- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Amiri wa Hizb ut Tahrir Tafuteni Kheri kutoka kwa Wanajeshi wa Waislamu
(Imetafsiriwa)
Habari:
Mazingira ya kumbukumbu ya miaka 102 ya jinai ya kuivunja Dola ya Khilafah ambayo ilifanywa na mkoloni Kafiri Magharibi kwa usaidizi wa wasaliti wa Kiarabu na Kituruki, yangali yananing'inia juu yetu mnamo tarehe 28 Rajab mwaka wa 1342 H sawia na tarehe tatu Machi mwaka wa 1924 M.
Maoni:
Kwa mnasaba wa kumbukumbu ya miaka 102 ya kuvunjwa kwa Dola ya Khilafah, Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir iliandaa kampeni ya mtandaoni yenye kichwa: "Khilafah inasimamishwa vipi", iliyojumuisha amali mbalimbali. Kampeni yake ilifikia kilele jioni ya Jumamosi, 27 Rajab Al-Muharram 1444 H sawia na 18 Februari 2023 M, kwa kongamano maalum la kuhitimisha lililofunguliwa na Amiri wa Hizb ut Tahrir, mwanachuoni mkubwa Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, Mwenyezi Mungu amuhifadhi, kwa hotuba iliyoanza kwa kuukumbusha Ummah juu ya kuvunjwa kwa Khilafah yake mikononi mwa Magharibi kafiri, ikiongozwa na Uingereza, na kwa ushirikiano wa wasaliti wa Kiarabu na Kituruki. Na jinsi historia yake ilivyokuwa giza baada ya hapo, kwani Khilafah ilikuwa dola yake ya haki na uadilifu, dola zake sasa ni zaidi ya hamsini zilizovunjika vunjika, na jeuri ya watawala wake baina yao ni kali, hata tetemeko la ardhi la Syria na Uturuki, licha ya ukali wake, halikuweza kuondoa mgawanyiko wao na kuregesha umoja wao ndani ya dola moja, na jinsi Ummah na ardhi zake zilivyoporwa na kila mwenye tamaa, hata Mayahudi wa upeo usio wa kawaida walisubutu kuushambulia, ambapo waliumiliki na kunyakua ardhi yake iliyobarikiwa.
Kisha yeye, Mwenyezi Mungu amhifadhi, akawakumbusha Waislamu kwamba uchokozi dhidi yao haukabiliwi kwa maneno ya kuvutia na yasiyo na manufaa, bali uchokozi huzuiliwa kwa makali ya upanga, kwa mapigo yanayomfanya adui asahau minong’ono ya Shetani. Hivi ndivyo walivyokuwa Waislamu walipokuwa na Khilafah, na alisambaza taswira na matukio kadhaa kutoka kwenye historia angavu ya Khilafah ambayo ni dalili ya hili.
Kisha akamalizia hotuba yake, akiielekeza hotuba yake kwa watu wenye nguvu na uthabiti katika Ummah wetu kwa kusema: “Kwa kumalizia, narudia kuwasihi enyi watu wenye uwezo na ulinzi... Nyinyi pekee ndio mnaoweza kuuponya moyo wa Ummah kutoka kwa maadui zake, maadui wa Dini yenu. Nyinyi pekee ndio mnaoweza kukomesha udhalilifu uliowafikia Waislamu katika ardhi zao... Basi inukeni kutekeleza wajibu wenu, Mwenyezi Mungu (swt) awabariki. Simameni ili mutoe Nusrah (Msaada) yenu kwa Hizb ut Tahrir ili kusimamisha Khilafah Rashida. Sio njia pekee ya ushindi katika hali halisi ya sasa. Badala yake, ni kwa sababu ni faradhi kubwa ya daraja ya kwanza. Kwanza kabisa, yeyote asiyefanya kazi na hali ana uwezo wa kusimamisha Khilafah, na kumsimamisha Khalifa ambaye anastahiki Bayah (ahadi ya utiifu), basi dhambi yake ni kubwa kama kwamba amekufa kifo cha kabla ya Uislamu (Jahilliyah), ikidhihirisha ukali wa dhambi hilo kama alivyo sema (saw):
«وَمَنْ مَاتَ وَلَيْسَ فِي عُنُقِهِ بَيْعَةٌ، مَاتَ مِيتَةً جَاهِلِيَّةً»
“Yeyote anayekufa na hana shingoni mwake bay’ah (ahadi ya utiifu), amekufa kifo cha kijahiliya (zama kabla ya Uislamu).” [Muslim].
Pili, Waislamu walichukua kiapo cha Bayah kwa Khalifa, kabla ya kuanza maandalizi ya mazishi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) na kutekeleza wajibu wa mazishi yake. Yote hayo yanatokana na umuhimu wa Khalifa.
Tatu, Umar (ra) siku ya kifo chake, aliweka kikomo cha muda, cha siku tatu na si zaidi, kwa ajili ya kumchagua Khalifa miongoni mwa wale sita waliopewa bishara ya Pepo. Ikiwa hakuna makubaliano yaliyofikiwa kuhusu Khalifa, ndani ya kipindi hicho, basi mpinzani alipaswa kuuawa. Hili lilikuwa katika mkusanyiko wa Maswahaba (ra) ambao hakuna uovu wowote ulioripotiwa kuwahusu. Hivyo, ikawa ni Makubaliano ya pamoja ya Maswahaba (ra). Hata hivyo, kwetu sisi, “siku tatu nyingi sana” zimepita juu yetu! Hakika kusimamisha Khilafah ni jambo kubwa.”
Na hitimisho la hitimisho lilikuwa ni kusema kwake, Mwenyezi Mungu aongoze hatua zake: “Enyi askari wa Mwenyezi Mungu: Tunatambua kwamba Malaika hawatashuka kutoka mbinguni kutuwekea Khilafah. Bali Mwenyezi Mungu (s.w.t.) atatuteremshia Malaika watusaidie tu ikiwa tutafanya kazi kwa bidii katika kusimamisha Khilafah. Ni ahadi iliyothibiti katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu.
[وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ ءَامَنُوا مِنْكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ]
“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao” [An-Nur 24:55]. Ni bishara njema ya izza, baada ya utawala huu dhalimu, katika hadith ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (swt),
«ثُمَّ تَكُونُ مُلْكاً جَبْرِيَّةً فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ»
“...Na kisha utakuwepo utawala wa kutenza nguvu, na utakuwepo kwa muda atakao Mwenyezi Mungu uwepo kisha atauondoa anapotaka kuuondoa, kisha itakuwepo Khilafah kwa Njia ya Utume.” Kisha (saw) akanyamaza. [Imepokewa na Ahmad]. Pia tunatambua kwamba maadui wa Uislamu wanaona kusimamishwa tena Khilafah ni jambo lisilowezekana. Wanarudia kauli ya wasaidizi wao miongoni mwa wanaofanya kejeli,
[غَرَّ هَؤُلَاءِ دِينُهُمْ]
“Watu hawa dini yao imewadanganya.” [Surah Al-Anfal 8:49]. Lakini kama vile msemo huo ulivyokuwa laana kwa wale waliotangulia kusema, kwani Mwenyezi Mungu ameitukuza Dini yake na akawapa ushindi watu wake, ni laana pia kwa wale wanaosema hivyo leo, kwani Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Mwenye hekima, yuko pamoja na waja wake waaminifu wanaofanya kazi kwa bidii, bila ya kuachana katika nyoyo zao na viungo vyao, na kauli ya Mwenyezi Mungu (swt),
[إِنَّ اللَّهَ بَالِغُ أَمْرِهِ قَدْ جَعَلَ اللَّهُ لِكُلِّ شَيْءٍ قَدْراً]
“Hakika Mwenyezi Mungu anatimiza amri yake. Mwenyezi Mungu kajaalia kila kitu na kipimo chake.” [Surah At-Talaq 65:3]. Kila kukicha, wanazidi kukaribia Qadr "azma" hii, kwa Idhini ya Mwenyezi Mungu (swt).
[وَيَقُولُونَ مَتَى هُوَ قُلْ عَسَى أَنْ يَكُونَ قَرِيبًا]
“na watasema: Lini hayo? Sema: A'saa yakawa karibu!” [Surah Al-Israa 17:51].”
Ewe Mwenyezi Mungu, uteremsha wito huu wa Amiri wetu katika nyoyo za majeshi ya Ummah wetu, na uzifanye nyoyo zao zimtamani, ili wampe nusra ya kusimamisha tena jengo la izza ya Uislamu, na turegee kama Mola wetu Mlezi alivyotutaka na kututaja kuwa ni umma bora ulioletwa kwa ajili ya watu.
.[إِنَّ ذَلِكَ عَلَى اللَّهِ يَسِيرٌ]
“Hakika hayo kwa Mwenyezi Mungu ni mepesi.” [Al-Hajj 22:70]
Imeandikwa kwa Redio ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Muhammad Abdul Malik
Fuatilia na Usambaze Alama Ishara za Kampeni:
#Time4Khilafah |
#EstablishKhilafah |
#ReturnTheKhilafah |
#TurudisheniKhilafah |
#KhilafahBringsRealChange |
#بالخلافة_يحصل_التغيير_الحقيقي |
أقيموا_الخلافة# |
كيف_تقام_الخلافة# |
#YenidenHilafet |
#HakikiDeğişimHilafetle |