Jumamosi, 21 Muharram 1446 | 2024/07/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Karne ya Uturuki: Uasherati, Utegemezi, Kurudi Nyuma na Mengine Mengi

(Imetafsiriwa)

Habari:

Akizungumza katika mwaka wa 6 wa utunzi wa sheria wa muhula wa 27 wa Bunge Kuu la Uturuki, Erdoğan alisema, "Tukiregelea maadhimisho ya miaka 100 ya kuanzishwa kwa Jamhuri yetu, ambayo tutasherehekea pamoja kwa shauku mwaka ujao, tunakuja katika uwepo ya taifa letu mwaka 2023 na neno jipya. Ahadi hii ni kujenga 'Karne ya Uturuki' juu ya kazi na huduma ambazo tumeleta katika nchi yetu hadi sasa. (Yeni Şafak 03.10.2022)

Maoni:

Tunaporegea kipindi cha baada ya kutangazwa kwa Jamhuri mwaka 1923, tunakumbana na utegemezi kwa dola za kikoloni, ukosefu wa maadili, kurudi nyuma, kuyumba kiuchumi na kisiasa, mauaji, unyanyasaji dhidi ya wanawake, uhamiaji na mengine mengi mabaya ya jamhuri. Niamini mimi, mabaya ya jamhuri hayana idadi. Katika kipindi cha miaka 100 iliyopita, Jamhuri ya kisekula ya Kituruki haijaacha mafanikio yoyote bora zaidi ya machafu. Kwake, kauli mbiu isiyo eleweka na iliyofungwa ya "Karne ya Uturuki" si chochote bali ni kauli mbiu tupu na ya udanganyifu inayotolewa ili kuuhadaa umma katika viwanja vya uchaguzi.

Jamuhuri ya kisekula iliyojengwa juu ya magofu ya Khilafah, iwe ni nyakati za masekula wakali kuwa madarakani au iwe ni wakati eti wanaodaiwa kuwa Waislamu wako madarakani, kama ilivyo sasa, haijatoa chochote isipokuwa huzuni, mateso, uasherati nk. kwa Waturuki. Haitaahidi chochote tofauti na haya katika karne ijayo. Tatizo sio nani anatawala, bali ni nini kinachotawaliwa. Jamhuri ya kisekula, ambayo haichipuzi kutokana na aqida ya Umma wa Kiislamu, haiwezi na haitawezi kutoa maisha ya heshima wanayostahiki, isipokuwa kwa kuliburuza taifa la Uturuki kwenye bonde la ghayya (bonde la Motoni) katika karne ijayo.

Kwa sababu msingi wa ule mradi unaoitwa "Karne ya Uturuki" ni demokrasia ya kisekula. Demokrasia ya kisekula iko dhidi ya maumbile ya mwanadamu na haikujengwa juu ya akili. Miradi na kauli mbiu kama hizo zinagongana na maumbile ya mwanadamu na zisizoegemezwa juu ya imani ya watu wa Uturuki haziwezi kuahidi chochote isipokuwa mateso na kutokuwa na furaha kwa watu. Uthibitisho wa hili ni miaka 100 iliyopita. Kufeli ambako miaka 100 iliyopita imewasilisha kwa watu wa Uturuki kunasababishwa na mfumo. Hivyo basi, maadamu mfumo wa sasa wa kisekula unasalia kufanya kazi, miaka 100 ijayo haitakuwa tofauti sana na miaka 100 iliyopita, au itakuwa mibaya zaidi. Kwa sababu kutarajia bidhaa safi na isiyoharibika kutoka kwa mfumo mbovu na uliopitwa na wakati wa kisekula ni ndoto, mithili ya kufukuzia mangati.

Mradi wa "Karne ya Uturuki", ambao Rais Erdogan aliutambulisha kwa wananchi kuanzia kabla ya uchaguzi, ni simulizi yenye mwelekeo wa uchaguzi, iliyofungika na yenye utata inayolenga kuuhadaa umma, kama nilivyotaja hapo juu. Ni kama kutupa jiwe gizani. Kwa sababu ikiwa kweli tunataka kuelewa na kudiriki ni aina gani ya karne ijayo inatungoja, tunahitaji tu kutazama karne iliyopita. Karne iliyopita kulingana na mfumo wa kisekula ni ushuhuda wa karne ijayo.

Tofauti na Erdogan, kama Hizb ut Tahrir, tunasema kwamba karne ijayo itakuwa ni Karne ya Khilafah. Tunaposema hivi, hatutupi mawe gizani, wala hatuzungumzii suala la madhaniwa na ndoto. Kinyume chake, Khilafah ni ahadi ya Mwenyezi Mungu (swt) na bishara njema ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw). Aidha, Khilafah ni hitaji la Waislamu wote duniani, na hitaji hili linaongezeka siku baada ya siku. Ili hitaji hili liweze kugeuka kuwa vitendo, watu wenye

(وَعَدَ اللّٰهُ الَّذ۪ينَ اٰمَنُوا مِنْكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْاَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذ۪ينَ مِنْ قَبْلِهِمْ)

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao” [Surah An-Nur: 55] «ثم تكون خلافة على منهاج النبوة» “Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume” (Ahmad)

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Ercan Tekinbaş

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu