoka al-Shabab," alisema mchambuzi wa kisiasa Mohamed Mohamud. [Reuters]

Maoni:

Kujumuishwa kwa msemaji wa zamani wa Al-Shabab katika serikali ya kidemokrasia ni maendeleo ya hivi karibuni katika uhalisia wa kisiasa wa Somalia. Magharibi ilitupia jicho lake Afrika wakati wa zama za ukoloni na Somalia haikuwa tofauti kutokana na eneo lake la kistratejia ambalo ni sehemu ya Pembe ya Afrika. Amerika iliifanya kuwa ngome yake katika eneo hili kupitia mapinduzi ya kijeshi mnamo 1969 ya Jenerali Siad Barre. Koo ziliibuka, wababe wa kivita wakaibuka, na wanamgambo wote wakaibuka dhidi ya dikteta, Siad Barre, na ardhi hii imekuwa ukumbi wa vita tangu 1991. Kisha, Amerika ilituma jeshi lake kwa kisingizio cha msaada wa kibinadamu na kuunda serikali kibaraka ya mpito mnamo 2004.

Kufikia wakati huo, watu wa Somalia walikuwa wamekusanyika pambizoni mwa Muungano wa Mahakama za Kiislamu (ICU). Waliiona ICU kuwa suluhu ya mateso yao. ICU ilipata udhibiti wa maeneo mengi ya Somalia mwaka 2006. Wakati huu Amerika iliitumia Ethiopia kufanya vita na kuivunja ICU kuwa makundi makundi. Al-Shabab iliundwa kutokana na makundi ya Djibouti na Asmara mnamo 2006 kwa nia safi ya kupigana jihad dhidi ya Marekani na kuanzisha Sharia nchini Somalia. Mukhtar Roobow Abu Mansour, mmoja wa wanachama waanzilishi na msemaji wa vuguvugu la upinzani wa kisilaha linaloitwa Al-Shabab, aliwekewa zawadi ya kukamatwa kwake ya dolari milioni 5 za Kimarekani juu ya kichwa chake, kisha baada ya kuhama kwake na kuzuiliwa nyumbani, mnamo Juni 2017, Amerika iliondoa ofa ya zawadi yake ya dolari milioni 5. zawadi ya kukamatwa kwa Abu Mansour.

Baada ya kuasi, Mukhtar Roobow alijisalimisha kwa jeshi la serikali mnamo 2017; aliwekwa katika kifungo cha nyumbani, na mwaka wa 2022 sasa amejumuishwa katika wizara akiwa na wadhifa wa waziri wa masuala ya kidini. Kwa hatua hii, Amerika na jaribio lake la ubaraka la kurubuni waasi zaidi kutoka kwa harakati hiyo limedhoofisha harakati hiyo, na inajaribu kuisambaratisha kupitia shambulizi baada ya kuwadhoofisha. Ukosefu wa ufahamu wa kisiasa wa uhalisia, mipango na njama za makafiri, kukosa ufahamu wa kimfumo wa Uislamu na njia isiyoeleweka ya kusimamisha sharia, kutapelekea viongozi na harakati kuwa wahanga wa mipango ya kikatili ya wakoloni makafiri. Waumini, pindi wanapovutwa ndani ya mfumo wa Magharibi yaani demokrasia, kamwe hawataweza kufikia kile ambacho Uislamu unakitarajia; bali matokeo yanayopatikana ni matokeo machache yanayoruhusiwa ndani ya mfumo wa kidemokrasia. Mukthar Robow, ambaye alikuwa na historia ya kuvutia ya mujahid kupitia kushiriki katika vita vya Afghanistan na dhidi ya Ethiopia, sasa anatumiwa na Marekani kwa sura yake ya Kiislamu kuchukua udhibiti wa ardhi hiyo ambayo alikuwa na ushawishi wake na hili lilikuwa kupitia mazungumzo naye yaliyomfanya awe mtumwa. Kulikuwepo na harakati kadhaa ambazo ziliibuka dhidi ya ukandamizaji lakini hazikuweza kudumu kwenye ramani yake ya utendakazi; badala yake ziliangukia kwenye shinikizo na vitimbi vya makafiri.

Sheikh Taiquidin an-Nabhani (rh) anataja katika kitabu “Muundo wa Chama”, moja ya mambo yanayosababisha harakati kushindwa kufanikiwa katika mwamko ambalo ni, “Harakati hizo ziliwategemea watu ambao ndani yao utambuzi (wa’yi) sahihi ulikuwa haujakamilika na utashi (iraadah) sahihi haukukolezwa. Badala yake, watu hao walikuwa tu na matamanio na shauku pekee.” Toleo la Kiingerezac- uk. na - 04.

Vita vya wenyewe kwa wenyewe, wababe wa nchi, miili iliyokonda na njaa, hizi ndizo picha zinazojitokeza akilini mwetu tunaposikia jina Somalia, lakini kiukweli ardhi hii ina rasilimali nyingi za bahari na ina utajiri mkubwa wa madini ya urani, gesi asilia na mafuta ambazo mara kwa mara zinaporwa na dola kuu. Hii ni ardhi ambayo Uislamu ulifika katika zama za Mtume (saw); hii ndiyo ardhi iliyowahudumia maswahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu waliohama mara ya kwanza kutoka Makka. Ibn Battuta alitaja katika kitabu chake, “Mogadishu ni mji mkubwa sana. Wakaazi wake ni wafanyibiashara matajiri na huchinja ngamia mia moja kila siku”. Hii ilikuwa ndio sifa iliyokuwa nayo mahali hapa katika historia wakati wa utawala wa Uislamu. Ni kwa kusimamisha Shariah kupitia Khilafah Rashida kwa njia ya Utume pekee, kila nyanja ya maisha ya Somalia itatawaliwa kwa yale yote aliyoteremsha Mwenyezi Mungu (swt) na izza iliyopita ya Somalia itaregeshwa tena na maisha ya kaka na dada zetu huko watathaminiwa.

Kuhama kutoka kwa harakati ya Kiislamu na kushikamana na mfumo wa demokrasia wa Kimagharibi katika wadhifa wa uwaziri wa masuala ya kidini kamwe hakutashughulikia masuala ya watu na kutatua masuala ya mujtamaa kwa njia ya Kiislamu; badala yake, wanasisitiza kinidhamu juu ya usekula na kuiwekea mipaka dori ya Uislamu katika matambiko na maadili tu ya kiakhlaqi ya kibinafsi na si zaidi ya hapo. Hivi ndivyo Magharibi inavyotaka kutoka kwa waumini kama Mwenyezi Mungu Azza wa Jal anavyotahadharisha juu yao katika aya hii.

[وَلَن تَرْضَى عَنكَ الْيَهُودُ وَلَا النَّصَارَى حَتَّى تَتَّبِعَ مِلَّتَهُمْ قُلْ إِنَّ هُدَى اللَّهِ هُوَ الْهُدَى وَلَئِنِ اتَّبَعْتَ أَهْوَاءَهُم بَعْدَ الَّذِي جَاءَكَ مِنَ الْعِلْمِ مَا لَكَ مِنَ اللَّهِ مِن وَلِيٍّ وَلَا نَصِيرٍ]

“Mayahudi hawawi radhi nawe, wala Wakristo, mpaka ufuate mila yao. Sema: Hakika uwongofu wa Mwenyezi Mungu ndio uwongofu. Na kama ukifuata matamanio yao baada ya ujuzi ulio kwisha kujia, hutapata mlinzi wala msaidizi kwa Mwenyezi Mungu.” [Surah Al-Baqarah: 120]

Mwenyezi Mungu (swt) auongoze Ummah huu na auweke imara juu ya Haki bila ya kulegeza msimamo mpaka itimie ahadi yake.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Muhammad ibn Shamsudeen

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu