Ijumaa, 03 Rajab 1446 | 2025/01/03
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Mfumo wa Kibepari wa Kiulimwengu Unaoongozwa na Marekani, pamoja na Maamuzi na Taasisi zake za Kimataifa, Daima Zitaiweka Pakistan Utumwani

(Imetafsiriwa)

Habari:

Akisikiliza maregeleo ya rais kuhusu mradi wa mgodi wa shaba na dhahabu wa Reko Diq mnamo tarehe 2 Novemba 2022, Jaji Munib Akhtar, aliitaja faini ya Kituo cha Kimataifa cha Usuluhishi wa Mizozo ya Uwekezaji (ICSID) ya dolari bilioni 6.5 dhidi ya Pakistan kama "bomu la nyuklia," kwani linaweza kuchukuliwa popote duniani kwa ajili ya utekelezwaji.

Maoni:

Mnamo Julai 12, 2019, mahakama ya Benki ya Dunia ilitoa adhabu ya jumla ya $6.5bn kwa Pakistan, wakati wa kuamua mzozo kati ya serikali na Tethyan Copper Com¬pany Pty (TCCP), kuhusu Mgodi mkubwa wa Reko Diq. Faini hiyo ilitolewa baada ya Mamlaka ya Madini ya Balochistan kukataa ombi la TCCP la kutaka kukodishwa kwa mamilioni ya dolari za uchimbaji madini katika jimbo hilo, kufuatia hukumu ya Mahakama ya Upeo ya 2013. Tishio la tozo ya ziada ya $2-3bn, katika usuluhishi unaosubiriwa mbele ya Jumuiya ya Wafanyibiashara wa Kimataifa, inakaribia kuwa kubwa, endapo Pakistan itashindwa kufikia makubaliano kufikia tarehe 15 Disemba, 2022. Mlango mwingine wa shinikizo kwa Pakistan utafunguliwa na Sheria ya Uwekezaji wa Kigeni nchini Pakistani (Ukuzaji na Ulinzi) (FIPPA) 2022.

Sio kawaida kwa serikali kuitaka Mahakama ya Upeo kutakasa mapema makubaliano ya kibiashara kati ya nchi “huru”, Pakistan na kampuni inayoongoza duniani ya uchimbaji madini, ambayo ina amri ya Kituo cha Kimataifa cha Usuluhishi wa Mizozo ya Uwekezaji (ICSID), ambayo mamlaka yake yanatekelezeka kimataifa.

Imedhihirika kuwa katika mfumo wa sasa wa ulimwengu, hakuna ubwana kwa dola yoyote, nje ya dola kubwa. Kwa hiyo “ubwana wa kitaifa” unaochukuliwa kuwa “mtakatifu” katika mfumo wa sasa wa ulimwengu si chochote ila ni udanganyifu. Kwa upande mmoja, dola zinaruhusiwa kutunga sheria zao wenyewe, kwa jina la ubwana wa kitaifa. Hata hivyo, seti nyingine ya hukumu na sheria imelazimishwa juu yao, kwa jina la Sheria ya Kimataifa na taasisi za kimataifa kama vile ICSID.

Maamuzi ya kimataifa yanapata utukufu juu ya sheria za kitaifa, kwa sababu dola zina haki ya kutunga sheria, kutokana na mfumo wa kidemokrasia. Kwa hivyo sheria hutungwa kulingana na maagizo ya nchi za wakoloni, kuhakikisha utukufu wa maamuzi na hukumu za kimataifa, kama tulivyoona katika Sheria Iliyopendekezwa ya Uwekezaji wa Kigeni nchini Pakistan (Ukuzaji na Ulinzi) ya 2022 (FIPPA) .

Kwa hiyo, baada ya kuwa mwanachama wa Umoja wa Mataifa, Shirika la Biashara Duniani (WTO), Mahakama ya Kimataifa ya Haki, FATF na IMF, mazungumzo yoyote ya ubwana wa kitaifa na uhuru wa kweli ni udanganyifu tu. Mfumo wa kidemokrasia, utaratibu wa kimataifa na taasisi za kikoloni za kimataifa, ni "mabomu ya nyuklia" ya maadui zetu, ambayo kwayo wanatufanya watumwa pasi na kutumia silaha halisi.

Ili kufikia uhuru wa kweli, ni lazima kukomesha mfumo uliopo wa kiulimwengu. Hilo haliwezekani bila ya kusimamisha Khilafah kwa Njia ya Utume. Khilafah ni dola ambayo sheria zake zinatokana na Qur'an Tukufu na Sunnah za Mtume pekee. Hakuna sheria ya ulimwengu inayoweza kuwa na utukufu wa aina yoyote juu yake.

Khilafah ni mfumo wa serikali utakaounganisha maeneo ya Waislamu na kugeuza rasilimali zao za kibinadamu na asili kuwa nguvu kubwa, ambayo baada ya hapo hatutahitaji kusalimisha ubwana kwa ajili ya uwekezaji wowote mkubwa kutoka nje. Hii ndiyo njia pekee ambayo kwayo tunaweza kupata heshima, ustawi na radhi za Mwenyezi Mungu (swt).

[وَمَنْ أَوْفَى بِمَا عَاهَدَ عَلَيْهُ اللّٰهَ فَسَيُؤْتِيهِ أَجْراً عَظِيماً]

“na anaye tekeleza aliyo muahadi Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu atamlipa ujira mkubwa.” [Al-Fath, 48:10].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Mhandisi Shahzad Shaikh
Naibu Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu