Jumapili, 22 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Upande wa Giza wa K-Pop:

Mashini ya Unyonyaji wa Soko dhidi ya Vijana wa Kiislamu Barani Asia

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mapema Disemba 2022, Mwanadiplomasia alichapisha makala kuhusu upande wa giza wa K-Pop; ambayo chini ya picha inayometa ya sanamu za K-pop kuna moyo kama wa Dorian Grey wa tasnia ambayo inadhulumu na kuwatupilia mbali wanafunzi na nyota wake. Ingawa K-Wave inaangazia Korea Kusini na kutoa nafasi ya kimataifa ya ushawishi wa kithaqafa, umakinifu huu huja ukiwa umefinikwa na janga. Kutendewa vibaya, kujiua, kandarasi za kazi ya watumwa, ratiba za mafunzo zinazochosha, vifungu vya "kutokuchumbiana", unyanyasaji wa kingono na ugeuzaji watoto kuwa vyombo vya ngono na mashirika ya K-pop haviwezi kukosa kutambuliwa.

Kashfa ni za mara kwa mara katika K-pop, ambapo mwezi huu wa Novemba pekee ulishuhudia msanii maarufu Lee Seung-gi akigundua shirika lake la Hook Entertainment likizuia faida zote za mitiririko ya kidijitali na upakuaji wa nyimbo zake kwa kipindi cha miaka 20. Omega X, bendi ya wavulana iliyoundwa na nyota 11 waliopata nafasi ya pili, ilirekodiwa ikifokewa vikali na usimamizi. Baadaye ilishtakiwa kuwa shirika hilo lililifanya kundi kufanya kazi wakati likiwa na maambukizi ya COVID-19.

Hallyu, au K-Wave, iko mstari wa mbele katika mapinduzi ya ushawishi wa Korea Kusini na mara nyingi huunganishwa kwa kulazimishwa. Ushawishi, au nguvu ya mvuto na ushawishi wa kithaqafa, ni zana hatari na ngumu kutumia. Kwa zaidi ya miongo miwili, Korea Kusini imekuwa ikisaidia kikamilifu tasnia yake ya burudani kama injini ya "ushawishi" na ukuaji wa uchumi. Hata hivyo, linapokuja suala la wajibu wake wa kulinda Haki za Binadamu, imefeli kutekeleza. Sekta hiyo inaona faida tu katika kupanua ushawishi wake kwa Mashariki ya Kati, China, au hata Amerika Kaskazini.

Maoni:

Kilicho giza zaidi kuliko kashfa za unyonyaji wa wasanii wa K-Pop ni unyonyaji wa ushabiki kama masoko - ambao wako mamilioni. Cha kusikitisha ni kwamba wengi wao ni vijana wa Kiislamu kama waathirika. Upande wa giza wa hili unaonekana mara nyingi kuwaepuka waangalizi wa tasnia ya K-Pop. Kwa mfano, mwezi wa Novemba, bendi ya K-pop - NCT 127 ililazimika kukatisha tamasha lao la kwanza nchini Indonesia mapema baada ya wasichana 30 kuzirai kwa kuangukiana. Tamasha hilo lilikuwa likiendelea kwa saa mbili wakati mashabiki walianza kusongea mbele ili kukaribia jukwaa.

Hatari ya K-Pop kama nguvu laini ni madhara ya maadili na mitindo ya maisha, kwa sababu K-Pop imefaulu katika kunadi maadili huria, maovu na ibada ya masanamu ya mtindo wa Kimagharibi na vifurushi vya kitamaduni vya Korea ya mashariki. Zaidi ya hayo, ushabiki mkali wa K-pop kawaida hujengwa kwa kujitolea vilivyo, ambapo hujazwa na mamilioni ya mashabiki ambao wanaugua kutokana na udanganyifu na kuvutiwa kupita kiasi. Na hii ina athari ya moja kwa moja kwa Waislamu kwani nchi nyingi za Waislamu zinahesabiwa kuwa soko kubwa zaidi la tasnia ya K-Pop ambayo vijana wake wanatumiwa kama mashabiki wa nyimbo na sinema zao. Kulingana na ripoti ya Twitter mnamo Januari 2022, Indonesia inaongoza kwenye orodha kwa idadi kubwa zaidi ya Tweets za K-pop kwa mwaka wa pili mfululizo. Wakati huo huo, Malaysia iko kwenye nafasi ya 8 ambayo iko kwenye 10 bora.

Kampuni za wakala za bendi za wavulana za Korea hazisiti hata kutekeleza kile kinachoitwa unyonyaji wa soko. Jeshi la BTS, kundi la mashabiki wa kimataifa wa miondoko ya K-pop, mapema mwaka huu limeonyesha hasira yake kwa kampuni hiyo ya burudani kwa upanuzi wake mkali. Mashabiki wengi wanalalamika kuwa shirika hilo limedhamiria kuchuma pesa kwa kuuza bidhaa za mashabiki kwa bei ya juu. Bei ya bidhaa hizo ilizua mtafaruku: Seti ya pajama ya vipande viwili na mto bei yake ni Won 119,000 ($99.70) na Won 69,000 mtawalia.

Vivyo hivyo pamoja na ziara za tamasha za muziki za K-Pop zinazofanyika kote nchini, soko la mashabiki ni kubwa sana. Zaidi ya watu milioni 2.85 wanatarajiwa kuhudhuria matamasha ya K-pop katika nchi zingine mnamo 2022, huku ulimwengu ukitafuta mabadiliko kutoka kwa janga hadi janga, kulingana na Hyundai Motor Securities. Tamasha hizi hata zilizua jambo linalojulikana kama 'vita vya tikiti'. Idadi kubwa ya ratiba za tamasha la K-pop nchini Indonesia, litakalokuwa Jakarta mwaka wa 2022, imefanya mauzo ya tikiti kupingwa sana na vijana. Tamasha la Black Pink, ambalo limeratibiwa kufanyika 2023 pekee, limeanza kupingwa juu ya tiketi miezi michache iliyopita. Kufikia sasa, bei za tikiti za tamasha la K-pop ambazo zinauzwa ni kati ya dolari 50-350, sio bei rahisi kwa mifuko ya vijana wa Indonesia.

Athari ya moja kwa moja ya K-Pop kama tasnia ya utamaduni maarufu ni uharibifu na kudhoofika kwa kizazi cha Kiislamu cha siku zijazo. Vijana wa Kiislamu wamekuwa kizazi cha imma'ah ambao hawana msimamo, na ambao wana mwelekeo wa kufuata mienendo ya maisha maovu. Imma'ah ni roho ya labil inayokwenda na mwenendo wa mtiririko na walio wengi. Haina kanuni, yenye mgogoro wa kitambulisho na mawazo ya wafuasi. Kutoka kwa Hudhaifah amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

«لاَ تَكُونُوا إِمَّعَةً، تَقُولُونَ: إِنْ أَحْسَنَ النَّاسُ أَحْسَنَّا، وَإِنْ ظَلَمُوا ظَلَمْنَا، وَلَكِنْ وَطِّنُوا أَنْفُسَكُمْ، إِنْ أَحْسَنَ النَّاسُ أَنْ تُحْسِنُوا، وَإِنْ أَسَاءُوا فَلاَ تَظْلِمُوا»

“Msiwe Imma’ah; mnasema: ikiwa watu watatenda wema, sisi pia ni tutatenda wema. Na ikiwa watadhulumu, sisi pia tutadhulumu. Lakini jiandaeni (kupokea haki na kheri); Ikiwa watu watatenda wema, nanyi tendeni wema, na ikiwa watatenda maovu, nyinyi musidhulumu.” (Imepokewa na Tirmidhi).

Kutokana na hayo, K-Pop si chochote zaidi ya chombo cha ukoloni wa Kimagharibi chini ya pazia la uso wa mashariki. Ukoloni usioshikika, ambao ulifanyika kwa hila zaidi, ulitumia ukosefu wa utulivu wa akili wa vijana, ukakamua mifuko yao, na kuwafanya kuwa na utiifu wa hali ya juu kwa viigizo vyao. Huu ni mtindo wa kikoloni wenye mbinu ya 'nguvu laini' ambayo ni hatari zaidi kwa sababu imefichwa na inacheza nafasi kubwa katika maeneo ya 'syubhat' [Shub’ha] ambayo hayaeleweki, yamezibika, au hayako wazi. Zinaambatana na mtiririko wa maadili ya vyama vingi vya kisekula kama vile udhibiti wa kidini na mpango wa kupotosha ambao unaendelea kufanyiwa kampeni miongoni mwa wanafunzi wa Kiislamu. Vijana wa Kiislamu hatimaye wanakuwa mawindo rahisi ya Ubepari!

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Dkt. Fika Komara
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu