Jumamosi, 11 Rabi' al-awwal 1446 | 2024/09/14
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hijab sio Chaguo la Kibinafsi; ni sehemu ya Nidhamu ya Kijamii katika Sharia

(Imetafsiriwa)

Habari:

Teen Vogue alitoa hadithi yenye kichwa “Kuvaa Hijab Kunapaswa Kuwa Chaguo la Kibinafsi, Wanawake wa Kiislamu wa Kimarekani Wanasema.” Madhumuni ya makala hayo ilikuwa ni kukuuza utofauti na ujumuishwaji na kutoa sauti kwa yale yanayoitwa makundi yaliyotengwa. Nukuu ifuatayo inaweza kupatikana katika makala hayo, “Tangu mwishoni mwa karne ya 19, alama hii ya kibinafsi lakini ya hadharani ya imani ya mwanamke wa Kiislamu imetumika kama chombo cha kisiasa kudhibiti uhuru wa kimwili wa wanawake. Tukio la kwanza linalojulikana la kupiga marufuku hijab lilianzia wakati Waingereza walipoikoloni Misri. Balozi mkuu, Lord Cromer, aliita hijab "kizuizi hatari" kwa wanawake wa Misri wanaoshiriki katika hadhara ya Kimagharibi. Ikurudi nyumbani Uingereza, hata hivyo, alisimamia Ligi ya Kitaifa ya Kupinga Upigaji kura kwa Wanawake.”

Maoni:

Makala kama haya yametungwa kimakusudi ili kulenga akili zinazogusika za vijana wa Kiislamu na vile vile hali ya jamii kuwa na mitazamo isiyovumilika kuhusu Uislamu. Wamejichanganya katika hoja zao ili waonekane kuwa wao ni wafuasi wa Muslimah, lakini ni lazima tuwe macho ili tuwe tunatoa uthibitisho wa aina yoyote kwa hoja hizi zenye dosari. Tunakumbuka tu historia chafu ya mashambulizi ya Wasomi wa Mashariki dhidi ya fikra za Waislamu ambayo yangali changamfu na hai hadi leo katika mitindo na maumbo mapya.

Hijab haina uhusiano wowote na chaguo kwani hii ni dhana ya Kiliberali ya Kisekula inayoruhusu uvumilivu kwa maasi, hiyo ndiyo hoja nzima ya mjadala! Ikiwa tuko huru kufanya hivyo, pia kiasili tuko huru kutofanya, hilo bila shaka linahujumu sheria za Mwenyezi Mungu (swt) kwani hii inampa ushindi Shetani na maadui wa Uislamu. Vijana wa kike wa Kiislamu hawasifiwi kwa kweli kwa Hijab, wanasifiwa na kumsherehekea dada yake ambaye HAVAI hijab kama jambo la haki za binadamu lililopachikwa na akili ya mwanadamu.

Hii inathibitishwa na ukweli kwamba patina zote kama vile Ufaransa na China, kuvaa Hijab ni uhalifu "huvumiliwa" kwa ajili ya kulinda haki za binadamu hata wakati wanawake wanazuiwa kupata elimu, matibabu na hata kushambuliwa kwa ukatili.

Unafiki huu mbaya hauwezi kupenya katika fikra za vijana wetu kwani unatuweka katika hali ya kufeli katika maisha yajayo;

Mwenyezi Mungu (swt) anatuonya juu ya uwongo wa Makafiri;

(لَا يُكَلِّفُ اللَّهُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا لَهَا مَا كَسَبَتْ وَعَلَيْهَا مَا اكْتَسَبَتْ رَبَّنَا لَا تُؤَاخِذْنَا إِنْ نَسِينَا أَوْ أَخْطَأْنَا رَبَّنَا وَلَا تَحْمِلْ عَلَيْنَا إِصْرًا كَمَا حَمَلْتَهُ عَلَى الَّذِينَ مِنْ قَبْلِنَا رَبَّنَا وَلَا تُحَمِّلْنَا مَا لَا طَاقَةَ لَنَا بِهِ وَاعْفُ عَنَّا وَاغْفِرْ لَنَا وَارْحَمْنَا أَنْتَ مَوْلَانَا فَانْصُرْنَا عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ)

“Mwenyezi Mungu haikalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya iwezavyho. Faida ya iliyo yachuma ni yake, na khasara ya iliyo yachuma ni juu yake pia. (Ombeni:)Mola wetu Mlezi! Usituchukulie tukisahau au tukikosea. Mola wetu Mlezi! Usitubebeshe mzigo kama ulio wabebesha wale walio kuwa kabla yetu. Mola wetu Mlezi Usitutwike tusiyo yaweza, na utusamehe, na utughufirie, na uturehemu. Wewe ndiye Mlinzi wetu. Basi tupe ushindi tuwashinde kaumu ya makafiri.” [2: 286].

Funzo hapa ni endapo tutawaona ndugu na dada zetu wenyewe wa Kiislamu wakichukua msimamo huu wa maridhiano na utofauti huu utakuwa kama hila ya kuwatoa Waislamu kwenye njia ya Khilafah na mamlaka ya Uislamu. Hivi ndivyo nafsi ya Muislamu itakavyobaki kuridhika na Quran na Sunnah kuyeyushwa maishani na kuonekana tu katika ibada za kibinafsi badala ya utawala wa kilimwengu.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Imrana Mohammad
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu