- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Vita vya Waterloo: Dhihirisho la Ubepari Halisi
(Imetafsiriwa)
Habari:
Mifupa ya wanajeshi waliokufa kutokana na Vita vya Waterloo yatumiwa katika viwanda vya sukari.
Maoni:
Katika kila uwanja wa vita vilivyofanyika katika historia ya hivi karibuni, kuna aina fulani ya mabaki ya wanadamu ambayo yanaweza kufuatiliwa hadi katika tukio hilo, isipokuwa Vita vya Waterloo vilivyotokea mnamo 1815 huko Uholanzi Kusini ambayo siku hizi ni mahali nchini Ubelgiji, karibu na Brussels mji mkuu wa kisiasa wa Ulaya. Vita hivi vilifanyika kati ya Wafaransa chini ya uongozi wa Napoleon na muungano wa Waingereza, Wajerumani na Waholanzi. Maelfu ya wanajeshi waliuawa kwa mujibu wa vyanzo vya kihistoria na takriban miili 20,000 ilitoweka kwenye makaburi ya halaiki, lakini ni nadra kwamba kuna mabaki ya binadamu yaliyopatikana wakati wa uchimbaji mpaka sasa.
Mzozano kati ya wanahistoria na wanaakiolojia wanaohusika na kesi hii ni iwapo mabaki ya wanajeshi hao yamesagwa kuwa unga wa mifupa kwa ajili ya kutumiwa kama ya mbolea katika kilimo au kama mifupa hiyo imesindikwa kwa wingi katika sekta ya sukari tangu 1834. Katika kesi hiyo ya mwisho, kabichi la mfupa lilitumiwa kusafisha sukari kutokana na viazi sukari. Hii kawaida hufanywa kwa mifupa ya wanyama. Lakini kulingana na watafiti, mifupa ya wanajeshi kwenye makaburi ya halaiki ilitumika katika viwanda hadi chanzo cha mifupa kilipokwisha mnamo 1860.
Uzalishaji wa sukari kwa mifupa ya binadamu yaonekana haikuwa siri wakati huo kwani gazeti la Ujerumani liliandika mwaka wa 1879 kwamba kwa kutumia asali kuwa kirutubisha utamu, unaepuka hatari ya "kuyeyusha chembe chembe za babu yako ndani ya kahawa yako."
Kila mwanadamu anayesoma haya atachukizwa. Hata hivyo, ikiwa tunafikiri kwamba njia hii ya kuchukiza inayochafua tumbo ilikuwa tu tukio la mara moja pekee, basi hatuna habari kabisa ya urasilimali mkatili unaotuzunguka. Namna inavyoonyesha kuogofya, kusaga na kutumia mifupa ya binadamu kama njia ya kuongeza uzalishaji, hiki ni kielelezo tu cha mawazo ya kibepari. Mawazo haya yamehalalisha mataifa ya Kirasilimali kuvamia mataifa mengine, kuwaua, kuwapora njia zao, hadhi yao na utu wao na kuwafanya watumwa. Ingetosha kuutaja ukatili unaofanywa na watu hawa waliojitajirisha wenyewe kwa mifupa ya watu wao dhidi ya watu wa Congo. Waliua kati ya watu milioni nane hadi kumi wa Congo, wakajeruhi vibaya mamilioni na kuwafanya watumwa.
Muda mfupi baadaye, mnamo 1958, walifanya Maonyesho ya Ulimwenguni yaliyopewa jina la Expo 58 huko Brussels, ambapo walikuwa na mbuga ya wanyama iliyojumuisha watu kutoka Congo ili kuonyesha mataifa ya Kimagharibi "Waafrika Washamba." Watu hawa ambao walitiwa kwenye mapango kama wanyama na wageni wangenunua njugu na ndizi na kuwarushia, nyuma ya uzio.
Mawazo haya ndio yale yale yaliyosaga mifupa, nyama na damu za mamilioni ya Waislamu kutoka Afrika Kaskazini hadi Indonesia na bado yangali yanaendelea kufanya hivyo. Hili kamwe halitabadilika isipokuwa Waislamu waungane chini ya kivuli cha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Hapo tu ndipo wanadamu wataweza kuokolewa kutokana na Urasilimali katili.
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Okay Pala
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Uholanzi