Alhamisi, 01 Ramadan 1444 | 2023/03/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Urusi Yatishia Nchi za Asia ya Kati

(Imetafsiriwa)

Habari:

Moscow hujenga sera yake kwa washirika katika Asia ya Kati kwa misingi ya "uvumilivu wa kistratejia" na kupunguza mahusiano na Shirikisho la Urusi huwatishia kwa gharama kubwa. Tishio kama hilo lilitolewa katika makala ya Gazeti la Kommersant ya mkuu wa idara ya tatu ya Wizara ya Mambo ya nje ya Urusi, Alexander Sternik. "Tunatathmini vitendo vya wahusika wote hasa kutoka kwa upande wa kusababisha au kutosababisha uharibifu kwa maslahi ya Urusi," alisema. "Na tunapata hitimisho la kutosha kutoka kwa hili, ikiwemo pamoja na washirika ambao wana nia kubwa ya kutopoteza mafungamano haya ya pande nyingi na Shirikisho la Urusi. Hata dokezo la kupunguzwa kwao linaweza kugeuka kuwa zile gharama za kiuchumi ambazo hakuna ahadi za fidia kutoka kwa mabwana zinaweza kugharamia", - alisema.

Maoni:

Waangalizi wanaona kuwa hofu ya Kremlin kuhusu kudhoofika kwa ushawishi wake katika nchi za Asia ya Kati dhidi ya hali ya kushindwa kijeshi nchini Ukraine sio ya msingi. Kwa upande mmoja, mkopeshaji mkuu wa nchi za Asia ya Kati, China, inajaribu kuharakisha miradi ya njia za usafirishaji zinazopita Urusi, ambayo sasa iko chini ya vikwazo, na inaimarisha ushawishi wa Beijing. Na kwa upande mwingine, tunaona uchangamshaji wa nchi za Magharibi, EU na Marekani, ambazo kwa uchangamfu zinatafuta kupatiliza fursa ya hali hiyo ili kujaza ombwe lililopo la kijiografia na kisiasa. Kwa kuongezea, pia kuna Uturuki na mradi wake wa "Muungano wa Dola za Turkic", ambao unaweza pia kushindana vinali na Urusi.

Kumbuka kwamba hii sio kesi ya kwanza ya kauli za matusi za maafisa wa Urusi dhidi ya nchi za Asia ya Kati katika siku za hivi karibuni. Sio kitambo sana, naibu mwenyekiti wa kwanza wa Kamati ya Jimbo la Duma la Masuala ya Kimataifa Svetlana Zhurova, alitishia Kyrgyzstan kwa hatima ya Ukraine baada ya taarifa ya spika wa bunge la Kyrgyz Nurlan Shakiyev kuhusu kubadilishwa majina kwa haraka kwa majina yote ya Kirusi ya wilaya za Bishkek na majina ya makaazi ya kibinafsi ya nchi. "Labda, wataripoti kwa Vladimir Vladimirovich, atatoa maoni kwa mwenzake, rais wa Kyrgyzstan," Zhurova alibaini wakati huo.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Muhammad Mansour

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu