Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Imam kutoka Crimea Afungwa Miaka 17 Jela kwa Kulingania Uislamu!

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mnamo Januari 12, shirika la habari la BBC NEWS liliripoti kwenye ukurasa wake wa lugha ya Kirusi: "Mahakama ya kijeshi huko Rostov-on-Don ilimhukumu Imam Raif Fevziev, anayezuiliwa nchini Crimea iliyounganishwa na Urusi, miaka 17 katika gereza kali la serikali. Alishtakiwa katika kesi ya Hizb ut-Tahrir, shirika ambalo linatambuliwa kuwa la kigaidi na lililopigwa marufuku nchini Urusi lakini sio nchini Ukraine.

Imamu huyo mwenye umri wa miaka 42 kutoka kijiji cha Crimea cha Strogonovka alihukumiwa chini ya sheria ya Urusi: alituhumiwa kwa kupanga seli ya kigaidi (Sehemu ya 1 Kifungu cha 205.5 cha Kanuni ya Jinai) na kuandaa kunyakua mamlaka (Kifungu cha 278 cha Kanuni ya Jinai).

Siku moja kabla, katika "Mahakama hiyo hiyo ya Kijeshi ya Wilaya ya Kusini ya Rostov-on-Don, Waislamu watano wa Crimea walihukumiwa kifungo cha miaka 13 - wako katika kesi mithili ya hiyo ya chama cha Kiislam "Hizb ut-Tahrir", kinachotambuliwa kama cha kigaidi katika Shirikisho la Urusi". Hii inaripotiwa na wanachama wa chama cha umma "Crimean Solidarity".

Maoni:

Kremlin inaendelea na jinai zake dhidi ya Waislamu wa Crimea, na hasa dhidi ya Waislamu wachangamfu wanaolingania Uislamu. Ikijua kwamba Waislamu wa Crimea hawataachana na Uislamu na wataendelea kutekeleza na kueneza dini yao, utawala wa Kremlin, ili kulazimisha nguvu yake juu ya Waislamu wa Crimea, hutumia njia ya vitisho vya kimwili kwa njia ya upekuzi, ukamataji, mauaji ya mahakamani na tuhuma za uwongo za shughuli za kigaidi.

Hizb ut Tahrir inalingania Uislamu kama mfumo kamili wa maisha unaotatua matatizo ya mwanadamu, jamii na serikali. Uislamu una sheria za mfumo wa kijamii, serikali, uchumi, sera ya elimu, sera ya kigeni ya serikali, mfumo wa adhabu, na sheria zengine.

Hizb ut Tahrir hufanya kazi za kimfumo na kisiasa kwa mujibu wa njia ya Utume, kuunda mujtamaa wa Kiislamu. Mawazo ya Hizb ut Tahrir, yakiwa ya kifikra, yanashawishi akili ya mwanadamu, na kuafikiana na umbile lake. Mawazo haya yana ushawishi mkubwa kwa wabebaji wake, na kila mtu ambaye angalau mara moja aliwasiliana na Mashababu wa Hizb. Na kwa hivyo, Waislamu wa Crimea, wakiwa wamekinaishwa na fikra za Hizb ut Tahrir, wakiwa wamepokea utulivu nyoyoni, na kwa imani thabiti, wanafanya kazi, juu ya mwamko wa maisha kamili ya Kiislamu bila huzuni na bila hofu ya kukamatwa na kukandamizwa. Na kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu, hivi karibuni, Mwenyezi Mungu atatimiza ahadi yake kwa Waislamu wa Crimea na kwa Waislamu wote duniani. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Kitabu Chake Kitukufu:

(وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُم فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَى لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُم مِّن بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْنًا يَعْبُدُونَنِي لَا يُشْرِكُونَ بِي شَيْئًا وَمَن كَفَرَ بَعْدَ ذَلِكَ فَأُوْلَئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ)

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu.” [24:55]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Eldar Khamzin
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu