Jumatano, 02 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/04
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Tukio la Kifedha la Uingereza

(Imetafsiriwa)

Habari:

“Mnamo Ijumaa asubuhi, Chansela wa Hazina ya Uingereza, Kwasi Kwarteng, aliitwa siku moja kabla kurudi London kutoka Marekani moja kwa moja hadi Downing Street, ambako aliachishwa kazi yake. Hatua hiyo ilikuja wiki tatu baada ya Kwarteng kutangaza bajeti ndogo yenye utata iliyojaa hatua za kupunguza ushuru ambazo hazijafadhiliwa zilizopelekea masoko ya fedha kudorora. Wakati mmoja, pauni ilishuka hadi kiwango cha chini kabisa dhidi ya dolari katika miongo kadhaa.” Ripoti ya CNN iliendelea: “Kuondoka kwa Kwarteng, hata hivyo, haimaanishi kuwa Truss ametoka hatarini. Ushuru wa chini, sera za soko huria ambazo Kwarteng alitangaza zilikuwa tikiti halisi ambayo kwayo Truss aligombea kuwa waziri mkuu.”

Maoni:

Liz Truss amekuwa afisini siku 39 baada ya chama cha conservative kumuondoa mcheshi wake wa zamani wa waziri mkuu, Boris Johnson. Sasa, waziri mkuu wake mpya yuko matatani kutokana na msukosuko wa kiuchumi uliosababishwa na bajeti ndogo, inayojulikana kama tukio la kifedha (fiscal event), iliyoanzishwa ndani ya siku chache baada ya kuchukua madaraka. Katika taarifa fupi baada ya kumfuta kazi chansela wake alisema: "sehemu za bajeti yetu ndogo zilikwenda mbali zaidi na haraka zaidi" na ilhali alisema bado “amedhamiria kabisa kuona kile nilichoahidi - kuleta ukuaji wa juu zaidi, na ustawi zaidi wa Uingereza ili kutuvusha ile dhoruba tunayoikabili.”

Kinachojulikana kama punguzo kubwa la ushuru la bajeti ndogo lilipaswa kufadhiliwa na ukopaji ambao ungeongeza viwango vya riba. Kilichofuata ni kuweka dau la fedha za ukingoni dhidi ya pauni na kupata faida kubwa huku thamani ya sarafu ya Uingereza ikiporomoka kwa viwango vya kihistoria na Benki Kuu ya Uingereza ikilazimika kuingilia kati ili kuleta usawa katika soko la bondi - ambalo huamua ni kiasi gani kitaigharimu serikali kukopa pesa. Tangu wakati huo, baadhi ya ahadi za kupunguzwa kwa ushuru zilighairiwa na Truss aliendelea na sera ya U-turns baada ya kumfuta kazi Kwarteng. "Tunahitaji kuchukua hatua sasa ili kuyahakikishia upya masoko" alisema alipokuwa akibadilisha lengo la bajeti ndogo la kuondoa ongezeko lililopangwa la ushuru wa makampuni.

Aliulizwa ni kwa nini abakie kuwa waziri mkuu wakati janga la bajeti ndogo lilikuwa kama mpango wake kama ilivyokuwa kwa Kwarteng na ikizingatiwa kuwa ilitekeleza sehemu kubwa ya ahadi yake ya uchaguzi ili kupunguza kodi na kuchochea ukuaji. Majibu yake hayajatia imani katika uongozi wake. Uzembe unaoonekana katika kutangaza mabadiliko makubwa ya kibajeti bila kueleza ipasavyo jinsi upunguzaji huo ungefadhiliwa, ikifuatiwa na U-turns kulazimishwa zilizofuata mtikisiko wa soko uliotokea imemweka yeye na chama chake katika hali ngumu. Hata hivyo, kuna maswali mengine ya kuuliza hapa.

Kwa upande moja, ni nini kilichotokea kwa Uingereza kwamba inatatizika kupata viongozi wa dola wanaoweza kuongoza nchi kwa werevu nyumbani na kwa uhuru kwenye jukwaa la ulimwengu? Kwa upande mwingine, bila kujali hesabu potofu za bajeti ya uchumi mkuu na za kisiasa, kuyumba kwa uchumi unaotegemea riba wa nchi za Magharibi kunaendelea kuwaadhibu maskini kwa gharama ya matajiri. Bajeti yenyewe ilipendelea sana matajiri kuliko maskini, na dau la fedha za ukingoni ambazo zilisisitiza ukosefu wa utulivu zilipata faida kubwa kwa matajiri kwa gharama ya maskini kwa muda wa masaa chache tu. Truss aliahidi kutafuta ukuaji, lakini kwa kutumia njia mpya. Iwapo atafaulu, pamoja na Chansela wake mpya, Jeremy Hunt, mwendo usio na kikomo wa kuelekea kuwafanya matajiri kuwa matajiri zaidi utaendelea huku wengi wakitarajia, bora zaidi, msimu wa baridi kali na ghali katika miezi ijayo na, baya zaidi, kuzorota zaidi kwa msukosuko wa kiuchumi, na sera ya NATO ya kumkausha damu adui yake wa zamani Urusi kupitia vita vya Ukraine vinavyokaribisha hatari zaidi ya maafa ya nyuklia.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Dkt. Abdullah Robin

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu