Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Marekani Ina Siku Chache Pekee Kabla Matumizi Yake Yanayozidi Kufikia Kikomo cha Mamlaka yake ya Ukopaji

(Imetafsiriwa)

Habari:

Kichwa cha habari cha gazeti la ‘The Washington Post’ mnamo 13 Januari 2023: "Wabunge wa Republican waandaa mpango wa dharura wa kukiuka kikomo cha deni." Imeripotiwa kuwa, "Wabunge wa Republican wanatayarisha mpango wa kuiambia Wizara ya Hazina nini cha kufanya endapo bunge la Congress na Ikulu ya White House hazitakubaliana kuondoa kikomo cha deni la taifa baadaye mwaka huu, wakisisitiza kwamba wahafidhina waliopewa mamlaka wapya wataleta majadiliano ya hali ya juu ya kuepusha kushindwa kulipa madeni kwa Marekani, kwa mujibu wa watu sita wanaofahamu mijadala ya kindani.”

Maoni:

Deni la Marekani linaendelea kupanda na sasa limefikia $31.4 trilioni. Janet Yellen, Waziri wa Hazina wa Marekani, aliliambia Bunge la Congress wiki iliyopita kwamba Marekani itafikia kiwango cha juu kinachoruhusiwa cha kukopa mnamo tarehe 19 Januari. "Mara tu hatua zote zinazopatikana na pesa zilizopo zimekamilika, Marekani haitaweza kutimiza wajibu wake kwa mara ya kwanza katika historia yetu," kwa mujibu wa Waziri wa Hazina wa Marekani, Yellen. Alimuonya spika mpya aliyechaguliwa wa Baraza la Wawakilishi “Kushindwa kutimiza majukumu ya serikali kungesababisha madhara yasiyoweza kurekebishwa kwa uchumi wa Marekani, maisha ya Wamarekani wote, na ustawi wa kifedha duniani. Ninaiomba kwa heshima Congress kuchukua hatua haraka ili kulinda imani kamili na sifa za Marekani.”

Congress huamua kiwango cha juu cha deni na hiyo huweka mipaka ya kiasi cha pesa ambazo Amerika inaweza kukopa kila mwaka. Hata hivyo, deni hilo linaendelea kuongezeka na kikomo kinafikiwa kila baada ya miaka michache, na mgogoro unawezekana kutokea kwani wana Republican na wana Democrat hulitumia tishio linalokuja la maafa ya kiuchumi kwa kujipatia maridhiano ya sera zao wenyewe ili kufikia makubaliano ya kuongeza kikomo. Mnamo 2011, mgogoro ulisababisha wakala wa mikopo kupunguza ukadiriaji wa mkopo wa Amerika kabla ya makubaliano kupitishwa. Mnamo mwaka wa 2013, serikali hiyo ya kifederali ilifungwa kwa siku 16, na mnamo 2018 kufungwa kulidumu kwa siku 35 wakati Bunge linalodhibitiwa na Democrat lilibishana na Trump kuhusu ufadhili wa ujenzi wa ukuta wa mpaka wa Amerika na Mexico. Mambo yako kinyume sasa, na Rais ni Mwanademocrat, na Baraza la Wawakilishi, ambalo licheza dori kuu katika mijadala ijayo, linadhibitiwa na wana Republican. Mabishano yale yale na shutuma zile zile za kinafiki zitapita baina ya pande zote mbili huku kila mmoja akimshutumu mwenzake kwa mambo yale yale ambayo wao wenyewe waliyafanya wakati wa mgogoro wa mwisho wa deni.

Kunaweza kuwa na ukosefu wa utulivu katika soko la fedha katika wiki zijazo, lakini mgogoro huo utachukua muda kuendelea kwa sababu serikali ya kifederali imetekeleza 'hatua maalum.' Hizi ni mbinu za uhasibu za kutumia pesa kwa miezi michache zaidi bila kuonekana ndani ya vitabu vya hesabu na kuchelewesha malipo mengine kama yale ya mifuko ya pensheni. Ikiwa pande hizo mbili hazijafikia makubaliano kufikia msimu wa joto, basi kutakuwa na shida. Warepublican sio tu kwamba wamepata wingi wa kura katika Baraza la Wawakilishi, lakini pia wamebadilisha kanuni ili kufanya iwe vigumu zaidi kwa sheria (kama vile kuongeza kiwango cha deni) kupitishwa, na wanatiwa moyo na matatizo mengi yanayoukabili utawala wa Biden. Kuna uwezekano kwamba wataushinikiza utawala wa Biden kupunguza matumizi na hii inaweza hata kuathiri sera ya kigeni na kupunguza msaada wa kifedha wa Marekani kwa Ukraine, ambayo haipendelewi sana miongoni mwa wengi katika Chama cha Republican.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Dkt. Abdullah Robin

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu