Jumapili, 22 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Waziri wa Fedha Hawezi Kurekebisha Uchumi wa Pakistan Unaodhibitiwa na IMF

(Imetafsiriwa)

Habari:

Waziri wa Fedha wa Pakistan, Bw. Ishaq Dar mnamo Jumapili, tarehe 16 Oktoba 2022, aliusihi Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) na wafadhili wa kimataifa kutoa usaidizi mkubwa wa kisera. Aliiomba IMF kuunda muitiko wake kuafikiana na hali ya Pakistan na nchi zilizo na hali kama hiyo kwa kuzingatia changamoto kubwa za kiuchumi, kijamii na kisiasa zinazokabiliana nazo huku kukiwa na majanga yanayosababishwa na tabianchi, kulingana na taarifa moja kwa vyombo vya habari iliyotolewa na wizara ya fedha.

Finance Minister of Pakistan, Mr. Ishaq Dar on Sunday, 16th October 2022, urged the International Monetary Fund (IMF) and multilateral donors to provide greater policy support. He asked the IMF to tailor its response to the situation in Pakistan and similar countries by taking into consideration the serious economic, social and political challenges that they face amid climate-induced calamities, according to a press release issued by the finance ministry.

Maoni:

Bwana Ishaq Dar alichukua jukumu la Wizara ya Fedha mnamo tarehe 28 Septemba 2022. Ujio wake ulisherehekewa na serikali, pamoja na wanauchumi wengi, ambao walikuwa na matarajio makubwa kwamba ataweza kuleta ustawi wa kiwango cha ubadilishaji wa Rupia ya Pakistan, ambayo ilikuwa ikianguka kwa mteremko dhidi ya dolari, na hivyo kuutoa uchumi nje ya hatari. Bw. Dar alidai kuwa kwa maoni yake kiwango halisi cha ubadilishaji wa Rupia ya Pakistan ni karibu Rupia 200 kwa dolari. Aliposhika madaraka, dola ilikuwa ikiuzwa kwa Rupia 232 katika soko la wazi. Baadaye Rupia ilianza kupata faida na mwendo wa kasi uliendelea, hadi ikagusa Rupia 218 dhidi ya dolari moja. Lakini ilianza tena kupoteza nguvu na kwa sasa inafanya biashara kwa kiwango cha Rupia 224, dhidi ya dolari katika soko la wazi.

Ili kudumisha thamani nzuri ya Rupia dhidi ya dolari, Pakistan inahitaji akiba nzuri ya dolari. Kuna vyanzo vinne vya kupata dolari zaidi, mahuruji, fedha kutoka nje, uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje na mikopo ya nje. Kwa kuwa ni nchi ambayo inaagiza bidhaa nyingi kutoka nje, ikilinganishwa na mauzo ya nje, Pakistan daima inabakia kuwa nchi yenye upungufu wa dolari, licha ya kupokea pesa kutoka nje. Ili kuziba pengo hilo, Pakistan inategemea uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni au mikopo kutoka kwa IMF, Benki ya Dunia na zile zinazoitwa nchi rafiki. Hata hivyo, hata kama una akiba kubwa sana ya dolari, hata hivyo huwezi kuimarisha Rupia dhidi ya dolari, kama tulivyoona katika kesi ya India. Rupia ya India inaendelea kupoteza thamani yake kwa mwaka mmoja uliopita. Leo hii inauzwa kwa Rupia 82 za India dhidi ya Dolari ya Marekani, licha ya kuwa na akiba ya zaidi ya dolari bilioni 550. Fauka ya hayo, Benki Kuu ya India (RBI) iliingiza karibu dolari bilioni 100 sokoni katika kipindi cha miezi 12 iliyopita ili kuleta ustawi kwa Rupia ya India.

Matarajio makubwa kutoka Dar yalianza kwa haraka sana. Ana zana zile zile tu zinazotolewa na mfumo wa kirasilimali, ambao umetumiwa na kila waziri wa fedha wa Pakistan. Kwa hiyo, Bw. Dar naye pia anaiomba IMF na Benki ya Dunia ile ile kutoa msaada mkubwa zaidi. Pakistan tayari imekuwa ikipokea kile kinachoitwa msaada wa IMF na mashirika ya wafadhili wa kimataifa. Hata hivyo, msaada huu umesababisha tu kutegemea zaidi dolari, Marekani na Magharibi, kiasi kwamba tumepoteza uhuru wetu wa kiuchumi. Hivyo kudai msaada mkubwa kutoka kwa IMF na Benki ya Dunia bila shaka kutasababisha utegemezi na utumwa zaidi.

Tunahitaji mabadiliko msingi. Tunapaswa kuhamia sarafu ya dhahabu na fedha, kutangaza mafuta, gesi, umeme kama mali ya umma, ambayo itapunguza bei, kuanzisha viwanda vizito ili kujitegemea, kukomesha riba na malipo yote ya riba, pamoja na mambo mengine mengi ambayo yameamrishwa na Mwenyezi Mungu (swt). Hata hivyo, mabadiliko haya msingi hayawezi kamwe kutokea chini ya demokrasia. Yanaweza kutokea tu kupitia kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume. Khilafah itang'oa mfumo wa kiuchumi wa kirasilimali. Itatabikisha mfumo wa kiuchumi wa Uislamu, na kukaidi mfumo wa sasa wa kiuchumi wa kiulimwengu, kwa kuanzisha mfumo wa kiuchumi wa kiulimwengu wa Kiislamu. Na hii ndio njia pekee ya kusonga mbele.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Mhandisi Shahzad Shaikh
Naibu Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu