Jumamosi, 26 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Ni Khilafah Pekee ndiyo Itakayomaliza Mgogoro wa Kawi Nchini Uzbekistan!

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mnamo Disemba 14, 2022, Redio ya Liberty ilichapisha makala kuhusu kauli za Imam Rakhmatullo Sayfiddinov: "Katika muongo wa kwanza wa Disemba, Uzbekistan ilishikwa na mgogoro wa kawi. Kukatika kwa umeme kwa saa moja na foleni ndefu katika vituo vya mafuta kulionekana kote nchini. Katika wakati wa mvutano wa umma, imam mkuu wa Tashkent, Rakhmatullo Sayfiddinov, alitoa hotuba akiwahimiza watu kuwa na shukran na subira. Alisisitiza kuwa "babu zetu waliishi bila umeme na gesi," na kuwasihi Waislamu "kutoiaibisha nchi mbele ya ulimwengu mzima" kwa kuibua suala hili katika mitandao ya kijamii. Kiongozi huyo wa dini alionya kwamba "hofu, machafuko na maandamano hayatatatua tatizo hilo".

Hotuba hii ya imam mkuu wa mji mkuu wa Uzbekistan iliwakasirisha wanaharakati wa jamii. "Kwa mara nyengine tena, wito wa shukran, subira, na kampeni ya kuwapotosha watu kutoka kwenye njia ya haki ili kuendana na mtindo wao unazidi kupamba moto. Hili lazima likomeshwe mara moja. Ili kulikomesha, tunahitaji kuonyesha kutoridhika na kuandika," anaandika mwandishi wa habari Umid Soriev katika chapisho lake la Facebook. Kulingana na mwandishi huyo wa habari, imamu "anashajiisha watu wa kawaida kwenye utumwa na utiifu".

Maoni:

Huu sio mwaka wa kwanza kwamba watu wameteseka katika msimu wa baridi kutokana na ukosefu wa upashaji joto na mwanga. Licha ya hifadhi kubwa ya gesi asilia na uzalishaji wa kutosha wa umeme, ukosefu wa gesi na kukatika kwa umeme umekuwa ni mtindo nchini Uzbekistan.

Hospitali na hospitali za uzazi hazina vipasha joto, na watoto hufa kutokana na baridi kabla ya kuzaliwa. Familia zinakufa katika moto, kutokana na kupumua hewa ya carbon monoxide kutokana na usimamizi usiofaa wa vifaa vya ukanzaji moto. Viwanda vimefungwa kwa sababu usambazaji wa gesi umekatwa.

Shida hizi zinatoka wapi? Imam Rahmatullo alisema kwamba matatizo haya yanatoka kwa Mwenyezi Mungu. Ndio! Lakini si kwa sababu Mwenyezi Mungu ameyataka. Ni kwa sababu Mwenyezi Mungu (swt) ametuonya kwamba tusipofuata makatazo na maamrisho ya Mwenyezi Mungu tutaishia katika hali hii. Kwa sababu wale walio madarakani wanafanya jinai na wala hawatawali kwa Sheria za Mwenyezi Mungu, na watu hawataki kuwahesabu, wanaacha jinai hizi bila kuadhibiwa, wakifumba macho yao na kuruhusu yaliyoharamishwa kufanywa. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

(ظَهَرَ ٱلْفَسَادُ فِى ٱلْبَرِّ وَٱلْبَحْرِ بِمَا كَسَبَتْ أَيْدِى ٱلنَّاسِ لِيُذِيقَهُم بَعْضَ ٱلَّذِى عَمِلُوا۟ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ)

“Ufisadi umedhihiri bara na baharini kwa iliyo yafanya mikono ya watu, ili Mwenyezi Mungu awaonyeshe baadhi ya waliyo yatenda. Huenda wakarejea kwa kutubu.” [30:41]

Huzayfah (ra) amepokea kwamba Mtume (saw) aliapa na kusema:

»لتأمرنَّ بالمعروف، ولتنهون عن المنكر، أو ليوشكن الله أن يبعث عليكم عذابًا من عنده، ثم تدعونه فلا يستجيب لكم«

“Hamutaacha kuamrisha mema na hamutaacha kukataza maovu, isipokuwa Mwenyezi Mungu atakaribia kuteremsha adhabu juu yenu kutoka kwake, kisha mutamuomba wala hatajibu dua zenu”. [Imepokewa na Imam Tirmithi].

Wale walio madarakani wanauza utajiri wa asili wa nchi, na kudhibiti matumizi ya watu wao bila kuogopa kuambiwa au kuadhibiwa. Ambapo Mwenyezi Mungu amepitisha kwamba utajiri wa asili wa nchi kimsingi ugawiwe miongoni mwa raia wake. Imesimuliwa kutoka kwa Ibn Abbas kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

«الْمُسْلِمُونَ شُرَكَاءُ فِي ثَلَاثَةٍ: فِي الْمَاءِ وَالْكَلَإِ وَالنَّارِ» “Waislamu ni washirika katika vitu vitatu: maji, malisho, na moto”. Hadith hii hii imepokewa na Anas ikiwa na ziada «وَثَمَنُهُ حَرَامٌ» “... na uuzaji wake ni haramu.” [Imam Abu Dawud].

Wanablogu na umma wana haki ya kueleza kutoridhika kwao. Lakini kwanza, wanahitaji kuchunguza kwa kina uhalisia na kutafuta sababu halisi ya matatizo haya. Kisha wanahitaji kuelekeza kutoridhika kwao kwenye suluhisho sahihi.

 Hakuna maana kumkosoa imam aliyewekwa na serikali hii ya kihalifu. Maimamu wetu leo ni watumishi wa wale walio madarakani. Wanachoambiwa wafanye, watasema. Wanatamka maamuzi ya mabwana zao na hawajali mwamko wa Uislamu na Waislamu. Na chanzo cha matatizo haya ni mfumo wa utawala usioegemezwa katika sheria za Mwenyezi Mungu. Wale walio mamlakani wametenganisha dini na maisha, na wamechukua mahali pa watunga sheria wao wenyewe. Rais Mirziyoyev, mabwana zake na msafara wake wa wahalifu wamenyakua madaraka nchini humo na wanatekeleza uvunjaji wa sheria bila ya kuogopa ghadhabu za Mwenyezi Mungu.

Tunafanya nini!? Waislamu!? Sisi ni wale ambao Mwenyezi Mungu amewakabidhi jukumu takatifu la kuhuisha Uislamu na kueneza ujumbe wa Mwenyezi Mungu kote duniani! Katika Uislamu uamuzi ni wa Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo, suluhisho sahihi litakuwa tu mabadiliko msingi ya uhalisia wa sasa wenye kasoro. Ni lazima tuupindue mfumo wa Taghut na tusimamishe mfumo ulioteremshwa na Mwenyezi Mungu!

Waislamu! Kazi hii inafanywa na Hizb ut Tahrir. Jiungeni na kazi hii ya kuhuisha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu ndani ya Dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Ewe Mwenyezi Mungu tusaidie!

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Eldar Khamzin
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu