Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Chini ya Mfumo Uliofeli wa Kirasilimali, Wakristo Wanakuwa Mawindo Rahisi ya Wahalifu

(Imetafsiriwa)

Habari:

Polisi wa Kenya walimkamata mwinjilisti wa televisheni wa Kenya mwishoni mwa Aprili, 2023 na kufikishwa mahakamani Ijumaa tarehe 28 Aprili 2023 baada ya ripoti za "mauaji ya halaiki ya wafuasi wake," Waziri wa Mambo ya Ndani Kithure Kindiki alisema, huku mamlaka zikichunguza vifo vyengine vingi vinavyohusishwa na ibada za kundi la kidini kutoka eneo hilo hilo. Huku habari za kuzuiliwa kwa Mchungaji Ezekiel Odero zikienea, maafisa walisema idadi ya waliouawa Shakahola sasa imefikia 110 katika uchunguzi wa kundi tofauti la kidini ambao umelishtua taifa na kusababisha wito wa kufanywa msako kwa makundi ya kidini.

Maoni:

Ulimwengu unapoamka na habari hizi za kutisha, idadi ya miili iliyofukuliwa hadi sasa ni zaidi ya 110 huku watoto wakiwa ndio wengi wa waliofariki. Watu wengi wanaanza kujiuliza ni kwa jinsi gani watu wanaweza kufikia kiwango hiki cha kufa kwa njaa ikiwa ni pamoja na watoto wao wachanga kwa imani ya "kukutana na Yesu" au kitu chengine kilichopangwa ambacho kingeweza kuwa sababu ya uhalifu huu wa kinyama. Ama kuhusu sababu ya pili ni njama zaidi kuliko uhalisia, kwa sababu nyepesi ya madhehebu katika Jumuiya ya Wakristo ya aina hiyo ambapo wafuasi wanauawa kwa wingi ili kuamini kupata uzima wa milele ilitokea katika historia yake yote.

Ili kuwa na utambuzi bora wa tukio hili la kusikitisha na lisilo stahiki, lazima tujizungushe na uhalisia wote ikiwemo hali ya kijamii na kisiasa ambayo imewezesha hili. Siasa inafafanuliwa kuwa ni sayansi ya kudhibiti uhusiano wa kibinadamu na yote yanayotokana na uhusiano huu ikiwa ni pamoja na mihemko k.m., furaha, huzuni, simanzi, msongo wa mawazo na fahamu kama matumaini n.k. Leo matumizi mabaya ya dawa za kulevya na ulevi yanaongezeka kama vile mzazi mmoja katika familia malezi ya watoto, na vilevile ongezeko la umaskini na ukosefu wa ajira unaoambatana na kufeli kwa uongozi wa kisiasa kama ilivyo kufeli kwa idara ya mahakama. Kwa maneno mepesi mfumo wa kiitikadi (URASILIMALI) uvurugika na wanadamu wametumbukia katika dimbwi la ukosefu wa matumaini na hatimaye kuwa mawindo ya wahalifu waliojigeuza kuwa "WATU WA MUNGU".

Pia, hii inaonyesha itikadi ya Kikristo haiafikiani na umbile la mwanadamu, yaani, ukosefu wa uongofu na kugongana na umbile la mwanadamu. Uislamu ndio itikadi pekee inayoafikiana na umbile na akili ya mwanadamu. Mfumo wa Kiislamu humuongoza mwanadamu kuishi chini ya sheria za Mola wa Rehema ambazo ziko ndani ya mipaka ya uwezo wa mwanadamu. Mfumo unaomuepusha mwanadamu na madhara na maovu yanayoweza kuanguka katika maisha yake.

[وَمَا أَرْسَلْنَٰاكَ إِلَّا رَحْمَةً لِّلْعَالَمِينَ]

“Nasi hatukukutuma ila uwe ni Rehema kwa walimwengu wote.” [Al-Anbiya: 107]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Ali Omar

Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Kenya

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu